Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Mimi mapanga napenda sana ila huwa nakereka historical drama ziko na 'vawulence' sana. Yaani kuna watu wako juu ya sheria kabisa...mtu anamtengenezea mwenzie zengwe anauwawa na familia yake yote [emoji26][emoji26]
Halafu nashangaa kwa nini watu wanalilia kuwa wafalme wakati mimi naona katika watu wanaoishi kwa tabu basi ni wafalme... yaani mtu anakuwa tu kama roboti...hawezi kufanya jambo lolote na maisha yao yanakuwa hatarini kulishwa sumu kupo nje nje tu....hapo hapo kuna yupo tayari kuua ndugu yake ili awe king/ crown prince
 
Aisee watu mko deep.
 
Ni kama viongozi wetu wapo tayari kwenda kwa waganga na kufanya lolote kisha wanaishia kulalamika ati uongozi ni mzigo,uongozi mgumu. Huwa naona kwa wafalme na viongozi wowote anaefaidi sana ni mpambe. Mfalme anakua mtu wa kuweweseka muda wote huku akiogopa kuuliwa
 
Missing the other sides season 2 nimeipenda. Napenda drama zinazohusu mizimu(ghosts)hasa wasiotisha. Humu inaelezea watu walifariki kwa kuuliwa ama ajali kisha miili yao ikazikwa kwa kificho hivyo wanajikuta kwenye kijiji wasichokifahamu. Mwili ukigundulika anapotea kule kijijini.

Nianze safari ya kuivuta season 1 nayo nione yaliyomo

Variety show three meals a day. wanakula hawa watu kama mchwa😂😂😂😂
 
Pole sana, maana hizi historical drama zetu hasa kuanzia Goryeo mpaka zile za 3 Kingdoms zimekaa kiume sana, lazima uwe na moyo wa chuma. Kwanza mie ndo napenda historical yenye Episode nyingi.
Mfano Emperor wang gun in episode 200. Nilitumia mieza 11 kuimaliza wakati Daemusin( MZANZIBARI) Alitumia miaka 2.
The Age of Warriors ina Episode 158 na nyingine nyingi.

Mie nakupa recommendation ya Princess Ja myung Go. Episode 39 tu.

Hii drama kwakuwa na story nzuri sana naweza kuiweka meza moja na Dae Jang Geum & Dong yi. Kwenye ile list yangu sikuiweka sababu niliweka kwenye category nyingine ambayo nitashare. Hakuna drama ambayo iliwahi kuvuta hisia zangu kama hii.
Huyu dada(Princess Ra-hee)nilimchukia sana kupitia drama hii, yaani aliuza Nchi kisa mapenzi. Alidhani anamkomoa dada yake( Princess Ja myung Go), maana wote hawa mpenzi wao alikuwa ni mmoja Prince Hodong wa Gogryeo mtoto wa Mfalme Daemusin( Muyul).

👆🏽Princess Jamyung Go

Drama nzuri sana, ila uwe na leso karibu ili ufutie machozi.

Nipe recommendation za Family drama.
 

Hizo zinakuwaga nzuri ila mimi hadi naota
Sa kutizama lazima nijue akili yangu ipo sawa maana usiku

Kuna moja niliishusha bi/bw harusi na photograher wanapiga picha uko maporin mara kisiki kikabubujika we nikastop kwanza

Nimeisahau jina ila nimeshusha siku kichwa kikiwa tulivu naitazama
Hata blind lile giza nikaacha kuitazama, kiporo


Three meals nilitazama ile ya hospital playlist
Halaf uyo Director inaelekea anakubalika sana.
 
Huyo director inaonekana anapenda misosi mno😂😂😂naona kila variety yake seo jin anakuwepo

Ya hospital playlist sijaiona nitaitafuta

Aah ile inaitwa island niliiangalia mpaka mwisho japo kwa kupeleka mbele pale wakianza kubadilika na kuweka masura ya kinyaa hata kuangalia haikai poa. Blind sijawah hata kuidownload
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…