Jang bo ra
Member
- Nov 24, 2018
- 67
- 159
TelegramDramania inazingua msaada wa app nyingine kama hii ya dramania
Rookie Historian Goo Hae Ryung Daemusin Ost Zake Ni Balaa Hasa My Dream By Yoonmirae..
Bogoshipo Chingu Sana Sana.
Uje Basi Twende Busan.
Juzi Wakati Naiangalia, Nikakumbuka Ule Usemi Wako Na Hiki Ulichoandika Apa.jewel in the palace, dong yi, jang hee bin, jang ok jung drama.zote hizi zilikuwa zinaelezea historia za wanawake ikiwemo mafanikio yao pamoja na changamoto walizokutana nazo ambazo baadae walizigeuza kuwa ni fursa, lakini ukiziangalia drama zote hizo kwa umakini simulizi zake utagundua ya kwamba kwa kiasi kikubwa sana watengenezaji wa project hizi waliendelea kumfanya mwanamke awe chini ya kivuli cha mwanamme kiutegemezi.
inanilazimu nikiri ya kwamba hizo project zote nilizozitaja hapo juu hakuna hata moja niliowahi kuiangalia hivyo basi kama nitakuwa nimeteleza kifikra na mtazamo basi nipo tayari kusahihishwa kwa lugha safi isiokera na mdau yeyote.
Rookie Historian Goo Hae Ryung drama nayo pia sijawahi kuifuatilia hata episode moja lakini baada ya kusoma maoni ya wadau mbali mbali kupitia vyanzo tofauti na kuangalia short videos nimejifunza ya kwamba hii ndio drama pekee ambayo imemuandika mwanamke kama ndiye muhusika mkuu halisi wa hadithi ukilinganisha na drama hizo hapo juu nilizozitaja ambazo kwa kiasi kikubwa mission nyingi zilikuwa zinafanywa zaidi na mwanamme.
chingu, bado nipo kwenye mgomo wa kuingiza project mpya kwa sasa hivyo basi hii drama acha kwanza iende pengine huko mbeleni naweza kubadili msimamo.
goo hae ryung ndiye wa kwanza kuziweka wazi hisia zake za kimapenzi kwa mwanamme ambaye ni mtoto kutoka royal family, si hilo tu pia mwanadada ndiye wa kwanza aliyeanza kuonyesha uthubutu wa kutamani kumbusu (kiss) mwanamme, cha ajabu unapozifuatilia hizo drama nyengine zenye kutuonyesha ushujaa wa mwanamke zimejaribu kutuwekea ukomo wa matendo ya mwanamke anayopaswa kuyatenda kana kwamba ni dhambi kwa mwanamke kuyatenda matendo hayo jambo ambalo linamfanya mwanamke abebe sifa za parasite wa hisia (amsubiri mwanamme adhihirishe hisia zake ndipo naye afuate mkondo kama maji ya mto ruvuma) nyakati ambazo bwana mdogo anatengeneza mipango ya kumtokea hae ryung na bidada pia naye amekuwa akisuka mipango yake ya kutamani kuwa na mwana wa mfalme, ni nadra sana kuona mwanamke anaziweka wazi hisia zake za kimapenzi kwa mwanamme kuanzia kwenye maisha ya maigizo hadi kwenye maisha halisi labda kwa kuhofia jamii itamchukulia kama ni mwanamke asiyeiheshimu thamani yake.
View attachment 1189845
teh teh teh nimeona leo ndio siku nzuri kujibu hizi comment.Kapo yenu iko lit mno.. Mwaendana!! Hope hayataishia humu
alikuwa anajifanya maitreya (buddha mpya) kumbe ni mshenzi aliyekuwa anajificha kwenye kivuli cha dini.Loo! Wakati King Goonyae( Sujong) yeye alilazimishwa na kwa nguvu mno kuoa, Jamaa alikuwa hapendi wanawake yule, alikuwa anahisi ni kama watu ambao wametanguliZa hisia badala ya mantiki.
kwa mujibu wa drama mtoto wa kwanza kuzaliwa na wang guhn pamoja na mke wake wa kwanza alifariki dunia ndipo baadae mke wake wa pili ndio akafanikiwa kumzalia mtoto mwengine aliyeitwa wang mu a.k.a mfalme hyejeong.Msimulizi anadai huyo binti wa mfanyabiashara wa Geumsung ndiye aliyemzaa mrithi wa Wang guhn.
wakorea wanachosha ndio maana tunabadilisha stori baadhi ya nyakati.Msituletee mambo ya Liver huku ninyi
@aminas kumbe tupo pamoja kwa Liverpoolteh teh teh nimeona leo ndio siku nzuri kujibu hizi comment.
bwana davinci kwa mara nyengine tena umekalia ukuwadi juu yangu na aminas.
sidhani kama tunaendana kitabia kati yangu mimi babu mtarajiwa na huyu ahjumma mtarajiwa baada ya miaka 20 kwa sababu:
- anapenda simba sports club wakati mimi napenda ile timu kutoka mozambique a.k.a msumbiji inayoitwa UD Songo pamoja na yanga
- anapenda liverpool fc wakati mimi napenda man utd pamoja na everton fc.
- anampenda haji manara na maneno yake ya ovyo na hajiwezi kukaa bila ya kusoma comment zake wakati mimi nachukizwa na tabia zake anazoziwasilisha kwa njia ya uandishi (tabia za dharau na ujuaji mwingi)
- anajua kuzungumza kiingilishi wakati mimi hata kuandika barua rasmi kwa kiingilishi kunanipa tabu mpaka nitembelee gogoli.
ni mshabiki lia lia wa captain henderson@aminas kumbe tupo pamoja kwa Liverpool
Ndiowakorea wanachosha ndio maana tunabadilisha stori baadhi ya nyakati.
kwani huko nyumbani kwako unapika ugali kila siku?
Hapo tu ndio tunapishanani mshabiki lia lia wa captain henderson
Jamaa( Sujong) na mshikaji wake( Advisor) jamaa wanaonekana wakatili 100%, halafu maovu yao wanayaficha kwa kujichekesha kila mara, walinikera walipomuua Madam Bukwon( binti wa General Yangil), kiukweli hiyo miamba ilikuwa mikatili.alikuwa anajifanya maitreya (buddha mpya) kumbe ni mshenzi aliyekuwa anajificha kwenye kivuli cha dini.
huyo mjinga aliichoma moto familia yake hadharani akiwemo mke wake na watoto wake wawili mapacha.
baadae alikuwa mkatili sana ndio maana wafuasi wake wakaribu wakaamua kumpindua kwa kumtumia general wang guhn ambaye alimchukulia kama ni mdogo wake wa kupanga.
Nimeangalia king gwangaetto na dae joyoung, gwangaetto ina mission nyingi za battle lakin dar joyoung ina hassle nyingi,binafsi dae joyoung ni moto,
Wakuu dramania yng inafanya ivi nikitaka ku donwload ni zote au yng tu haliti chochote na hata uki lazimisha ina feli tu ni week ya 3 sasa View attachment 1189916
hhhhhhsina cha kuongeza kwenye andiko lako na kama ni mtihani umeramba 10.
huo msemo wa akili ni nywele kila mtu ana zake nauchukia sana, ina maana sisi tuliojaaliwa na nywele kipilipili ndio uwezo wetu wa kufikiri utaendela kuwa mdogo kama nywele zetu?