Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Happy new year 2021
mwaka 2020 nilijiwekea lengo kuu la kupunguza dozi ya kuangalia wakorea, nashukuru zoezi hilo lilifanikiwa kwa kiwango kinachoridhisha.

mwaka 2021 nimejiwekea lengo la kutokuangalia korean drama, si jambo rahisi kutekelezeka hususani ukishakuwa ni muathirika ila kwa kuwa nimeweka nia na dhamira imara natumai nitaifanikisha azma yangu.
Na Ikawe. Si Rahisi Ila Kama Una Kitu Cha Kukufanya Tyt Kidogo Unapunguza au Ukipata Mbadala Unaweza.
 
uraibu ni ugonjwa mbaya sana,
jambo nililolikusudia kulifanya kama nitalifuatilia kama ninavyofanya kwa wakorea basi nitafanikiwa.
ni jambo litakalonilazimu kupoteza muda, si hivyo tu nahitajika kuwa makini kifikra muda wote.

nitakapoweka bidii naamini Mungu atakuwepo pamoja nami kuliko shetani, kinyume chake nitaendeleza uraibu nisiojua tarehe ya kuachana nao.

inakaribia miaka 9 tokea nianze kuangalia wakorea, nisipotosheka kipindi hiki ...............................
Itakusaidia Ukiamua na Ukiwa Hasa Bizee Aaah Wakorea Hutawaona.
 
Back
Top Bottom