nimekuja kwa ajili yako chingu japo kwa siku mbili (leo na kesho), umekuwa ni mshirika mkubwa kwangu ndani ya hii thread kwa miaka miwili mfululizo, bila ya comment yako ambayo nimeipuuzia tokea jana nisingeliwajibu hao wahuni uchwara wa bodi ya mapato hapo juu
😀 😀.
hongera kwa ubingwa wa bara la ulaya, ubingwa wa Tanzania na pia nikupe hongera kwa kuwasaidia watani zako wa jadi yanga wapate nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao, rafiki wa kweli ni yule aliye tayari kumsaidia mwenzake pindi anapokuwa na matatizo, simba mumethubutu kufanya hivyo.
hongereni sana.
angels last mission drama: nimeipenda sana nimejikuta natamani niwe malaika muda huu, maisha ya ubinadamu yameshanichosha.
one spring night drama: hadithi yake inakwenda taratibu sanaaa lakini ipo vizuri, kila mmoja anaogopa mahusiano mapya ya kimapenzi, cha kushangaza wote wawili wameshaelezana siri za maisha yao wanayoyapitia na walioyapitia.
the nokdo flower drama: historical drama ya ukweli bado naendelea nayo, general Jeon Bongju alikuwa ni great thinker wa ukweli tuache utani kwa hii mikakati yake. dah jamaa maisha yake yaliishia mikononi mwa wajapani. cha ajabu Korea bado imeendelea kuwa ni nchi dhaifu sana licha ya kupata kwao uhuru.wakorea walikuwa dhaifu sana jambo lililopelekea nchi za kigeni ziigeuze ardhi ya korea kuwa ni uwanja wa kujaribu nguvu zao, kwa wapenzi wa historical drama hiki chuma kinawahusu imeshafika episode ya 14.
arthdal chronicles: wanasema wakorea wameiba idea nzima ya games of throne series, sifahamu kama kuna ukweli wowote au la kwa sababu si mfuatiliaji wa american series, kwa aliyeangalia hizi project mbili naomba atusaidie tafadhali. Nikipata muda nataka niziangalie tena episode mbili za mwanzo kwa umakini nipate kuielewa zaidi baadae kama nitapata muda nije niisifie au kuiponda humu ndani. tuache utani yule binti anayeitwa kim ji won ni mrembo wa ukweli, ni mimi pekee ninayeamini ya kwamba song jong ki ni overrated actor au mwenzenu itakuwa nina wivu naye?
different dreams: bado naendelea kujifunza harakati za kupigania uhuru wa korea, mgawanyiko wa korea ulikuwa hauepukiki kwa sababu ukiangalia haya makundi ya harakati za uhuru yalikuwa mengi kama zanzibar. hivi yule mwanadada
lee yo won ni kweli ana miaka 38, hizi makeup zinaweza kumfanya
Daemusin awe na sura ya magufuli.
mwisho nimalizie my love chingu na wengineo naomba munipunguzie notifications ifikapo siku ya jumatatu, za leo na kesho nitajibu but ikianza wiki mpya sitojibu, nawaomba sana munisaidie kwa hili ombi nililoliwasilisha kwenu kwa wote jamani.
hii comment sitoifuta ili wadau wote waione humu ndani.
Oh bird, oh bird, oh roller
Do not sit in the Nokdu fields
For when the Nokdu flower falls
The jelly seller weeps.
Oh bird, oh bird, oh roller
Why did you come out
For the pine and bamboo leaves are green
We thought it was summer
But it is freezing with snow
roller = wanajeshi wa japani waliokuwa wanavalia fomu blue.
Nokdu fields = jeong bong jun mkuu wa mapinduzi ya donghak peasant
when the Nokdu flower falls = kunyongwa kwa jeong bong jun
jelly seller = wafanya biashara wadogo wa korea (joseon), au walalahoi wanaotegemea zaidi kilimo na biashara dhaifu
Why did you come out = malalamiko ya peasant wa korea dhidi ya uvamizi wa nchi za kigeni nchini kwao.
mashairi hayo yalikuwa maarufu sana nyakati hizo za
donghak peasant revolution nchini joseon mnamo karne ya 19.
aminas huyu malaika wetu amepewa mpaka zawadi ya sauti nzuri