Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Nilijiegesha kwenye VPN nikitegemea tutarudi kwenye bundles za night pack soon kumbe ndo kwanzaa njemba zinatafuna mb na kutubebesha mizigo mikubwa
mwaka mmoja nyuma nilikuwa nanunua GB 3 kwa shilingi 2000.
leo hii nauziwa mb 980 kwa shilingi 2000.

nilijaribu ha tunnel kupitia simu yangu kwa kutumia laini ya airtel ila bahati mbaya haifanyi connection ya internet.
hali imekuwa mbaya kweli.
 
Kinachonifanya nipende picha za kikorea haswa historical ,jamaa maneno yao inaelekea wanayachagua kwa umakini yaani full madini hafi na screenshots baadhi kutumia kama Quotes .Tukija hata katika mazungumzo yao ya kawaida tu kwenye drama hawafiki nje ya picha kwa kuzungumza utumbo kama wabongo na wengine muda wote unatamani uwasikilize wao hata tukikutana na wachekeshaji.
 
Kuna historical drama inahusu historia ya Baikije star wa picha humo anatumia jina la Yeogi(Yogusu) nineishia episode kama ya 10 hivi naona haijanivutia vipi kali ?
inaitwa king geunchogo, mmoja kati ya wafalme walioacha legacy bora ndani ya baekje.
aliweza kuitanua himaya ya baekje ndani na nje ya three kingdom
aliweza kuwasambaratisha goguryeo katika uwanja wa vita na kupelekea kifo cha mfalme wa goguryeo aliyeitwa gogugwon........huyo bwana alichapwa ndani ya mji mkuu wa Pyongyang.

huyo Gogugwon ndiye mfalme pekee wa Goguryeo aliefia katika uwanja wa vita.

Gogugwon alikuwa na watoto wawili ambao ni sosurim na gogugyang.
huyu gogugyang ndiye baba wa damdeok(gwanggaetto the great)

sosurim alikuwa hana mtoto hali iliopelekea madaraka yarithiwe na ndugu yake ambae ni mfalme gogugwon.
hii drama haikuwa na mafanikio makubwa ila ukiifuatilia ndio itakupa mnyororo wa simulizi hizi za three kingdom.

kumbe damdeok alikuja tu kulipiza kisasi cha kupigwa kwa babu yake na mfalme geunchogo.
kulifahamu hili lazima urudi kwanza kuifuatilia king geunchogo

both goguryeo na baekje wanatokanwa na mzizi wa Jumong na Soseono
mfalme asin wa baekje akijisalimisha mbele ya mfalme damdeok wa goguryeo
 
kingine hasa zile za historical dramas,ukiangalia zile siasa zao ni kama hapa nchini tu,unakuta king puppet
 
Kongole kwa nondoz adhimu , Geunchogo anaheshimika sana hata kwenye hiyo picha upanga wa kifalme unaoheshimika unaitwa 'upanga wa chogo ' ambao iki uitwe mfamle lazima ukabidhiwe . King Gwangaetto nimecheki Asin baada ya kubisha muda mrefu mpaka akaamua kusurrender mazima, itabidi nitafute hiyo ya Geunchogo niicheki vizuri mwanzo mwisho.
 
Script writters wao wako serious na kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huzo three kingdoms ni Silla, Baekje na Gogryeo au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna family drama moja. Jamaa kijana tu kaajiriwa kama mtu wa mapokezi sasa ile siku ya kwanza tu akasimama reception akisalimia kila anayeingia kwa sauti kubwa. Boss wake akamuuliza hivi kuna ancestors wako aliefariki bila kutoa salamu,mbona salamu nyingi hivi😂😂😂😂
 
Nimemaliza leo kuangalia 18 again, hata nikiifuta nitabakiza episode ya kwanza niwe nacheka[emoji1787][emoji1787][emoji1787] mimi fantasy drama kwa kweli nazipenda zina ka-vibe fulani hiviii.
Nataka nianze Today's webtoon japo ratings zake sio nzuri nitaangalia tu vile nampendaga Kim sejeong na Choi Daniel huwa namsikia tu sijawahi kuona kazi yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…