Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

pole sana dae. Karibu ulimwengu wa simu. Cd nyingi zimetafsiriwa au kukatwa part one hadi four
daktari amenipa majibu:
motherboard imeungua na rasmi nimeyaanza maisha ya kutokuwa na computer.
tafsiri yake:
  • korean drama bye bye kwa muda usiojulikana....hata kama nitaifanya hard disk yangu iwe external nitakuwa bado nakosa wasaa wa kudownload drama......nirudi kwenye maisha ya kuuziwa cd?......hapana hapana hapana
  • JF nitakuwa nachungulia
  • nitakuwa naishi maisha ya kutegemea redio, now nimekuwa msikilizaji mkubwa wa wasafi fm asubuhi kupata taarifa za michezo na DW jioni kupata taarifa za kiulimwengu.......teh teh teh yajayo ni tabu tupu
 
Kweli binadamu tunatofautiana. Kwangu simu ndo kila kitu. Laptop ilishawahi kuharibika ipa simu iliokoa jahazi
ulimwengu wa simu pia ni majanga kwangu..... natumia simu fulani za microsoft na betri yake niliiharibu (nilikuwa naitumia kwa hotspot huku nimeiweka chaji, unajua tena ukishajiunga mabando ya GB 4-10 unafanya israfu)

nimeshatafuta betri yake takribani asilimia 80 ya maduka yaliopo zanzibar, niliposhindwa ndio nikatafuta modem kwa ajili ya internet na kurudia simu za kawaida.

itokezee leo nimepata laki 3 hadi 5 basi uamuzi wangu utabaki vile vile Numbisa wa kununua kwanza computer (iwe laptop au desktop) ndipo nifikirie simu.

kwangu mimi simu ni mawasiliano tu (call +receive) na computer ni kazi zangu zote zikiwemo zinazofanywa na simu (whatsapp).
 
sijaangalia drama kwa takribani wiki mbili....

hivyo vidrama vyako uchwara pia sijaviangalia.

Ushauri wa bure kutoka kwa chama dola..

Ongezea penthouse drama.
kama una fikra za kimasikini usiangalie Ila sikukumbuki kuwa na fikra hizo.

Zile swagger za sky castle, ndivyo wasemavyo wenyewe walioaiangalia.

huku kwetu wanaitwa wazaliwa wa baghani, shangani, hurumzi, michenzani....

Utasikia tu...
aunt talnam ile dollar 3900 umeshaituma kwa shangazi farhini wa chukwani?

akina sisi...
wewe daee ile 1599 iliobaki kwenye tigo pesa hebu itoe tukapate dagaa.


unabaki

Mhhhhhh mamaa hii ni ya bando la usiku, Kuna wahuni wa telegram wanajifanya hawajui kupakua season.

Mama mwenyewe na majibu yake

Ebooooosssss!!!! pumbavuuu hiyo telegram ndio inayokulisha, ndio maana umekonda Kama miguu ya popobawa.

Umasikini laana
Hahahaha 18 again yani natizama tuuu
Ila do do Sol ni taaaamu

Nimeanza kutizama 1&2 penthouse kabla ya hii comment na surely Ina itikadi za sky castle, na inahamasisha kuendelea.

Hii kairos nayo naivutia episode ingawa mambo ya time dimension sijui yananiumizaga kichwa

Sent from my Hisense T5 Plus using JamiiForums mobile app
 
Search
tells the story of a member of the army who, as part of his military service, has dedicated himself to training dogs for his team, but when he is about to retire from this work and be discharged from the military, he is sent to a special mission to the demilitarized zone of South Korea.
images (2).jpeg

Nipo zangu sehemu ya nne, imetoka mpaka ep. ya 6 ( ongoing) karibu sana, tupate kitimtim kinachotokea hapo DMZ ( mpaka wa SK & NK)
 
Whaaat..?!(In korean) ahjummoni???!
kama nimekuelewa vyema:
ahjumma na ahjumeoni ni maneno yanayofanana kimaana ila utofauti wake unakuja muda wa matumizi.

ahjumma = liaweza kutumiaka kwenye mazingira yanayopelekea kukosekana kwa nguvu ya kiheshima, kwa kuangalia kwangu drama unaweza kumkuta kijana au binti amekasirishwa na jambo fulani hatimaye anamkaripia mama fulani kwa hasira (mfano ahjummaaaaa nipe chakula)

ahjumeoni= modest or polite.....
 
kama nimekuelewa vyema:
ahjumma na ahjumeoni ni maneno yanayofanana kimaana ila utofauti wake unakuja muda wa matumizi.

ahjumma = liaweza kutumiaka kwenye mazingira yanayopelekea kukosekana kwa nguvu ya kiheshima, kwa kuangalia kwangu drama unaweza kumkuta kijana au binti amekasirishwa na jambo fulani hatimaye anamkaripia mama fulani kwa hasira (mfano ahjummaaaaa nipe chakula)

ahjumeoni= modest or polite.....
Hujanielewa
 
Search
tells the story of a member of the army who, as part of his military service, has dedicated himself to training dogs for his team, but when he is about to retire from this work and be discharged from the military, he is sent to a special mission to the demilitarized zonend
wewe endelea kushabikia simulizi za kivita utadhani una vinasaba vya bwana yule genghis khan....
watu kama wewe ndio wale wanaowakilisha kundi lile linalojishindilia mapande ya sabuni ili wapate ugonjwa wa kuharisha pindi wanapotakiwa watoke mbele kwa dhumuni la kuipigania haki iliozimwa kama mshumaa.

waendeleaje na masomo yako muhuni wewe?
 
Back
Top Bottom