NDUGU ZANGU HABARI ZENU
Leo nimetumia weekend yangu kucheki drama hii inaitwa "Dangerous Promise" au kwa jina lingine inaitwa "Fatal Promise" kiukweli hawa wa korea wanajua kweli kweli si masiala sasa hivi nipo episode ya 28 lakini mwisho wa hii drama ni episodes 104 hiv, nilicho notes kuanzia episode 1 ni moto mpaka sasa yaani ni drama ambayo ina amsha amsha kuanzia mwanzo mpaka mwisho kila inapoisha episode unatamani kuangalia inayofuata.Kiufupi kila episode inatumia nusu saa.Pamoja ya kuwa hii drama ina matukio ya kuvutia lakini pia ina love story ndani yake ya maana si kama nilizowahi kuangalia ya hii ni ya kipekee ambayo inagusa maisha yetu kiujumla.
Binafsi me sio mpenzi wa love story lakini ya hii drama nimeikubali mno ni [emoji91], ni drama ambayo hujuti kupoteza bando lako ina mtihiririko mzuri wa story inayomvutia mtazamaji kuangalia zaidi.
Jambo lingine niliyokubali kwenye hii drama haina utoto mastaa waliocheza wa hii drama wapo serious hawana uweuweu kitu ambacho inaongeza mvuto zaidi wa drama.Asikuambie mtu pamoja na kuwa napenda Sana mpira lakini Jana sijaangalia mpira na leo pia singalii kwaajili ya hii drama.
NB: Nimeona ndugu zangu tushehe mambo mazuri na nyie kama hivi.
Khantwe
Daemusin
missyrose
Numbisa
kdrama_masters
aminas