Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

jamani kuna hizi series mbili za mwaka huu mzidowload jamani ni nzuri sana, mi huwa naangalia online. ya kwanza hii ambayo watu tayari wameitaja tho bado haijaisha lakini ni balaa. ina episodes 16 mpaka sasa wameshaonyesha episode 14 mbili zinaisha week ijayo. inaitwa descendants of the sun, na nyingine inaitwa jackpot (daebak) ndo kwanza ina episode 4, si mchezo jamani ni shidaaa.
 
Wapenzi wenzangu wa Korean Movies And Series Pata App Yenye kukidhi Haja zetu....
Watch online and Download for freee.....
#Dramania download hiyo app hapo....
 
na mtu kama anapenda kuangalia reality show ya hao watoto the triplets wa kiwa na huyo baba yao inaitwa "the return of superman", ni show ambayo ni nzuri sana watoto hao wanafurahisha sana. wameamza kuigiza, actually sio kuigiza wanafanfanya vile ambavyo wanaona inafaa kwasababu ni watoto hawajui chochote. imeshaisha, ni show ambayo ilianza toka walivyokuwa wadogo mpaka sasa wana miaka minne. show imeisha nafikiri mwezi wa pili kama sio watatu. they are funny kids jamani, mtaifurahia
 
Naomba nifahamu filamu nyingine alizocheza Choi soo jong, maana jamaa nimemkubali aisee ni bingwa wa hisia sijawahi ona, pia ana dialogue za ukweli balaa!
 
City Hunter
Warrior Baek Dong So
A Man Called Himself God
Heart Strings
ila kiboko ya yote ni Athena Goddes of War
 
images

Movies
Drama Series
Asante mkuu!
 
Wanaopenda "historical drama series" angalieni "sword and flower/ the blade and petal" ina kila aina ya vitendo vya kufurahisha, kusisimua na hata kuhuzunisha (wivu, ubabe, mapenzi, usaliti, nk).
 
Mzigo mpya... 'Jackpot'/the "royal Gambler"
baada ya 'six flying dragons' kuisha sasa hivi imeanza iyo Jackpot.... bonge moja la historical drama...
 
Mzigo mpya... 'Jackpot'/the "royal Gambler"
baada ya 'six flying dragons' kuisha sasa hivi imeanza iyo Jackpot.... bonge moja la historical drama...
Hebu tupe dondoo kidogo maana Nina ulevi na hizi historical drama.
 
Jackpot:

Inahusu uhasama uliopo kati ya msomi mkubwa wa kipindi iko na Mfalme wa Joseon wa wakati huo.... uyo mwanazuoni/msomi anataka kulipa kisasi kwa mfalme na kuwa mtu mwenye power kuzidi ata mfalme maana mfalme ndo mtu anayeogopewa kiasi cha kuitwa "Beast"

Uyo msomi ana mastermind kila kitu kinachohusiana na Palace na serikali ya Joseon kwa ujumla... anapandikiza maafisa na kutoa rushwa kwa kila mtu anayeona ana nguvu katika serikali ile afanikishe kisasi chake...

Moja ya plan zake ambazo ndo kama "core" ya hii movie ni kumpandikiza mwanamke ambaye aliolewa na mcheza kamali ambaye ni addicted na ku-gamble... kuna plan anaisuka apo matata mpaka anahakikisha uyo mwanamke anakua moja ya wake za mfalme... ila uyo mwanamke atapata ujauzito ambao atajifungua kabla ya miezi 9!!

Hali iyo ya kujifungua mapema itazua taharuki ktk Palace hasa ukicheki background ya uyo mwanamke... itaonekana yule mtoto sio wa mfalme... Alaf uyo dogo aliyezaliwa chini ya miezi 9 ndo mmoja wa sterling wa drama...

Kingine kizuri kuhusu hii movie inahusisha mambo ya michezo ya kubet ila betting za humu mtu anaweza kuweka rehani ata maisha yake...

kingine ninachokikubali ni ule undava na umafia wa uyo msomi mkubwa wa wakati huo... uwezo wake wa ku-manipulate situation ila bado anashindwa kuuvaa mziki wa mfalme wa Joseon... mambo ya kulipiziana kisasi na Martial arts za kueleweka!!!
 
Back
Top Bottom