Habari, Leo nimekuja na list ya historical drama 10 ambazo zilinivutia zaidi kwa kuwa na
story nzuri.
1.
Dong Yi: Jewel in the Crown
Hii tamthilia haijawahi kunichosha kuanzia sehemu ya kwanza mpaka mwisho kwa jinsi ambavyo uhusika unavovaliwa na waigizaji lakini pia mpangilio wa visa na mikasa ndani ya tamthilia hii. Credit kwa mzee Lee Byung-Hoon, ambaye ndiye muongozaji wa kazi hii akisaidiwa na Kim Sang-Hyub · Kim Yi-Young ambaye ndiye mwandishi. Kazi ilirushwa na
MBC
mwaka: 2010
2.
Dae Jang Geum: Jewel in the Palace
Hii tamthilia ilitwaa tuzo nyingi sana, pia inatajwa kuwa ndio tamthilia iliyotangaza utamaduni wa korea duniani kote, pia ilichochea ongezeko la utalii, sababu ilitangaza vivutio vya utalii. Hii tamthilia kwangu mimi naipa vyeo vyote. Mzee wetu Lee Byung Hoon(mtayarishaji) akiwa na msaidizi wake Kim young( mwandishi) ndio walikuletea hii kazi kupitia
MBC
Mwaka: 2003
3.
Prince Of Legend: Jumong
Kazi hii niliipenda tu, miaja ya 2008 nilipokuwa naifuatilia kupitia ITV Tanzania ingawa. Ratiba yake ilikuwa J.tatu mpaka J.tano kuanzia saa 5 usiku enzi hizo ikifika saa 4 au 3 na nusu tayari mtu ushaambiwa kasome au kalale kesho uwahi shule. So Jumamosi ndio muda mzuri wa kuirudia.
Umewakumbuka wale wahuni 3( Mari, Hypobo na Oi) ? Pamoja na mkubwa wao Jumong? Ebuana ile combination ilikuwa si mchezo. Seossoneo na watu wa kwao huko Keru na Pyiru ilikuwa inavutia zaidi. Ingawa ilikuja kupungua kidogo baada ya mwamba kuwa mfalme maana huyu Gook il son ndiye alikuwa anainogesha zaidi, maana ukishakuwa kiongozi wa taifa huishi tena kisela bali kwa utaratibu maalum. Hii kazi nimeirudia maranyingi mno bilA kuichoka.
Imetayarishwa na Lee Joo Hwan akisaidiwa na Kim Keum Hong.
Hii kazi ilitwaa tuzo nyingi mno, na haki zake za kurushwa na vituo vingine iliuzwa sehemu nyingi duniani, na ilipendwa zaidi Nchini Iran(90% Audience) walivutiwa zaidi na kazi hii kuliko South Korea (40% Audience) ndio walikongwa nyoyo nayo.
Kupitia umaarufu wa kazi hii ulipelekea sintofahamu kati ya Serikali ya China na S.korea kuhusu historia ya Gogryeo. Si unajua wachina walikuwa wanadai ni Gogryeo ilikuwa yao?. Drama hii ilikuwa na Episode 60 lakini kulingana na umaarufu wake MBC walizirefusha mpaka kuwa 81. Ilirushwa na
MBC
Mwaka: 2006
4.
The Great Queen Seon Deok
Hii ilikuwa kazi ya pili kunipeleka Korea. Nimeirudia mara nyingi mno. Washiriki wa humu ndani walifanya kazi njema. Hii drama inakupa kila kitu, story nzuri, Comedy, action, naweza kusema most complete historical drama. Humu ndani utajifunza mengi ikiwamo fitina katika siasa na mengine mengi. Na kumbuka Daek man kule jangwani, hata aliporudi Seorobelo alimuweza sana mwana mama Mishil aliyekuwa ameshindikana. Unamkumbuka Jukban na Goddo wake? Mtaalam Gukson Munno na Bidam wake. Hii kazi ilifanyavema sana sana. Mtayarishaji ni Park Hong Kyun akisaidiwa na Kim Keum Hong( alihusika kuandaa pia Prince of Legend) ilirushwa na
MBC
Mwaka 2009
Kumbuka Queen Seon Deok, Jumong, Dong Yi zote zilichezewa kwenye Setting moja.
5.
Emperor Wang Gun
Kazi hii ya kibabe ilinifurahisha kwa kuwa na historia nzuri sana, naweza kusema kazi hii ilifanya niyajue majimbo mengi ya Goryeo hutojuta kuitazama kila kitu kilikuwa very correct. Humu ndani kuna Acumen Military Advisors nadhani nikitoa Gwanggaeto, The Great Conqueror kwakuwa na watu wenye akili za vita hii Emperor Wang Gun ndio inafuata.
Mzanzibari unakumbuka Sutra hata moja ya kibudhism?! Aliokufundisha mzee wako Gung ye?. Kifupi hii kazi ni nzuri mno na ni kazi dume niwana maana ilainafaa uwe mvumilivu ziko Episode 200 hapa.
KBS1 ndio waliirusha. Iliandaliwa na Kim Jong Sun, mwandishi alikuwa Lee Hwan Kyung.
Mwaka : 2000
6. Haeshin, Sea God, Emperor of the Sea
Achana na ukatili wa Lee do hyeong, penzi la Lady Jung hwa dhiya Jam bogo na Yeom Jang. Kipindi kile naitazama bado nilishangazwa sana kwani hawa jamaa wanamng'ang'ania huyu mdada?. Miaka michache baadae ndio nilikujakuwaelewa. Nakumbuka( kama sikosei) ilikuwa Bandari ya Yangzhou mida ya jioni kabisa, Yeom Jang alimfuata Lady Jung hwa na kumwambia najua moyoni mwako yupo Jang bogo lakini mie naomba hata huo mwili wako. Hapa nilijifunza kuwa kumbe kweye maisha haya mtu aliyenamoyo wa mtu ndiye wa thamani zaidi. Lee do hyeong alikuwa akimuona huyo mwnamke kama chanzo cha udhaifu wa Yeom Jang. Kama sikosei hawa wote( Jang Bogo na Yeom Jang) hawakuweza kuishi nae mwanadada huyo. Adventure za baharini zilinivutia zaidi pia, Jang Bogo kuwa Gladiator baada ya kuuzwa utumwani. Kifupi kazii hii tamu na sijawahi kuitazama Episode ya mwisho na sina mpango huo. Mbali na yote hii ndo drama ambayo ulikuwa unamu- admire adui. Story ya drama hii inamuunganiko flani na Emperor wang gun drama, maana Gung ye ambaye ni ambaye alikuwa ni Prince wa Shilla, mama yake alikuwa binti wa Jang Bogo. Kazi hii ilitayarishwa na Il-soo Kang, akisaidiwa na Kang Byung Taek. Ilirushwa kupitia
KBS2
Mwaka 2004
7.
Sang Do, Joseon Merchant
Utajifunza mambo mengi kuhusu biashara, kuna mambo umejifunza shuleni kuhusu Ujasiliamali lakini huku ndani utaona watu wakifanya kwa vitendo, ni kazi nzuri kweli kweli. Ilitayarishwa na mzee wetu Lee Byung Hoon, ilirushwa
MBC
Mwaka 2001
8.
Hur Jun, The Legendary Doctor
Inastory nzuri sana kama Jewel in the Palace, ilinivutia kwa kila kitu. Mtayarishaji ni yule yule Gwiji Lee Byung Hoon, kupitia
MBC
Mwaka 1999
9. Chuno, The Slave hunter
Mara ya kwanza nilimuona Jang Hyuk ndani ya hii kazi, hutojuta kuitazama. Iliandaliwa na Kwang Jung Hwan, kupitia
KBS
mwaka 2010
10
. God of War, Military Official, Soldier
Hii ni kazi ya kibabe yenye story nzuri sana, utaifurahia sana. Alocheza uhusika mkuu alishapoteza maisha. Drama inamuelezea Mtumwa ambaye alipata Bahati na kuwa kiongozi Mkuu wa Jeshi na kuwa conrol serikalini( Overlord). Scene ya malavidavi kati ya mtoto wa Choe ilikuwa nzuri pia. Hii drama ni kama mwendelezo wa Dude la Kiumeni The Age of Warriors. Ilitayarishwa na Lee Hwan Kyun, ikarushwa na
MBC
Mwaka 2012
Nakupa hii ya chini kama bonus
11. Shin Don
Hii drama pia inastory nzuri sana, inafanana baadhi ya Visa na
Empress Ki, hii drama ni Prio story ya Jeong Do Jeon, Six flying Dragon na The Great Seer.
Drama hii ya
Shin Don ilirushwa na
MBC
mwaka 2004.
UNAWEZA KUTAJA ZAKO 10 ZENYE STORY NZURI ZAIDI
View attachment 2609356
Posta ya drama iitwayo SangDo