Age of warriors, ukikutana na handsome boy humu ndani nitakulipa.
ni mwendo wa kutuonyesha mtiririko wa matukio yote ya kidikteta yaliofanywa na wanajeshi walioamua kuvua gwanda na hatimaye kujiingiza katika ulimwengu wa siasa.
Kundi fulani la wanajeshi wanampindua mfalme 18 wa Goryeo na kuondoa civillian government baadae wanamweka mdogo wake ili wasionekane wamefanya tendo hilo kwa nia chafu kwa amri ya queen dowager.
yi uibang: huyo mzee aliyeigiza uhusika wa yi uibang utamuona kwenye emperor wang guhn ambapo ameigiza uhusika wa mfalme kyu hyun from later baekje. Madaraka yanamtia upofu kiasi ambacho alifikia hatua ya kuwasambaratisha marafiki zake wawili muhimu ambao kwa muda mrefu walikuwa na ndoto kwa pamoja ya kuinyoosha goryeo iliokwisha poteza muelekeo. kuanzia mwaka 1170 hadi mwaka 1174 jamaa ndiye aliyekuwa ameshikilia mpini wa maamuzi ndani ya goryeo,
karma is bitch bwana yi ui bang alikufa kifo cha aibu sana. Aliyemuua ni mtoto wa jeong jung bu.
jeong jung bu: kifo cha bwana yi ui bang kilipelekea kubadilika kwa upepo hatari wenye uwezo wa kuvunja ghrofa za burji khalifa, ukoo wa yi ulipoteza nguvu na hatimaye ukoo wa choe ukashikilia nguvu ya kuiendesha royal family. Huyu mzee kwa kushirikiana na mwanawe walitenda matendo zaidi ya yale aliyoyatekeleza yi ui bang. Karma is bitch baadae alijitokeza bwana mdogo ambaye inasemekana alikuwa na miaka 26 tu ya kuzaliwa na jina lake aliitwa gyeong dae sung, huyu general ndiye aliyeongoza kampeni ya kumuondoa madarakani jeong jung bu na koo yake nzima. hatimaye jeong jung bu, mwanawe, mkwe wake na kizazi chote kinachotokea koo ya choe walikutana na mkono wa kifo. jeong jong bu alishika madaraka kuanzia mwaka 1174 hadi mwaka 1179.
gyeong dae sung: alichukiwa mnooo na mfalme, vitabu vya kihistoria vya joseon havikumrekodi vibaya huyu jamaa. hakuwa na uchu wa madaraka na alijaribu kurudisha mfumo wa serikali kama ilivyokuwa mwanzoni (civillian govenrment) lakini alikutana na upinzani mkali sana kutoka kwa wanajeshii na hata mfalme mwenyewe, jamaa inasemekana alifariki kwa ugonjwa. alitawala kuanzia mwaka 1179 hadi 1183.
yi ui min: huyu muhuni ndiye aliyemuua mfalme wa mwanzo kwa amri ya bwana yi ui bang, cha kuchekesha zaidi amri ya kifo ilitoka moja kwa moja kwenye royal family ndani ya chumba cha queen dowager (yaani queen dowager alitoa amri ya kuuliwa mwanawe wa kumzaa kwa mujibu wa drama), huyu fala na yeye aliyatumia madaraka yake vibaya sana pamoja na watoto wake wawili wakorofi kiasi ambacho hakuona tabu kuwanyanyasa kingono watumishi wa royal family, kudhulumu mali za walala hoi, Yi ui min maisha yake yaliishia mikononi mwa jamaa mmoja anaitwa choe chung heon. Yi ui min alitawala kuanzia mwaka 1183 hadi mwaka 1196.
choe chung heon: baada ya kufanikiwa kumsambaratisha bwana yi ui min hatimaye jamaa akawa ndiye bosi mkuu wa goryeo, huyu jamaa pamoja na ukoo wake waliitawala goryeo kwa muda mrefu sana kwa njia ya kurithishana madaraka (baadae walitawala watoto wake choi woo, choi hae, choi ui).Madaraka yalimtia upofu na woga kiasi ya kufikia hatua ya kumsambaratisha ndugu yake.
Kwenye drama hii utawala wa kijeshi uliishia hapa, ila kiuhalisia ulikwenda mbele zaidi.