Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Assignment kama hizi unazotoa unadhani lini miye nitaketi na kutazama Drama za mjini?!
 
Wakuu habarini sana..... Nilikuwa nashida na app au nielekezwe jinsi ya kudownload Korean dramas kwenye PC.......
 
Kwa Sasahiv hamna drama kaliiii eh?
Natizama Mother of mine dah napenda uhusika wa TJ kwingine naruka ruka, Fiery Priest Yan sio ya kukosea usingizi nilianza Banker naona ina wahusika weng epi. 2 za mwanzo ntairudia tho. Na Waikiki Kuna vitu vinafanana na 1st dah. Au my Mood na Korean iko down kwa sasa
 
Nimefanikiwa kuitazama episode 1, inavyoonyesha ni ya 2004-2003,lakini ipo vizuri.
Nimejiongezea Mzigo wakati sijamalizana na Great King na Jeong do jeon
 
Nimefanikiwa kuitazama episode 1, inavyoonyesha ni ya 2004-2003,lakini ipo vizuri.
Nimejiongezea Mzigo wakati sijamalizana na Great King na Jeong do jeon
masahihisho:
mkuu ni ya mwaka 2000 na si 2003/ 2004.
nyakati hizo iligonga rate ya 60% kwa kuangaliwa zaidi nchini korea, si unajua tena ilikuwa ni mwendo wa TV za serikali.🙂🙂
 
Shukrani sana mkuu kwa taarifa hizi nzuri......bahati nzuri katika kustruggle nimefanikiwa kuweka mambo sawa aiseh....
 
[QUOTE="Daemusin
2020 presidential election
nimesikia kuna timu uchwara zikiongozwa na maembe mabichi, lipumbavu, mzito mwepesi, kitundu kidogo na wengineo wameshaanza vikampeni uchwara kwa dhumuni la kurithi madaraka ya Tanzania Bank.

nimebaki nawacheka muda huu kama katuni ya zootopia, sina haraka ya kuingia uwanjani na mshambuliaji wangu machachari anayevuruga pande zote bila ya kuangalia sura ya adui haijalishi mpinzani ana kichogo, kichwa bapa kama ng'ombe, masikio kama panya n.k

kama walalahoi wa tanzania bank mumechoka kuongezewa interest rate, kama mumechoka kushuhudia benki yenu inatumika kutakatisha fedha chafu za wanasiasa uchwara pamoja na wafanya biashara basi ni muda muafaka wa kumshawishi baadae kumpigia kura auditor noh dae ho kupitia vita ya uraisi.

kwa nini tumchague?
  • kwa sababu ana ndevu kama sefu wa pemba.
  • ana elimu kama alivyo lipumbavu.
  • ana sifa ya kujua kuchanga karata zake kama maembe mabichi.
  • si muoga wala mkurupukaji kama mfungaji aliyesahau kula daku hatimaye akaamka saa 11 za alfajiri huku chipsi kuku zikiwa bado hazijaliwa
  • ukitaka mijadala ya jazba pia anaweza kuliko tundu dogo la kupitishia maji machafu
  • hana sifa za kijinga kama juma soda mzee aliyenunua kunguru 10 wasioliwa.

kama bado munataka kuendelea kutafuta maji ya kuosha nyuso zenu kwa kutembea kilomita 10 kama wehu basi wachagueni wanasiasa uchwara, lakini kama munataka kuyafaidi maisha na kushuhudia.
mgombea pekee asiyekabia( kuchomekea) koti kama alivyofanya mzee hassira
mifereji kutoa maziwa ya kondoo,
umeme wa sauti,
kila mtanzania kumiliki private jet,
kila mtanzania kukoga mara tano kwa siku kama samaki
hatolala na nyinyi mbele wala nyuma kama bwana yule anavyotishia
wanaume wote kubarikiwa nguvu za kiume bila ya kutumia vumbi la unguja
wanawake wajawazito kuacha kula udongo mwekundu kama jongoo (millipedes)
wafugaji wa kimasai wote kumiliki magari ya kupakia ng'ombe zao pindi wanapoelekea mipaka ya nchi nyengine
wachaga wote kutoa michango kwa fedha zao kama mzee regina kidogo (nimemnukuu madaladala).

nawaomba ifikapo october 2020 mumchague auditor noh dae ho kupitia chama cha hatulali na njaa milele.
je kina dada mutampaaaaa
je ma ahjumma wote mutampaaaaaaa
wanaume mutatoaaaaaaaaa japo kwa siriii
nimekusudia kura jamani

team kampeni itaongozwa na damushin bin makinikiyya bin noah bin DED bin korooshooo.
napokea michango kuanzia leo.​
==================================================================================================

hii wiki imekuwa ya furaha sana kiupande wangu kwa sababu kwa mara ya kwanza tokea nianze kufuatilia korean drama kama kumbu kumbu zangu zipo sahihi nimeshuhudia drama mbili zinazoonyeshwa na vituo tofauti kumaliza kwa siku moja.

finally nimemaliza kuangalia the banker drama, hatimaye auditor noh dae ho a.k.a professor assad amefanikiwa kumuangusha president kam sang do ambaye ni raisi aliyedumu kwa muda mrefu kwenye daehan bank.

daebak, ilikuwa ni vita ngumu sana kuliko vita kati ya simba na bwana mtembeza bakora kwa wapinzani wake jimboni (code nyepesi hii)

likizo yangu inakuja muda si mrefu.
ramadhan kareem
View attachment 1101984
[/QUOTE]
huyo mzee wa kushoto bado nina mfaidi huku kama Mfalme 대조( Taejo/tejo) cha kushangaza Yi Bangwon ( 이 방원) ndo anaanza harakati za kuchukua Nchi, Confucious scholar( Ha- ryun) anamfanyia mipango Bangwon, wakati upande wa Pili huku Ha ryun kalazimishwa kujiuzulu na Mfalme 대종( Lee Bangwon) .mbali zaidi Sejong the great ameshika nchi but hana nguvu, mshua wake bado yuko powerful licha ya kujiuzulu.
We acha tu ni uhondo baada ya uhondo, cha kuvutia drama zote hizi mbili zimeshea washiriki kwa asilimia 80. Hata hii niliyoianza ni mulemule.
 
Nimetimiza siku 380 tangu nilipojiunga Jamvini. Majukwaa niliyowahi kubandika nyuzi ni la kimataifa, Intelligence, Hoja mchanganyiko. Since nilipoingia kwenye uzi huu mwezi wa 11, sijawahi kuyatembelea majukwaa mengine.
 
Aigoo sunbaenim, nini mbaya? Sio kwa povu hilo. Kwani huyo binti ana kasoro gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…