Nifah na Khantwe: "historical drama" hasa za mahusiano hugusa sana mioyo ya watazamaji kwa kuwa kuna uhalisia unaofanana na maisha yetu hapa. Tamthilia zingine za Korea za kisasa zinaiga za majuu.
Nadhani 'producers' wa filamu zetu kuna umhimu kutengeza filamu au tamthilia za hali halisi ya maisha yetu hasa kabla ya uhuru. Naamini zitapata soko kubwa ndani na nje ya nchi. Hii yawezekana kwa kutumia vitabu vya historia, simulizi zilizoandikwa na zisizoandikwa km mapigano kati ya kabila na kabila, unyampala (kodi ya kichwa), mapenzi na ndoa enzi hizo, nk