View attachment 464605 View attachment 464608 View attachment 464610 View attachment 464611 View attachment 464612 View attachment 464605 View attachment 464608 View attachment 464610 View attachment 464611 View attachment 464612
Korean drama film location (1)
Naweza kusema tv ndio dirisha la ulimwengu huu,kwani inatusaidia kuona maeneo mbali mbali ambayo hatujawahi hata kuyaona,hususan pale tunapoangalia korean drama ambazo kiukweli zimetufanya tuwe kama wajoseon wenye asili ya afrika naamini kuna maeneo ambayo location zake zinatuvutia sana.
N seoul tower(namsan tower)
ndio icon ya mji wa seoul, Kama ni muangaliaji wa korean drama basi huu mnara naamini utakuwa umeuona mara nyingi sana, kwenye mnara huu kuna cable car service ambayo inakupeleka kwenye njia kuingilia ndani ,kwa mfano kama umeangalia boys over flower utagundua kuwa ndio eneo ambalo kwa mara ya kwanza tulishuhudia bitterly cold date kati ya goo jun pyo na geum jan di jambo ambalo liliwafanya wagande kwenye cable car usiku mzima.pia kwenye my love from another star
Gwanghwamun :ni eneo ambalo lina historia ya takribani miaka 600,ndio eneo ambalo utakutana na feature ya mfalme sejong pamoja na admiral lee soo shin.kama umeangalia tamthilia ya iris 1 utagundua kuwa ndiio eneo ambalo wale magaidi wa north korea ndipo walipotegesha nuclear bomb,pia kama umeangalia queen hyun man ndio sehemu ambayo utashuhudia romantic kiss kati ya scholar kim beung do (ji hyun woo)pamoja na kim hee jin(yoo in na)
View attachment 464605
Korean folk village : naweza kusema ni eneo ambalo linafanana na maisha ya utawala wa joseon dynasty kuanzia makaazi ya kitamaduni,vifaa vya kitamaduni n.k.kutokana na sifa hizo ndio maana asilimia kubwa ya historical drama shooting location zinafanyika hapo,
Sungkyunkwon Scandal,
the moon that embrace the sun,
jumong,
gu family book ni baadhi ya drama ambazo location zilifanyika hapo.
Petite france :
unalikumbuka lile magic kiss kutoka kwa domin joon kwenye
my love from another star, kiukweli ni eneo ambalo linavutia, ni safi, simple design,pia kama umeangalia
secret garden utagundua kuwa ndio eneo ambalo walikutana kwa mara ya kwanza kim joo won(hyun bin) na gil ra im(ha ji won) ni eneo ambalo lina takriban majengo 16 ambayo unaweza kuyatembelea na pia kupata chakula cha kifaransa pia muna maduka makubwa.
View attachment 464610 View attachment 464611
Bukchon Hanok Village: ni eneo ambalo limezungukwa na gyeongbokgung palace,jongmyo shrine,na ni eneo lenye nyumba nyingi za utamaduni wa joseon.
personal taste,
heartstring ni miongoni mwa drama ambazo location zake zilifanyika huko.
Gyeongbokgung Palace: ni ikulu ya mwanzo kujengwa katika utawala wa joseon mwaka 1395 asilimia kubwa ya drama zinatumia eneo hili hususan kama ni eneo la mfalme,miongoni mwa drama zilizotumia location ya gyeongbokgung palace ni
rooftop prince,
the moon that embrace the sun,jang young sil,
king sejong the great,n.k
Yeouido Hangang Park:je unakumbuka makutano ya lee yun seong na kim nana kwenye city hunter? ni eneo ambalo lipo mkabala na hangang river ,
Yeouido Hangang Park ni kivutio cha watalii,ni eneo ambalo michezo mbali mbali huwa inafanyika kama vile marathon na pia ni eneo ambalo limekusanya ofisi na makaazi ya watu(resident)