Sikuhizi napata shida sana kupata drama nzuri za korea, hii ndio shida ya kuwa umeangalia drama nyingi nzuri , imefikia hatua natamani ndo ningekuwa sijawahi kuziangalia ili nizianze kwasasa.
Kila dram unayoshika a hovyo tu, hata zile zinazosifiwa ukiishika unakuta ni ya hovyo tu tofauti na zamani kitu kikiwa recommended ukikitafuta unakuta ni moto kweli, sasahivi drama nyingi ni za issue pet pet za kuangaliwa na dada zetu, zile genre za maana (thriller, Suspense, Crime&Investigation..nk) sikuhizi hawazifanyii project tena kama ilivyokuwa miaka ya nyuma (2000-2019)
Kibaya zaidi nishakuwa addicted na wakorea, drama culture nyingine sina hata moyo wa kutaka kuzifuatilia. Ngoja nitundike daruga kwasasa, nisubirie labda miaka ijayo watarudi vizuri tena.
Sent using
Jamii Forums mobile app