Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

The King of Tears Lee Bang Won, ni moja ya drama nzuri sana. Inafaa sana kina dada na kina mama muitizame hii drama. Katika drama hiyo inaonyesha vile mwanamke anapaswa kumsimamia mume wake katika nyanja nyingi mno, kiushauri na ata kumpambania mume wake ili atimize ndoto zake. Bonge la drama kwakwel.
 

Kweli Lady Min ana mchango mkubwa kwenye mafanikio ya mumewe Bang Won ila sio kama anavyotaka! Ati nusu ya Joseon ni mali yake? Ujinga mtupu anaojazana na baba yake.
Huu ni mtihani mwingine ambao natamani kuuona Bang Won atauvuka vipi?

Bado baba yake (Bang Won) aliyepata ruhusa ya kuondoka kwenye palace alikowekwa kizuizini na Bang Won, je huko nyumbani kwao alikoenda atatulia tuli bila kulipiza kisasi?

Mwanzoni alipokweka kizuizini alijaribu kumtumia swahiba wake Ji Ran kufanya shambulizi la kulipiza kisasi Ji Ran akagoma…
Naisubiri kwa hamu ep 21 na 22!
 

Boooonge la drama, akili kubwa tupu zinatumika humu!
Yote uliyoyasema ongezea na sapoti. Unajua mwanaume anaweza kuwa anataka kufanya jambo kubwa la manufaa ila akasita au lah akapingwa na watu wengine… hapa ndipo inapohitajika sapoti ya mwanamke wake!

Nimekuwa inspired sana na ushupavu wa Queen Sindeok na Lady Min, sana sana!
 
Naam ni sahihi kabisa, kingine nimejifunza ni kutoka kwa mfalme Lee Seong Gye. Ni sahihi kabisa watoto hukosea tena kwa maudhi makubwa mno ila sio sahihi kuonyesha chuki za waziwazi kabisa mbele ya wototo wako. Lee Seong Gye hakutaka kutoa msamaha kwa watoto wake alizidisha chuki za waziwazi, hii ilipelekea Lee Bang Won kuchukua maamuzi magumu.
 
ndio mwanzo wa kuvurugika kwa mahusiano yao ya kindoa na kiukoo, kwa mujibu wa maandiko lee bang won atawaua hao kaka zake wawili ambao wamekuwa msaada mkubwa sana katika kampeni ya kufanya mapinduzi, baadae watatofautiana kwenye urithi wa madaraka ya bang won, lady min na ndugu zake wengine wawili walimpigia kampeni mtoto wao wa kwanza awe mrithi wa madaraka wakiamini ndiye atakayeweza kurudisha mahusiano yaliofifia kati ya pande mbili hizo, taarifa za bang won za kutaka kuachia madaraka ziliwapa bashasha na furaha hao ndugu jambo lilimughadhibisha taejong, akawapa adhabu ya kuwatekeleza nafikiri na hao wawili wengine pia aliwaua
(sina uhakika). bang won aliongeza mke na inasemekana lady min akawa anamtesa huyo concubine, pia lady min alizaa mtoto mwengine wa kike na hakumtaarifu mume wake jambo lililozidisha ghadhabu na inasemekana bang won alimsusia mkewe.mwishoni bang won akamuachia madaraka mtoto wake wa tatu(mfalme sejong the great) badala wa kwanza kama kumkomoa mke wake na ukoo wao. licha ya kumuachia madaraka mtoto wake lakini bado aliendelea kuwa remote kuu ya serikali ndio maana si ajabu akamuua baba mkwe wa mtoto wake. bang won alikuwa ni mshenzi mwenye uelewa mkubwa wa siasa na diplomasia.
 
uzuri hiyo drama imebase na historical events, natumai watatuonyesha upande wote wa bang won mpaka kuondoka kwake. kama utakuwa na mzuka baadae itafute the great king sejong drama. huyo mzee kim young chul aliyeigiza yi seong ye ndiye ameigiza uhusika wa lee bang won. utamchukia
 
Hahaaaa, mi ndio maana huwa sipendi hizi ongoing drama. Ujue mpaka nimeanza kuifuatilia ni pale tu nilipata taarifa kuwa imepigwa stop baada ya farasi kuanguka vibaya kisha kuvunjika shingo wakati wakishuti. Nilitaka iishe kwanza ndio nishushe mzigo wote, sasa baada ya kuona hivyo ikabidi niitizame tu.

Sasa kwa wakati huu ngoja nikaicheki hiyo ya The Great King Sejong, sema Lee Bang Won alikuwa mwamba sana yaani mpaka unatamani kuwa kama yeye. Kwenye Six Frying Dragons kule nako aliwasumbua sana kina Sambong
 

Hii drama imenifanya nikarealize kuwa niliielewa sana six flying dragons. Nilikuwa na idea ya kila tukio, ikiwemo Jeong Do Jeon alivyouawa kwenye lile daraja kwa rungu la chuma na jamaa aliyeko juu ya farasi, Bang Won kumuua Sambong n.k
Ila hii drama iko deep zaidi.

Kiukweli nipo upande wa Bang Won, japo nimekoshwa sana na umahiri wa bibie Lady Min ila mwisho wa siku Bang Won anakwenda kuwa mfalme, anapaswa kuwa juu ya wote na sio kuwa na usawa na yeyote.
Nimefurahishwa pale Bang Won alipogundua janja ya ‘fisi’ ya mkewe kujirudi kumbe alikuwa anamlaghai [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Bang Won ni jembeeee [emoji1433][emoji1433][emoji1433]
 

Mbona imenitisha? Episode 86? Hapana
Isubiri kwanza nikiwa bored nitaiangalia tena.

Muhusika pekee niliyemkubali aliyemuigiza Seong Gye ni Ji Jin Hee kwenye The Great Seer
 
Kwa wale tuliokua tunafatilia young lady and a gentleman nadhani tutakua tumeridhishwa na bonge moja la happy ending!
Tutammis sana ms wang,sejong na dan dan wa kulia lia😂
 
Kwa wale tuliokua tunafatilia young lady and a gentleman nadhani tutakua tumeridhishwa na bonge moja la happy ending!
Tutammis sana ms wang,sejong na dan dan wa kulia lia[emoji23]
Unazingua mkuu, watu mkoje lakini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…