jamani amkeni, amkeni wizara mpya ishafanya ya kwake.
sasa ni rasmi tumestaafishwa kufuatilia movies, series na drama kwa njia ya mtandao.
- bando la usiku limeondoshwa
- kifurushi cha siku kwa GB 1 kimeondoshwa
- vifurushi vyenginevyo vimerambwa mnoooo
halotel hongereni kwa hichi mulichotufanyia
============
upande wa zantel kwa huku zanzibar
kutoka GB 3 kwa siku kwa shilingi 2000 hadi mb 900 kwa shilingi 2000
na mabadiliko mengineo
===========
watu wa Airtel na vodacom vipi huko tunaweza kuhamia?
sisi wengine tunahitaji japo kifurushi cha usiku
=========
kikao kimeanza rasmi chenye lengo la kujadili haya mabadiliko, kama huamini ingia kwenye menu yako.
aminas mlevi mwenzangu uliyebobea
Numbisa mlinzi mwenzangu wa usiku tunatokaje
talnam mfukuza upepo kimya kimya
missyrose mlevi mwengine wa korea
Great Conqueror huko kaskazini huduma zenu ni nzuri?
na malegendary wengineo mukipata wasaa muhudhurie kwenye kikao
dah! bye bye wakorea?