Nianze kwa kicheko, nilichopenda kwenye hili andiko lako, umejiuliza na ukajipa majibu.
Kwanza kabisa nadhani umzima wa afya.
Tuanzie hapo kwa Genghis Khan the Great. [emoji1787]Huyo mwamba alikuwa nadharau sana. Yaani alitaka kumiliki Dunia mikononi mwake. Unaambiwa hivi, hakuna Mbabe yoyote yule aliye- conquer aridhi kubwa kumpita the Great Khan. Si Julian Cesar the Great wa Roman empire, wala Alexander the Great wa Macedonia. Nakwambia hivi huyo mjinga alizaliwa kuja kutafuta sifa duniani. Kama si kum-study angekonka Ulaya yote. Jiulize angeweza kuiongoza na ikaendelea nchi yote hiyo?. Pamoja na ubabe wake wote jamaa aliawashindwa Asia kusini alipigwa huko India. Miaka ile China kulikuwa na Song Empire, hawa walimnyoosha mara ya kwanza Khan the Great. Song Empire ilikuwa ndio wanauchumi mkuwa duniani. Mbali na hayo Goryeo iliyokuwa imeoza kwaajil ya uongozi mbovu, Rushwa na ubadhili fu wa mali pamoja na ukandamizaji. Bado hao vidume walitumia miaka 30 kuipiga Goryeo( ikiwa na maana waliivamia Goryeo x 8 na uvamizi wa 9 Goryeo ikajisalimisha.) Na unaambiwa hakuna Taifa ambalo liliweza kuwazuia Mongolia miaka 30+ zaidi ya Goryeo Dynasty.
Huyo mjinga Khan alienda kutoa dozi mpaka Poland, Ukraine kabla yawao kujibu.
View attachment 2614750
Anyway, Chanzo cha mgogoro kati ya China katika historical drama umechagizwa na zile historical drama za 3 Kingdoms ndio maana sio nyingi. Kwasababu Wakorea wanadai eneo lao kubwa lilichukuliwa na China wakati wa vita kati ya Tang dynasty, Goryeo( Gogryeo) na Bakje. Wakati China wanadai Gogryeo ilikuwa Dynasty yao. Hapa kuna mvutano mkubwa mno kuhusu Gogryeo( Goryeo kama ambavyo lilifupishwa na Jang Su) kila mmoja anadai ni yake na hii ni sababu kuwq 3n3o kubww la Gogryeo lilikuwa Chinq. Kuhusu suala la ubabe, ni kweli hawa wakorea wamewhi kuwa tishio katika ukanda ule wa mashariki ya mbali yote, hasa kipindi cha Muhuni anaitwq Gwanggaeto the Great, huyu muhuni aliwaheshimisha Wakorea wengi, maana Gogryeo Empire iliogopeka enzi zake, huyu Gwanggaeto alikuwa anaconquer maeneo si kwaajili kwaajili ya kupanua aridhi, bali ile ilikuwa ni moja ya njia ya kutafuta amani ili watu wa Gogryeo wakae kwa amani, yaani ulikuwa ukijidai kuamsha vita na Gogryeo wakati wake, si tu dozi utakula bali mpaka angushe utawala wako ndo anatulia( means anang'OA mizizi ya Vita dhidi ya Gogryeo, ndio maana walimpa jina ya heshima la the Peace maker, Emperor, Gwanggaeto( an expander of territories), Taewang( the Great king), huyu mwana hakuwa na ambition kama za kina Great Khan za kuongeza maeneo. Kifupi enzi za Gwanggaeto hata wachina waliwaogopa wakorea. Baada ya kifo chake, mtoto wa Gwanggaeto Jang su, alipigana vita nyingi na wachina na aliwatwanga. Mzee wangu Gogryeo walikuwa wababe sana na Gwanggaeto alikuwa rolemodel wa kila shujaa wa zile 3 Kingdoms, baadae Goryeo mpaka sasa huko NorthKorea. ,Bakje pia enzi za Geuchogo walikuwa wababe, pia shilla walikuwa wako vizuri, Dynasty kukaa miaka 1000 sio kitu kidogo kama wangekuwa weak wasingeishi hata miaka 100, maaana zamani maisha yalikuwa kuwa mwenye nguvu ndiye anaishi, kwanza ni Dynasties chache mno duniani zilizofikisha miaka 900. Nasema ukimuona simba kafa kwa uzee ujue alikuwa anajiweza.
Kilichowaangusha, Shilla,Bakje,Gogryeo, Goryeo, Joseon sababu zao zinafanana na moja wapo ushazitaja; Utengano baina yao, Uongozi mbovu ulopelekea sababu nyingi, ikiwepo rushwa, ufisadi katika familia za kifalme, hata kwa viongozi wengine, uchu wa madaraka ubinafsi na mengine mengi, nq walijikuta wanafocus na zaidi kwenye vita za kuiba mali na utisadi watu wakawa na maisha ya hovyo, hata wanajeshi walikuwa hawaheshimiki walikuwa wanaonekana si kitu na hii ndio sababu iliyopelekea wanajeshi kufanya mapinduzi kwenye miaka ya 1170 kama sikosei utawala wa kiimla ulodumu kwa miaka 100. Kabla ya kuangushwa ya Yuan( Mongolia), hata hawa wanajeshi walifanya kilekile ulafi wa madaraka, mali n.k day by day Taifa lilikuwa linaoza. Mbali na hayo yote Gogryeo, Goryeo walikuwa na baadhi ya watu wachache ambao walikuwa ni remarkable, wazalendo wana Spirit za Ajabu, mfano Vita kati ya Tang na Gogryeo was the battle of death, General Yang manchun alichokifanya pale kwenye ngome ya Ansi ni outstanding, lakini shujaa huyu kabla hata vita na Tang haijaisha wao wenyewe walimuua kuwa atakuwa tishio. Hawa wajinga walijimaliza wao wenyewe kwa ubinafsi wao wenyewe, internal factors zilikuwa nyingi kwa wao kuanguka kuliko na zilikuwa na nguvu, kuliko external, hata marabaada ya kifo cha Yeon Gaesomun migogoro ya kisiasa utengano vilizidi ndani ya Goryeo( Kokryeo), watoto wake walikwenda kutafuta usaidizi kwq Nchi adui, mfano mtoto mkubwa alienda kujiunga na Tang kisha wakaishambulia Gogryeo, achana na Hiyo Vita ya Gogryeo na Tang, kulikuwq na muhuni anaitwa General Eulji Mundoek, huyu aliwatwanga Sui Dynasty na Jeshi lao watu milioni 1.8. Unamfahamu Gang Gam Chan, aliwapiga Khitan vibaya mno Khitan. Kim Yun shin, baada ya kufanikiwa kuwaangusha Gogryeo na Bakje, Tang walichukua eneo kubwa na hata kidogo kilichobaki, bado Tang walikuwa na control nqcho mpaka hata ndani ya shillq nq jamaa aliwapiga na kuwaondoa, kisha Shilla ikawa na kontroo kwenye 3 Kingdoms.
Kwakifupi hawa wakorea kama wangekuwa wadhaifu walawasingekuwepo, hawa walikuwq wanapigwa sababu zao za kisiasa, ila mashujaa walikuwa nao wengi na walofanya makubwq.
JOSEON DYNASTY, wao walipunguza kujenga jeshi kwa sababu walitaka kuboresha maisha ya watu wa chini na kuhakikisha wanapata elimu, uboreshwa wa zana bora za kilimo vilifanyika hapa wakati wa Sejong the Great, nq pia wengi walokuwa wanajeshi walip3lekwa mashambani ili kuongeza kazi ya uzalishaji mazao ili kukabiliana na janga la njaa. Hii ndio ilikuwa ni focus ya Joseon. Na ni moja ya sababu iliyopelekea Joseon kutokuwa Jeshi imara. Ila wakati huu wa Sejong Joseon ilizidi kupata ustarabu mkubwa sana wa maendeleo ya uchumi, sayansi, na elimu. Pamoja na mambo mazuri yaliyofanyika wakati huu bado Sejong aliapata upinzani mkubwa toka kwa Wakorea wenyewe ambao walikuwa wakitetea maslahi yao kwa china( Ming Dynasty), sababu zingine za Joseon kutokuwa na Jeshi imara ni negative factors kama amabazo ulizitaja.
Kuhusu wasomi, ni kweli hawa jamaa walikuwa na wasomi wengi sana ambao sitowamaliza ila Elimu yao ilikuwa Inspired na Elimu ya China( Confucianism) hii ilipelekea kuwa na wanafalsafa( Early& Neo- Cofucianist philosophers) mfano Sambong alitaka kuanzisha mfumo constitutional monarchy enzi hizo ndo baadae wazungu nao wakaanza kufanya, walimuua na kuona kama alikuwa ni anania ya madakara na kuikosea heshima familia ya kifalme., ni ukwel usiopingika kuwa jamaa walikuwa wamestarabika na walijifunza vingi kutoka China na Japan sababu wao walikuwa wamepiga hatua kubwa sana kiuchumi, kielimu, kiteknolojia. Sababu China ilikuwa inapokea watu kutoka mpaka Ulaya sababu walikuwa wanakwenda kufanya biashara, na pia wachina walikuwa wanazunguka duniani kwa ajili ya biashara. Na hata sisi huu ukanda wetu tumeqnza kufanya biashara na wachinq tangu Karne ya 1. Kwahiyo walijifunza mengi duniani, hivyo waliendelea sana kuliko wakorea. Unaiona Song Dynasty inakadiriwa kuwa ilikuwa na uchumi mkubwa kuliko hata Roman Empire, pia hata Ming na Quing dynasties zilikuwa zinaongoza kwa uchumi mkubwa duniani, wakifuatiwa na India then France. Uchumi wa China ulishuka baada ya back to back Vita na Britain na Japan miaka ya 1800s-1900s
Hakuna Drama iliyoandikwa kinyume cha history, unless director awemeongeza. Mfano Ukitaka kujua struggles halisi mpaka Joseon ilianzishwa itazame zaidi Jeong do Jeon sababu yenyewe ilijikita zaidi katika history kuliko Six flying dragon ambayo director aliwaongeza, wahusika na matukio ambayo kihistoria hayapo na alifanya hivyo ilikunogesha watazamaji na kuweka utofauti na ile drama ya Jeongdo Jeon(2014). Pamoja na hayoz badoWachina na wajapan wachorwa kwenye hizi drama kuwa wameendelea kuliko hata Wakorea. Historical drama zote zimeonesha haya, na hata wasomi, madaktari, na wanasiasa na wafanya biashara wengi walikuwa Inspired na wachina.
Tafadhali nitajie drama iliyochezwa kinyume cha history.
Namaliza kwa kusema,
Hivi historia inatunza nini ili kushep fyucha zetu?, je wakorea hawajawahi kuliju hili Tangu enzi za Dynasties zao zote mpaka wakati wa Korea Empire sababu zilizowaangusha ni zilezile.
Kifupi Wakorea hawakuwa wanyonge bali wamezungukwa na watu imara nawameweza kudumu mpaka sasa. Ni ukweli usiofichika kuwa bado mpaka sasa, China na Japqn ni wakubwa kwa Korea( SK&.NK). Ubinafsi baina yao ulipelekeq Marekani na Urusi kuwatenganisha. Ingawa ni miongoni mwa Mataifa yenye nguvu za kiuchumi, Kiteknoloji na Kijeshi duniani. Waza tu, kama North na South wakaungana basi ni balaa jipya duniani litakuwa limetengenezwa. Na marekani hatoruhusu hili litokee.
Si unaona Moon Jae in ambavyo alitaka kuweka ukaribu na North nini kilitokea?, na sasa Raisi wa korea ni kibaraka wa marekani.
Kwa taarifa zaidi kasome.
Samguk Sagi,
Goeryeosa,
Annals of Joseon
Maana kilichoandikwa kwenye vitabu hivyo ndicho kilichopo kwenye historical drama nyingi.
Asante.