Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Endelea tamu sana kwangu ni nzuri kuliko drama yoyote ya kikoreaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Aigoo.... kwa mlioangalia reply 1988 niendelee kula mtori nyama ziko chini? Maana nimeangalia episode tatu naona maruweruwe tu
 
Kwangu hii ndio namba moja yaaniyaani yule queen hata nikiona picha tu najikuta nacheka
Uko sawa pia, Wee ukienda YouTube ukasachi kuhusu K. comedy series, Waikiki ndio iliyokubaliwa na zaidi.
Huyo mfalme wa kwenye Mr. Queen ndiye alikuwa Faza hausi kwenye Waikiki
Naweza kusema kwamba hakuna Movie au series ambayo imewahi kunichekesha kama Waikiki.
 

Now nimeelewa, Hii 2013 ndio iliyochezwa na Kim Jun. Basi walianza kunichanganyia hapo kwenye Google.
2013 ni zama ambazo pia Wakorea walikuwa vizuri sana, vipi kali kati ya 1999( Geumwa) au 2013 ya ( Kim Jun)
 
Hawa wazee ni kizazi cha dhahabu, wako zaidi ya serious drama hazichoshi yani, hii drama inataka kunikumbusha Emperor of the see. Kifupi ni nzuri.
kwa huu mwendo wako yanipasa nikiri tayari umeshampiku mwalimu wako, hapo juu nimemuona mchumba wangu wa njia ya televisheni anayeitwa Kim Hyun-joo na nyakati hizo pengine ndio alikuwa kwenye ages zile za miaka 20.
nikushukuru kwa kunizawadia zawadi hizi mbili tena kipindi hiki nilichojaa upweke wa kutokuangalia period historical drama, naahidi kuzifanyia kazi assignment zako mwanafunzi wewe mtiifu
  1. Show All Episode of Sangdo - Dramanice
  2. Show All Episode of Hur Jun - Dramanice
hapo juu imeandikwa hii riwaya ya sangdo imeandikwa na choi in ho, kama ulikuwa hufahamu huyu muheshimiwa pia ndiye aliyeandika riwaya ya haeshin (emperor of the sea) si ajabu ndio maana imekurudishia kumbukumbu za drama hiyo.
 
Aigoo.... kwa mlioangalia reply 1988 niendelee kula mtori nyama ziko chini? Maana nimeangalia episode tatu naona maruweruwe tu
hizo nyama unazozitafuta humo ndani ninakhofia hilo dishi la pilau utalitoboa na bado hutofanikiwa kuziona.
mara yangu ya kwanza kuiangalia hiyo drama kikubwa nilichokishuhudia ni makelele mengi, vurugu nyingi, lafudhi mbaya, mavazi mabaya na miziki mibaya.
nikabaki najiuliza hivi hii ndio drama nzuri inayosifiwa na kila mshabiki wa korean drama?
nikaifuta haliyakuwa nilishaishusha episode zote na pia niliiweka telegram channel (imagine bando nililotumia)

miezi ilipita hatimaye nikaamua kuzungumza na nafsi yangu, kama hii drama inasifiwa na wengine kwa nini mimi nishindwe kuiangalia.
hatimaye nikaiandika historia ya kuwa miongoni mwa wanadamu walioiangalia hiyo drama.
nawewe zungumza na nafsi yako,
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kwamba hukuipenda ila ukaamua kwenda na trend
 
Daah basi bwana inawezekana...yule kaka (Mr Kim stiff) anajua sana. Natamani wakorea wampe nafasi nyingine
 
Kiukweli na mimi nipo kuzungumza na nafsi yangu kama niendelee au la. Hiki nilichotazama mpaka episode ya tatu sijui hata ni kitu gani...nnimepakua episode 6 nimeangalia tatu nina shaka hizi tatu zilizobaki sitaangalia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…