Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hapo mambo ya ukorea mwingi sana

Mambo ya golden spoon
Bora iwe reborn rich, iyo ya bundle tu, asante hapana
😎😎😎
Tuendelee kumuomba Mungu atuendelee huu mtihani wa kuwaza bando badala ya maswala mengineyo ya msingi zaidi.

Dedication song, mchana huu
Dont worry, dear - jeon in kwon
Huu wimbo alicopy kwa wajerumani

View attachment 2605958

View attachment 2605950

Hahahah
Mambo ya msingi na sipo kwenye nyongeza ya mshahara

Umenikumbusha nyimbo ya shaun wayback home, aah nyimbo kali ile. Wacha nimsjize huyo huyo diamond fellow
 
View attachment 2603761
The Imjini war
Amecheza Choi soo jong, huyu mwamba ni king wa historical drama. Hana kazi mbovu.

Tafadhali amabaye anajua huyu mzanzibari a.k.a mla urojo @Daemusin anijuze.
Mwambie nimerudi toka Goguryeo maana nimekuwa time traveller.
Kusema huyo ni King unatumia vigezo vipi ? nitajie kazi zake nikamcheki zaidi.
 
3274203737_c0b81e34d2.jpg

huyo bwana pichani ndiye alipaswa kuigiza uhusika wa yeom mun kwenye emperor of the sea drama.
kama umeangalia lobbyist drama huyo bwana alimpenda sana yule dada aliyeigiza uhusika wa maria (Jang Jin-Young).

maisha hayana formular, kwenye lobbyist alikuwa mpinzani wa song il kook ambaye huku alimpokonya tonge mdomoni

pumzika kwa amani wewe dada (cancer ilimsambaratisha mnamo mwaka 2009, miaka miwili baada ya kuigiza lobbyist).

Numbisa nikiandika magazeti ya song il kook hufurahi sana na baadhi ya wakati hunichomoa makusudi.
wiki 6 nyuma alinichomoa akishirikiana na al hadid ila nikaamua niepushe vayolence

==============
behind every successful man there is a woman
katika project ambayo song triplets father naamini hawezi kuisahau ni emperor of the sea,
kabla hajapata offer ya kushiriki emperor of the sea alikuwa ni muigizaji wa kawaida nchini korea lakini baada ya kuigiza uhusika wa yeom mun ambaye alikuwa anateswa na mambo mawili makubwa nayo ni mapenzi na ambition alipata umaarufu mkubwa sana kwa mashabiki hususani wasichana.

najiuliza kwa nini wanawake wengi walioangalia emperor of the sea walimpenda yeom mun ambaye alikuwa ni muuaji aliyebobea kuliko jang bogo ambaye alikuwa ni mtu mwema?
wanasema kwenye maisha yako unayoishi basi kuna nafasi tatu
hayo ndio maneno aliyoyazungumza song il kook baada ya kumaliza sherehe za kufanikiwa kumaliza kwa salama kurekodi drama ya emperor of the sea.

wakati alipopata offer ya emperor of the sea Song il kook alipata kwanza offer ya kuigiza kwenye drama ya ADMIRAL YI SOO SHIN, lakini kutokana na ishu za kisiasa wakati huo mama yake alikuwa anagombania uongozi wa serikali basi kulipelekea mpango wa kushiriki kutokufanikiwa.

nilimchukia sana mama yangu kwa sababu nilikwisha jiandaa vizuri kimazoezi, kuendesha farasi na mapigano lakini kwa sasa naamini sikustahili kuigiza kwenye drama ile, kama ningelishiriki kwenye ile drama naamini nisingelipata nafasi ya kuigiza kwenye jumong (MBC 2006). alisema song il kook.

kuondoka ghafla kwa muigizaji ji sung kwenye drama ya terms of endearment mke wa director aliamua kumshauri mume wake ampe nafasi song il kook wakati ambao director alikuwa anahangaika kutafuta muigizaji mwengine.

mke wa director alivutiwa sana na uwezo wa song il kook kupitia morning drama ya album of life.
kwenye terms of endearment kuanzia episode ya 25 song alicheza uhusika wa mwanamme ambaye alitokezea kumchukia mke wake baada ya kugundua maisha ya zamani ya mke wake,umaarufu wake ulizidi kuongezeka hususan kwa mama wa nyumbani baada ya kuonyesha uwezo mkubwa kwenye drama hiyo na kupelekea kushinda tunzo ya best couple pamoja na mwanadada han ga in.

tukirudi kwenye emperor of the sea timu nzima ya waongozaji wa drama hiyo walikuwa kwenye mtihani mkubwa wa kutafuta muigizaji wa kucheza nafasi ya yeom mun, muigizaji Han Jae Suk ndiye wa kwanza aliyepewa nafasi ya kuigiza na alikuwa tayari alishamaliza photo shooting ya drama hiyo lakini baadae kukatokezea matatizo kwani muda wake wa kwenda kutumikia jeshi ulikwisha fika.

mwanamama chae sira (madam jami) ambaye alishiriki kwenye drama ya terms of endearment pamoja na song il kook akatumia ushawishi wake kumtafutia nafasi song il kook ili aigize uhusika wa yeom jang.
wakati director kang il soo akielekea nchini china kwa ajili ya film location alimuona song il kook ni muigizaji wa kawaida tu ndipo akataka ushauri kwa mke wake lakini kwa mara nyengine nguvu ya mwanamke ilimbeba tena song il kook.

mke wake alisema;
unasemaje ?
kwa sasa ndani ya korea kusini amekuwa maarufu sana baada ya kuigiza terms of endearment na ni bora uharakishe kumpa nafasi kabla hujachelewa. hivyo basi ndani ya drama mbili alipata msaada mkubwa kutoka kwa wanawake. hii ni chance of a life time.

wanaume tunapaswa tuwaheshimu wanawake lakini si kila mwanamke anapaswa kuheshimiwa na kusikilizwa (sentensi tata).

wengine wanapenda vayolence akiwemo numbisa
Andiko zuri sana , Emperor of the Sea ni moja kati ya kazi bora kuwahi kuziona ,mimi drama kitu cha kwanza ni mpangilio mzuri na matukio ndio maana King gwangaeto Pamoja na kunikosha lakini ipo nyuma katika list yangu kutokana na matukio kutopangika na kuwa na mtiririko mzuri.

Baada ya kuziona na kuangalia mwaka uliotoka na kuona kuwa ilikuwa ya kwanza kabla ya Jumong ,nikajua moja kwa moja hakuna drama iliyompa credit kubwa isipokuwa hiyo jinsi alivyoigiza kwa ubora wa hali ya juu mule.
 
Mda wangu ni wa kucheki episode 3 au 2 kila weekend bado naendelea na Dae jo young nipo 14 Kati ya 100 na kitu ,Jang yeong-sill nimeimaliza nimeanza Six flying dragon maana inasifiwa nataka nicheki mtiti wa humo.
 
Wanasema Ukubwa huanza kwa mwanzo wa kinyenyekevu"
Chang Bong Sum alikuwa ni kijana ambaye ni mfanyabiashara mdogo na masikini ambaye alirithishwa nyumba ya kulala wageni ambayo alikuwa akiiendesha. , na kupitia kufanya kazi kwa bidii dhidi ya mfumo wa kirasimu, aliweza kuwa mfanyabiashara Tajiri na mwenye nguvu na kuwa kontroo nzima ya soko na hali ya Biashara wakati wa mwisho wa Yi dynasty( Joseon dynasty).

Hamjambo?, naamini ni wazima wa afya. Baada ya kupotea kwa muda mrefu sasa narudi kwa kuanza na kazi hii.
Hii story imetolewa kwenye kitabu cha Kim Joi young ambacho kilitolewa kwenye Seoul newspaper katika matoleo 10( volume ) toka mwaka 1979 june- 1983 feb.

Mwaka 2015 kituo chako bora cha KBS2 walikuandalia kazi iitwayo The Merchant: Gaekju 2015 ambayo ilikuwa ikielezea maisha ya Chong Bong Sum alivyoanza mpaka kufanikiwa. Hii kazi imejaa watu wenye uzoefu sana( Magwiji) watu wa kazi, wala si mabishoo wa miaka hii.

Jang hyuk tupo nae humu ndani akiwa ndie mshiriki mkuu akivaa uhusika wa Bong Sum, pia tunae Oh seong ye pia yumo ndani humu akiwa kama Gil So Gae, nadhani huyu mwamba tunamkumbuka vizuri kwenye Kim suro alikuwa ndie adui alijiita Grand Duke wa Gaya, pia Swallow of the sun, kwenye Joseon Gunman alikuwa ndie adui mkuu. Mwanadada moon ga young tulikuwa nae kwenye Waikiki zote 2 alifanya vizuri. Pia Mwanadada Min Jung Kim pia yupo ndani, nilimuona mwanadada gaidi huyu kwenye Mr. Sunshine lakini pia kwenye Mr. Devil Judge pote ni wamoto. Na vichwa vingine vingi tuliokuwanavyo kwneye The Age of Warriors na Emperor Wang gun.
Hii drama ina Episode 41 tu.

MV5BZWRmNjY3NGYtOWI5Ny00MmQ3LWE3MDUtOWExODE4YzBmODNkXkEyXkFqcGdeQXVyNzA2OTMxMjA@._V1_.jpg
 
View attachment 2607302
Huyu mzee wa kazi hapo kwenye poster sijamuona miaka mingi sana.
 
Habari, Leo nimekuja na list ya historical drama 10 ambazo zilinivutia zaidi kwa kuwa na story nzuri.

1. Dong Yi: Jewel in the Crown
Hii tamthilia haijawahi kunichosha kuanzia sehemu ya kwanza mpaka mwisho kwa jinsi ambavyo uhusika unavovaliwa na waigizaji lakini pia mpangilio wa visa na mikasa ndani ya tamthilia hii. Credit kwa mzee Lee Byung-Hoon, ambaye ndiye muongozaji wa kazi hii akisaidiwa na Kim Sang-Hyub · Kim Yi-Young ambaye ndiye mwandishi. Kazi ilirushwa na MBC
mwaka: 2010

2. Dae Jang Geum: Jewel in the Palace
Hii tamthilia ilitwaa tuzo nyingi sana, pia inatajwa kuwa ndio tamthilia iliyotangaza utamaduni wa korea duniani kote, pia ilichochea ongezeko la utalii, sababu ilitangaza vivutio vya utalii. Hii tamthilia kwangu mimi naipa vyeo vyote. Mzee wetu Lee Byung Hoon(mtayarishaji) akiwa na msaidizi wake Kim young( mwandishi) ndio walikuletea hii kazi kupitia MBC
Mwaka: 2003

3. Prince Of Legend: Jumong
Kazi hii niliipenda tu, miaja ya 2008 nilipokuwa naifuatilia kupitia ITV Tanzania ingawa. Ratiba yake ilikuwa J.tatu mpaka J.tano kuanzia saa 5 usiku enzi hizo ikifika saa 4 au 3 na nusu tayari mtu ushaambiwa kasome au kalale kesho uwahi shule. So Jumamosi ndio muda mzuri wa kuirudia.
Umewakumbuka wale wahuni 3( Mari, Hypobo na Oi) ? Pamoja na mkubwa wao Jumong? Ebuana ile combination ilikuwa si mchezo. Seossoneo na watu wa kwao huko Keru na Pyiru ilikuwa inavutia zaidi. Ingawa ilikuja kupungua kidogo baada ya mwamba kuwa mfalme maana huyu Gook il son ndiye alikuwa anainogesha zaidi, maana ukishakuwa kiongozi wa taifa huishi tena kisela bali kwa utaratibu maalum. Hii kazi nimeirudia maranyingi mno bilA kuichoka.
Imetayarishwa na Lee Joo Hwan akisaidiwa na Kim Keum Hong.
Hii kazi ilitwaa tuzo nyingi mno, na haki zake za kurushwa na vituo vingine iliuzwa sehemu nyingi duniani, na ilipendwa zaidi Nchini Iran(90% Audience) walivutiwa zaidi na kazi hii kuliko South Korea (40% Audience) ndio walikongwa nyoyo nayo.
Kupitia umaarufu wa kazi hii ulipelekea sintofahamu kati ya Serikali ya China na S.korea kuhusu historia ya Gogryeo. Si unajua wachina walikuwa wanadai ni Gogryeo ilikuwa yao?. Drama hii ilikuwa na Episode 60 lakini kulingana na umaarufu wake MBC walizirefusha mpaka kuwa 81. Ilirushwa na MBC
Mwaka: 2006

4. The Great Queen Seon Deok
Hii ilikuwa kazi ya pili kunipeleka Korea. Nimeirudia mara nyingi mno. Washiriki wa humu ndani walifanya kazi njema. Hii drama inakupa kila kitu, story nzuri, Comedy, action, naweza kusema most complete historical drama. Humu ndani utajifunza mengi ikiwamo fitina katika siasa na mengine mengi. Na kumbuka Daek man kule jangwani, hata aliporudi Seorobelo alimuweza sana mwana mama Mishil aliyekuwa ameshindikana. Unamkumbuka Jukban na Goddo wake? Mtaalam Gukson Munno na Bidam wake. Hii kazi ilifanyavema sana sana. Mtayarishaji ni Park Hong Kyun akisaidiwa na Kim Keum Hong( alihusika kuandaa pia Prince of Legend) ilirushwa na MBC
Mwaka 2009
Kumbuka Queen Seon Deok, Jumong, Dong Yi zote zilichezewa kwenye Setting moja.

5. Emperor Wang Gun
Kazi hii ya kibabe ilinifurahisha kwa kuwa na historia nzuri sana, naweza kusema kazi hii ilifanya niyajue majimbo mengi ya Goryeo hutojuta kuitazama kila kitu kilikuwa very correct. Humu ndani kuna Acumen Military Advisors nadhani nikitoa Gwanggaeto, The Great Conqueror kwakuwa na watu wenye akili za vita hii Emperor Wang Gun ndio inafuata. Mzanzibari unakumbuka Sutra hata moja ya kibudhism?! Aliokufundisha mzee wako Gung ye?. Kifupi hii kazi ni nzuri mno na ni kazi dume niwana maana ilainafaa uwe mvumilivu ziko Episode 200 hapa. KBS1 ndio waliirusha. Iliandaliwa na Kim Jong Sun, mwandishi alikuwa Lee Hwan Kyung.
Mwaka : 2000

6. Haeshin, Sea God, Emperor of the Sea

Achana na ukatili wa Lee do hyeong, penzi la Lady Jung hwa dhiya Jam bogo na Yeom Jang. Kipindi kile naitazama bado nilishangazwa sana kwani hawa jamaa wanamng'ang'ania huyu mdada?. Miaka michache baadae ndio nilikujakuwaelewa. Nakumbuka( kama sikosei) ilikuwa Bandari ya Yangzhou mida ya jioni kabisa, Yeom Jang alimfuata Lady Jung hwa na kumwambia najua moyoni mwako yupo Jang bogo lakini mie naomba hata huo mwili wako. Hapa nilijifunza kuwa kumbe kweye maisha haya mtu aliyenamoyo wa mtu ndiye wa thamani zaidi. Lee do hyeong alikuwa akimuona huyo mwnamke kama chanzo cha udhaifu wa Yeom Jang. Kama sikosei hawa wote( Jang Bogo na Yeom Jang) hawakuweza kuishi nae mwanadada huyo. Adventure za baharini zilinivutia zaidi pia, Jang Bogo kuwa Gladiator baada ya kuuzwa utumwani. Kifupi kazii hii tamu na sijawahi kuitazama Episode ya mwisho na sina mpango huo. Mbali na yote hii ndo drama ambayo ulikuwa unamu- admire adui. Story ya drama hii inamuunganiko flani na Emperor wang gun drama, maana Gung ye ambaye ni ambaye alikuwa ni Prince wa Shilla, mama yake alikuwa binti wa Jang Bogo. Kazi hii ilitayarishwa na Il-soo Kang, akisaidiwa na Kang Byung Taek. Ilirushwa kupitia KBS2
M
waka 2004

7. Sang Do, Joseon Merchant
Utajifunza mambo mengi kuhusu biashara, kuna mambo umejifunza shuleni kuhusu Ujasiliamali lakini huku ndani utaona watu wakifanya kwa vitendo, ni kazi nzuri kweli kweli. Ilitayarishwa na mzee wetu Lee Byung Hoon, ilirushwa MBC
Mwaka 2001

8. Hur Jun, The Legendary Doctor
Inastory nzuri sana kama Jewel in the Palace, ilinivutia kwa kila kitu. Mtayarishaji ni yule yule Gwiji Lee Byung Hoon, kupitia MBC
Mwaka 1999

9. Chuno, The Slave hunter

Mara ya kwanza nilimuona Jang Hyuk ndani ya hii kazi, hutojuta kuitazama. Iliandaliwa na Kwang Jung Hwan, kupitia KBS
mwaka 2010

10. God of War, Military Official, Soldier
Hii ni kazi ya kibabe yenye story nzuri sana, utaifurahia sana. Alocheza uhusika mkuu alishapoteza maisha. Drama inamuelezea Mtumwa ambaye alipata Bahati na kuwa kiongozi Mkuu wa Jeshi na kuwa conrol serikalini( Overlord). Scene ya malavidavi kati ya mtoto wa Choe ilikuwa nzuri pia. Hii drama ni kama mwendelezo wa Dude la Kiumeni The Age of Warriors. Ilitayarishwa na Lee Hwan Kyun, ikarushwa na MBC
Mwaka 2012

Nakupa hii ya chini kama bonus

11. Shin Don

Hii drama pia inastory nzuri sana, inafanana baadhi ya Visa na Empress Ki, hii drama ni Prio story ya Jeong Do Jeon, Six flying Dragon na The Great Seer.
Drama hii ya Shin Don ilirushwa na MBC
mwaka 2004.

UNAWEZA KUTAJA ZAKO 10 ZENYE STORY NZURI ZAIDI
BBZV7f.jpg

Posta ya drama iitwayo SangDo
 
UNAWEZA KUTAJA ZAKO 10 ZENYE STORY NZURI ZAIDIView attachment 2609356
Posta ya drama iitwayo SangDo
List ya kibabe hii. Nakubaliana na wewe kwenye kigongo cha Jumong, kisiki cha Chuno, Emperor of the sea na Dong-Yi hizi ni moja ya kazi bora za kikorea kwa upande wa hitorical.

Vipi umeshacheki Emprrss Ki? Land of the Wind?. Six flying Dragons? Haziingii kwenye list yako kama honourable mentions?
 
Back
Top Bottom