Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Unataka Niambia Hujazifurahia Hizi Tuzo Eti Eeh!?

Amekua New Actor Kwa Sababu Labda Ndo Tuzo Yake Ya Kwanza Kwenye Tuzo Hizi
 

Kamsahmnida Chingu.

Kwaiyo Apo Ubora Wa Muigizaji = Script Nzuri+Director +Kipaji
 
Ni Kiporo Nitakirudia Siku Si Nyingi InshaAllah
 
Inaonekana ata kwenye maisha halisi we ni mtu wa watu,kama ilivyo humu.
Ni kweli niliiandika mda utakua hujaiona,mi ndo mwenye kosa pia sikukutag.......kumradhi.
 
Kwenye Usiri Apo Tunafanana.

Keki Ya Mchele Ushakata!? Au Nivuke Maji Tukale Ulojo.

Ukawe Mwaka Wenye Kheri Nyingi InshaAllah Na Kila Utakaloliomba Mola Akaweka Wepesi Wake InshaAllah.

Mama Dae Leo Akupikie Vireja.
 
Naona We Unaielewa Kweli.

Kwangu Kiukweli Napata Nayo Shida Sana.
 
Duh uchambuzi mrefu mpo vizuri,mie nimefata scene za kiss tu,ile ya shingoni aiseee hadi nikatamani kuwa kale ka actress🤣🤣 .
 
Naona mnaendeleza libeneke wazee!!
Mi nilistaafu hizi korean baada ya kuona zinanitia uchizi hasa ile bandika bandua.
Now nimeichungulia hii Ķing makers~ The change of Destiny (wind,cloud and rain).
Naona mdogo mdogo uchizi unarudi.
 
Ts okay 😃😃kwakweli una marafiki wengi humu,wengine wamemute ila watakuja kiri kwa wakati wao ukiwadia.

Bila kusahau kufarijiana.wengne hz series zinatufariji sanaa na kutusahaulisha sometimes magumu tunayoyapitia kila leo......Sasa uwasilishaji wako juu ya hz drama humu kwakweli unatuhamasisha sanaaaa na wala hatutumii nguvu kutafta ipi nitazame.mi naomba nikushukuru kwa niaba ya wote🙏🙏
 
GHOST

Wataalamu wa cyber space

Hades na Phantom 0338

Hao jamaa na polisi ni kama Kigogo 2014 na TISS + polisi hapa kwetu

Fuatilia pamoja nami naingia ep 04
 
Woman of dignity ajali nyingine ndani ya ndoa hasa za wadada wa mjini wao wanajiita classic chics.

Eccentric chief moon ina vituko vya hapa na pale. Mwenyekiti wa wanawake hapo kijijini ni mfano bora kabisa wa wanawake watunza siri kwa sekunde tatu tu 🤣 🤣 🤣 . seol ah katoto kamejua kuicheza nafasi yake fresh hasa kipaji cha kujipatia misosi ya bure.

Nikarudi nyuma dream high zote mbili. Nimeipenda part two kuliko part one
 
Long time no see!

Natumai mu wazima wa afya na mnaendelea vyema katika kuliendesha jukwaa hili la burudani hususani upande huu wa Korean drama.

Ni muda sasa nimesitisha kufuatilia 'on going' ila nimeona ni vyema zaidi kuzihifadhi mpaka pale zitakapo malizika ama kukamilika ndipo nizitazame kwa ukamilifu wake.

Lakini wakati nikifanya hivyo nimeona si vibaya nikitazama baadhi ya kazi fupi fupi zilizopita ama za miaka ya nyuma.

Miongoni mwa projects nilizojichagulia kuzirudia kwa sasa ni hizi tatu;

  • The Innocent Man
  • Let's Fight Ghost
  • Master's Sun

Wengi wenu nafikiri mtakuwa mmekwisha kuzitazama kazi hizi.

Baada ya kuzimaliza kazi hizi tatu, nafikiri nitakuwa nimekwisha kujikusanyia kazi mpya ya kuitazama kadri mwenendo wa 'on going' utakavyokuwa ukielekea.

Pamoja sana!
 
Aisee! Hongera sana kwa kumaliza "assignment" hiyo ndefu na ya aina yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…