Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Hivi hii Arrow in the bowstring naweza kuipata online??
 
Bora umemjibu maana nilitakari ni utani au anamaanisha?
Baadae nikahitimisha kwa kudhania ni utani.

Mambo yanazidi kupamba moto huko Telegram, well done Daemusin [emoji1433][emoji1433][emoji1433]
Hata Usipate tabu, Nishajiunga huko Telegram.basi kuna muhuni anatupia vitu huko wacha niwe mpole mpaka zije zile nazopenda.
 
Hata Usipate tabu, Nishajiunga huko Telegram.basi kuna muhuni anatupia vitu huko wacha niwe mpole mpaka zije zile nazopenda.
na huyo muhuni anavyopenda sifa za kijinga tokea asubuhi ameikalia internet mpaka muda huu, hana muda hata wa kuwaza chakula inavyoonekana
ni mwendo wa kudownload na kuapload

kweli starehe gharama.

halafu sasa watu wenyewe mabubu au telegram hamuna kuchati?
anapost peke yake
anaongea peke yake
anajichekesha peke yake.
ndio maana naipenda JF, napata muda wa kuchati na mlevi kutoka pyongyang
teh teh teh
 

Wewe mtu sio mchezo, naweza kuimagine wale abandoned β€˜parasites’ wako wanaliaje? Sio kwa β€˜midrama’ unayotushushia kule [emoji1487][emoji1487][emoji1487]

Tatizo tukiruhusu chats pale aim ya Channel itapotea maana drama tutakuwa tunazitafuta kwa torch.
 
😁😁😁 Suala la msingi fanya kile kinachoifurahisha roho yako, Thamani ya maisha ipo ndani ya Furaha.
Wacha niendelee na muhuni wangu WANG GEON. sasa Empress Kang kachukia kweli kweli baada ya baba yake kuuliwa na Gung Ye.
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… Unadhani kuandika hicho kidhungu chako ulikuwa unanikomoa miye!!!!!. Sijasoma NG'O
 

Hahaha Panadol zinafaida sana kwenye mwili wa binadamu ( usiniulize faida hizo sababu miye si mganga). Lakini dawa hizo hizo zikitumika kupita kiasi zinageuka dawa za kulevya. Sasa wewe nakushauri mavi ya punda ni suluhisho la matatizo yako(usiniulize kuwa unashida gani).
 
β€œJuzi nimetembelea Hifadhi ya Katavi nimekuta viboko wanakaribia kufa hawana maji, sasa wakikimbilia huku msiwalaumu, kwanza viboko wale nawapongeza kwasababu wana akili sana(tuwapigie makofi) wamekuja wakae na nyinyi Mjini kwa sababu mmewazibia maji kule, TANAPA hawajachimba Mabwawa kule, nyinyi mmechimba Mjini na wao wamekuja, wakiwaua mnasema wamewafuata, eti mnataka kuwaua, kuwaua sio solutions wapeni maji”- JPM

========================================================
hilo jibu halijakutosha?
umeandika kama umevamiwa na kiboko
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… Hivi nani ambaye ameanza kuathirika kisaikolojia kama mimi sababu ya Historical Drama.
Mfano Ile tabia ya Kuweka mikono nyuma wakati wa kutafakari mambo kadha wa kadha.

Tabia ya kuguna kama Ma- General bado haijaniathiri.
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… Hivi nani ambaye ameanza kuathirika kisaikolojia kama mimi sababu ya Historical Drama.
Mfano Ile tabia ya Kuweka mikono nyuma wakati wa kutafakari mambo kadha wa kadha.

Tabia ya kuguna kama Ma- General bado haijaniathiri.
you have zero taste for modern drama.
kwa kiingilishi nimeandika sawa jamani, hii lugha naiogopa kuliko hadithi za popobawa lakini sikomi kujaribu kuandika porojo lake

hayo maisha unayoyapitia wewe ya kujimbwambafy na historical drama kiupande wangu nilishayapitia takribani miaka mitatu iliopita, baadae nikaacha ujinga

kila mara utamsikia muigizaji anaguna mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh utadhani anatoa choo kikubwa cha mapera machanga.

kila muda utamsikia eunuch anakimbilia kwa mfalme na kilio juu kama mtoto aliyenyimwa pipi "
pyehaaaaaaaaaaaaaaa (νν•˜) kuna uasi (banhang = λ°˜ν•­) unafanyikaaaaaa

tena mfalme utamsikia akijibu kwa sauti kubwa kama mwanamme mwenye hashuo la kufuatilia maisha ya watu.
niiiiiiiiniiiiiiiiiiiii ..............mwo (뭐) yooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

na usiombe ukamkuta general mshamba anamtongoza mwanamke mshamba, mama weeeeeeee utacheka
wanakaliana mita 100 kama wapo kwenye kituo cha kupiga kura

general (jang-gun μž₯κ΅°): saranghaeyoooooooooo
binti (agassi): na do sarangahaeyoooo
general (jang-gun μž₯κ΅°):bogoshipdaaaaaaa
binti (agassi): na do bogoshipoyoooooooo
mara paap general anatoka mbio na farasi wake mpaka kwa mwanamke basi mtazamaji anabaki kujiuliza huyu bwege anataka kufanya nini?
kumbe mbio zote anataka kumkumbatia mwanamke baadae amwambie nakwenda vitani agassiiiiiiiii

kituko wanapoamua kupigana busu mhhhhhhh
hilo vurugu lao utadhani ndio wanatafuta mtoto na si ajabu kumkuta mmoja kati yao amekatwa ulimi au ameng'olewa jino

endelea hivyo hivyo na ujinga wako wa kuwashikilia hao wavaa mapazia na wafugaji ndevu nyingi kama steel wire za kuoshea masufuria yaliopikiwa pilau
bwege weweeeeeee
=======================================================
happy birthday bae suzy
acha niangalie vagabond ep 7 kabla ya saa 2 kufika.

 
Hahaha Bado sijaijua ladha ya Modern Drama.
Huko kuna swaga gani?
Ati " Wavaa Mapazia" mbona huwasemi ndugu zako wavaa vikoiπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Nimeipenda Iyo Picha.

Oct Mwezangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…