Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

cjaziona "waikiki 1" na "the sound of your heart" ila naambiwa hizo drama ni kucheka tu mwanzo mwisho.....alieuliza drama za genre ya comedy ajaribu hizo, kupata full comedy ni ngumu nyingi ni rom-com
 
Ndiyo kwanza nipo sehemu ya 3.
Hawa wahuni ndiyo mastelingi wetu?!
"AGE OF WARRIORS"

Ila Hisia zangu zinanisukuma kama huyu Ui Bang na washkaji zake ndiyo mastelingi.
Kwako Daemusin
we bwege kutoka kolomijee ukisikia age of warriors ndio hiyo, hapo ni mwendo wa kutuonyesha mtiririko wa matukio yote ya dikteta mmoja moja kubeba madaraka, cha kuvutia anajitokeza dikteta mwengine anayejificha kwenye mwamvuli wa kuwapigania raia haki zao na kuanzisha harakati za kumpindua mwenzake, kichekesho zaidi akishafanikiwa kumuangusha mwenzake na yeye anakuja kuyatekeleza zaidi ya yale aliyoyafanya mwenzake.

madaraka ya kijinga ni matamu kuliko maziwa ya mnyama paka lakini yanalevya kuliko sumu inayotengenezwa na mpenda sukari, utakufa na utamu wako kama unakula visheti vya harusini.
  • hao wahuni wanampindua mfalme na kuondoa civillian government baadae wanamweka mdogo wake ili wasionekane wamefanya tendo hilo kwa nia chafu kwa amri ya queen dowager.​
  • yi uibang: huyo mzee aliyeigiza uhusika wa yi uibang utamuona kwenye emperor wang guhn ambapo ameigiza uhusika wa mfalme kyu hyun from later baekje. Madaraka yanamtia upofu kiasi ambacho alifikia hatua ya kuwasambaratisha marafiki zake wawili muhimu ambao kwa muda mrefu walikuwa na ndoto kwa pamoja ya kuinyoosha goryeo iliokwisha poteza muelekeo. kuanzia mwaka 1170 hadi mwaka 1174 jamaa ndiye aliyekuwa ameshikilia mpini wa maamuzi ndani ya goryeo, karma is bitch bwana yi ui bang alikufa kifo cha aibu sana. Aliyemuua ni mtoto wa jeong jung bu.​
  • jeong jung bu: kifo cha bwana yi ui bang kilipelekea kubadilika kwa upepo hatari wenye uwezo wa kuvunja ghrofa za burji khalifa, ukoo wa yi ulipoteza nguvu na hatimaye ukoo wa choe ukashikilia nguvu ya kuiendesha royal family. Huyu mzee kwa kushirikiana na mwanawe walitenda matendo zaidi ya yale aliyoyatekeleza yi ui bang. Karma is bitch baadae alijitokeza bwana mdogo ambaye inasemekana alikuwa na miaka 26 tu ya kuzaliwa na jina lake aliitwa gyeong dae sung, huyu general ndiye aliyeongoza kampeni ya kumuondoa madarakani jeong jung bu na koo yake nzima. hatimaye jeong jung bu, mwanawe, mkwe wake na kizazi chote kinachotokea koo ya choe walikutana na mkono wa kifo. jeong jong bu alishika madaraka kuanzia mwaka 1174 hadi mwaka 1179.​
  • gyeong dae sung: alichukiwa mnooo na mfalme, vitabu vya kihistoria vya joseon havikumrekodi vibaya huyu jamaa. hakuwa na uchu wa madaraka na alijaribu kurudisha mfumo wa serikali kama ilivyokuwa mwanzoni (civillian govenrment) lakini alikutana na upinzani mkali sana kutoka kwa wanajeshii na hata mfalme mwenyewe, jamaa inasemekana alifariki kwa ugonjwa. Hii drama nimeiacha episode ya 95 ambapo tayari jamaa anasumbuliwa na maradhi yanayotishia uhai wake na alitawala kuanzia mwaka 1179 hadi 1183.​
  • yi ui min: huyu muhuni ndiye aliyemuua mfalme wa mwanzo kwa amri ya bwana yi ui bang, cha kuchekesha zaidi amri ya kifo ilitoka moja kwa moja kwenye royal family ndani ya chumba cha queen dowager (yaani queen dowager alitoa amri ya kuuliwa mwanawe wa kumzaa kwa mujibu wa drama), huyu fala na yeye aliyatumia madaraka yake vibaya sana pamoja na watoto wake wawili wakorofi kiasi ambacho hakuona tabu kuwanyanyasa kingono watumishi wa royal family, kudhulumu mali za walala hoi, Yi ui min maisha yake yaliishia mikononi mwa jamaa mmoja anaitwa choe chung heon. Yi ui min alitawala kuanzia mwaka 1183 hadi mwaka 1196.​
hao ndio main characters wa hiyo drama mpaka nilipofikia episode ya 95, baadae wanakuja wendawazimu hawa:
  • choe chung heon: baada ya kufanikiwa kumsambaratisha bwana yi ui min hatimaye jamaa akawa ndiye bosi mkuu wa goryeo, huyu jamaa pamoja na ukoo wake waliitawala goryeo kwa muda mrefu sana kwa njia ya kurithishana madaraka (baadae walitawala watoto wake choi woo, choi hae, choi ui).​
  • kim jun: kama umefanikiwa kuiangalia god of war drama mule ndani wamejaribu kuelezea vizuri sana historia ya kim jun, kwa mujibu wa ile drama jamaa alikuwa ni mtumwa ambaye alipata mafunzo ya kijeshi kwenye hekalu la kibuddha. Kim jun ndiye aliyefanikiwa kuisambaratisha koo ya choe na hatimaye jamaa akawa ndiye mwanadamu mwenye nguvu kubwa ya kimaamuzi ndani ya goryeo, nyakati hizo tayari Mongolia walishaanzisha kampeni ya kuiangusha Goryeo.​
  • Im yeon: huyu bwenge ndiye aliyemuua kim jun mnamo mwaka 1268.​
  • Im yu mu: ni mtoto wa Im yeon na alitawala mwaka 1270 baadae akapinduliwa na kunid fulani linaitwa sambyeolcho kwa amri ya utawala wa mongolia, hatimaye zama za mashujaa zikaishia hapo (age of warriors).​
utabaki unajiuliza wale waandishi wababe wa stori ndefu kama hizi ndani ya korea wamekwenda wapi?

bwana Great Conqueror umeshafanikiwa kumuona mwanamme handsome boyiii humo ndani?
zawadi nono nimekuwekea pindi ukimuona mrembo wa kiume.
pengine kwa kutumia hii picha unaweza kumuona handsome boyiiiiii.
1569918050227.png

yi ui bang akishika rungu lake anakuwa mwehu zaidi ya kipepe.
yi ui min akishaikamata shoka yake anakuwa mwehu zaidi ya mkataji miti ya kuchomea makaa.​
 
Ahsante mkuu kwa masahihisho.

Nilidhani ndugu muuliza swali alihitaji ushiriki mwingine wa Yeong-po, yule wa kwenye Prince of Legend (Jumong) ama kwa jina lake halisi la Won Ki-jun ambaye ameshiriki pia katika hiyo Gu Am Heo Joon 'Remake' ya mwaka 2013. Ila kama ni mzee Jeong Gwang-leol, Yeah! upo sahihi kuwa ameigiza 'Orijino' Gu Am Heo Joon ama Heo Joon ya mwaka 1999.
ok, kumbe nilikuelewa vibaya.
upo sahihi ndani ya guam heo joon aliigiza uhusika wa kaka yake heo joon kwa mama tofauti, mama yake alikuwa anatokea ukoo wa mboga saba tofauti na mama yake heo joon ambaye alikuwa ni mtumwa.

jamaa alikuwa anamchukia sana heo joon lakini ndio hivyo DR heo joon alikuwa ni zaidi ya genius aliyewahi kutokea kwenye huu ulimwengu wa kidaktari.
=================================================================================

yan Stuntman anawasumbua professional killer ni hatat...ila korean now wanaweka Netflix... Na sijui kwann hawafuati ile taaratibu ya Netflix kushusha mzigo wote..kwa siku moja...pia ni njia nzur kuliwin soko
ni sawa netflix wana haki miliki ya kuonyesha vagabond drama online, lakini SBS ndio wamiliki wakuu wa hiyo project na kwa mujibu wa ratiba zao wanaionyesha vagabond kwa siku ya ijumaa na jumamosi usiku kwa saa za korea.
 
Shukrani mkuu, ngoja nianze na "I'm not a robot"
Duh! kukutajia Comedies 5 nzuri ndani ya kipindi hicho kifupi cha 2018/2019 ni 'Limited' kimtindo maana nzuri nyingi zipo ila katika miaka tofauti tofauti kuendana na mitazamo ya kila mdau katika tasnia.

Mfano, kuna hiyo uliyoitaja hapo, 'Come Back Mister' ni Comedy nzuri sana ila ni ya mwaka 2016. Pia kuna 'Kill Me Heal Me' ya mwaka 2015 ambayo pia ni moja ya Comedies nzuri "kwa maoni yangu".

Nyinginezo ni;
  • Legend Of The Blue Sea (2016-2017)
  • Suspicious Partner (2017)
  • Introverted Boss (My Shy Boss) (2017)
  • Welcome To Waikiki (2018)
  • Strong Woman Do Bong Soon (2017)
  • I'm Not A Robot (2017-2018)
Na kuna nyingine ya kitambo kidogo, 'Master's Sun' ya mwaka 2013.
 
aliyenisukuma kwa nguvu za ajabu hadi kwenye thread hii kwa siku ya leo ni mwanadamu anayeitwa song il kook / gook / kuk / guk/ song 1958
tarehe kama ya leo mnamo mwaka 1971 ndio siku aliyotoka ndani ya kiwiliwili cha mwanamama mtemi anayeitwa kim eul dong ambaye ni muigizaji wa zamani na pia ni mwanasiasa aliyeshindwa kurudi mjengoni kwa mara nyengine

mjukuu wa mbabe kim du han ambaye pia aliwahi kuwa mwanasiasa anayewawakilisha wananchi mjengoni kama ilivyokuwa kwa mwanawe kim eul dong.

kitukuu cha shujaa anayeitwa kim jwa jin a.k.a tajiri wa mali na tabia njema asiyesahaulika ndani ya ardhi ya korea, mpaka manowari za kijeshi zimepewa jina lake, mwanadamu wa mwanzo kuwanusisha harufu ya ushindi wakorea dhidi ya japani.
.

song il kook amenifanya niwe mlevi wa korean drama, song il kook ndiye muigizaji pekee mwenye sura zaidi ya 100 na
kama yupo mwengine naomba munitajie.

maisha ni kama mbio ndefu, unaweza kuachwa nyuma na wenzako kwa hatua ndefu sana lakini hupaswi kukata tamaa, ndivyo yalivyokuwa maisha yangu kwa sababu nimewashuhudia watu wengi wakinipita kimafanikio na wengine kunidhihaki lakini sikuwahi kukata tamaa.
(
maneno ya song il kook alipomaliza mbio za triathlon kwa msaada wa wanawe watatu miaka minne iliopita)

happy birthday ahjussi kwa kutimiza miaka 48 ya kimagharibi.

bodyguard drama.
jumong drama
lobbyist drama
a man called god drama
jang yeong sil drama
kingdom of the wind drama
fermentation family drama
album of life drama
jang hee bin 2002 drama
emperor of the sea drama
terms of endearment drama
detective in trouble drama.

dada yangu Nifah bado umeendelea kubaki na msimamo wako wa kusubiria mtoto mchanga adondoshe mguu wake upate kuutafuna kama simulizi za fisi?
unaonaje ukamtafuta mwengine kabla hujachelewa.
samahani kwa kukuita uchawini 😀😀😀

1569922030058.png
 
mwenye account hii hatokuwepo kwa muda ndani ya JF.
kampeni yangu ya kupunguza ulevi wa korean drama imeshika kasi zaidi, nimefunga vitabu vyangu vyote vya drama.
nakwenda likizo nikiwa nimeziacha drama zifuatazo.
  1. vagabond drama: nimeishia ep 2.
  2. when the camellia blooms: nimeishia ep 2.
  3. graceful family :nimeishia ep 10.

aliyepewa kapewa naapa hapokonyeki,
kwa alichojaaliwa wallahi hapunguziki,
wa tisa humpa tisa wa moja haongezeki,
alomyima kabisa pindi akitaharuki
mola mtoa hidaya yote kayamiliki

kwake ukiliya ng'o unajipatisha dhiki,
kwa aliemtunukia ndio yake haki
na asiye mtakia huwa si yake laini (foleni)
wewe ukifanya chuki
bure unajisumbua​

dah nimekumbuka taarab asilia za nyumbani kwetu.
wewe endelea kumchukia daemusin bin makinikiyya bin vipigo kwa mashangazi zenu bin msamaha wa raisi bila ya sababu ya msingi kama mlevi anavyomchukia mzinifu cha ajabu wote wanahonga fedha zao kwa njia tofauti.

ANYEONG.
huu wimbo ni dedication kwa mlevi mwenzangu zaidi, wapo walevi wengi humu ndani wa jinsia tofauti lakini mmoja tunaelekea kuendana haijalishi anapenda mikia FC na jogoo wa chato asiye na kizazi cha premier league

kim bum soo - bogoshipda (i miss you)
Stairway to Heaven (2003) drama ost
hivi kwa kiswahili ukitaka kumwambia mwenza wako i miss you unatamka vipi jamani.
nimekukosa
nimekumisi = kiswanglish
mimi kukukosa wewe.​

pumbavu zetu hii lugha ni dhaifu kama bunge la Tanzania na muhimili wa mahakama.
 
Nimekuhamu
 
Nimekukosa Pia!

Likizo Iyo Vipi Unaenda Wapi!?

Ndo Hutaki Kumuangalia Shemeji Wako Chang Wook Ni Nzuri Ile Drama Icheki Kwanza Ndo Uende Likizo Puleeeez.

Bogoshipseyo Chingu.
 
aliyenisukuma kwa nguvu za ajabu hadi kwenye thread hii kwa siku ya leo ni mwanadamu anayeitwa song il kook / gook / kuk / guk/ song 1958
tarehe kama ya leo mnamo mwaka 1971 ndio siku aliyotoka ndani ya kiwiliwili cha mwanamama mtemi anayeitwa kim eul dong ambaye ni muigizaji wa zamani na pia ni mwanasiasa aliyeshindwa kurudi mjengoni kwa mara nyengine

mjukuu wa mbabe kim du han ambaye pia aliwahi kuwa mwanasiasa anayewawakilisha wananchi mjengoni kama ilivyokuwa kwa mwanawe kim eul dong.

kitukuu cha shujaa anayeitwa kim jwa jin a.k.a tajiri wa mali na tabia njema asiyesahaulika ndani ya ardhi ya korea, mpaka manowari za kijeshi zimepewa jina lake, mwanadamu wa mwanzo kuwanusisha harufu ya ushindi wakorea dhidi ya japani.
.

song il kook amenifanya niwe mlevi wa korean drama, song il kook ndiye muigizaji pekee mwenye sura zaidi ya 100 na
kama yupo mwengine naomba munitajie.

maisha ni kama mbio ndefu, unaweza kuachwa nyuma na wenzako kwa hatua ndefu sana lakini hupaswi kukata tamaa, ndivyo yalivyokuwa maisha yangu kwa sababu nimewashuhudia watu wengi wakinipita kimafanikio na wengine kunidhihaki lakini sikuwahi kukata tamaa.
(
maneno ya song il kook alipomaliza mbio za triathlon kwa msaada wa wanawe watatu miaka minne iliopita)

happy birthday ahjussi kwa kutimiza miaka 48 ya kimagharibi.

bodyguard drama.
jumong drama
lobbyist drama
a man called god drama
jang yeong sil drama
kingdom of the wind drama
fermentation family drama
album of life drama
jang hee bin 2002 drama
emperor of the sea drama
terms of endearment drama
detective in trouble drama.

dada yangu Nifah bado umeendelea kubaki na msimamo wako wa kusubiria mtoto mchanga adondoshe mguu wake upate kuutafuna kama simulizi za fisi?
unaonaje ukamtafuta mwengine kabla hujachelewa.
samahani kwa kukuita uchawini 😀😀😀

Ngoja nikamtakie My Oppa Bae happy birthday mie, hakuna cha kubadili msimamo wangu huu.
Ill Gook Song is my forever Oppa Bae wa Korea, halafu anachotufanyia sio poa, haki nimemmissssss

BTW acha tabia yako yakufuta quotes zako kwangu dogo, nilikaa kimya zile nyingine ila ile ya juzi kwenye mabeki visiki nimesema hapana! Lazima nikuambie kama hivi [emoji4]
 
Jewel In The Crown (Dong Yi)
l_p0016601767.jpg

Drama bora kabisa kati ya nilizowahi kuzishuhudia.. Huyu jamaa Lee Byeong Hun ambaye ni mtayarishaji wa Tamthilia hii pia Amewahi kufanya Kazi nyingine nzuri ya kuitwa
Wind Of The Palace ( Yi San)
Hata hii Drama iitwayo
Jewel In The Palace( Dae Jang Geum)
atakuwa kutengeneza yeye sababu Hizi Drama zote Zimeshare wahusika kwa kiasi kikubwa sana.
 
My Country - Moto 🔥
Vagabond - Fire
The Tale of Nokdu - Fire
Melting Me Softly - Fire
Extraordinary You - 🔥

Zote Izo Ni Ongoing. Ndo List Yangu Kwa Sasa.
 
Back
Top Bottom