MY BEST KOREAN YOUNG ACTOR AND ACTRESS (U 25)
(Part 1)
1.
YEO JIN GOO:
View attachment 429300
kwangu mimi ndie muigizaji bora linapokuja suala la kuwashindanisha young actor,amezaliwa 1997 na nimebahatika kumuona kwenye drama mbali mbali kama vile
GIANT,
WARRIOR BAEK DONG SOO,
JACKPOT,
THE MOON THAT EMBRACE THE SUN na
PRINCESS JAMYUNG.nilimpenda kwenye PRINCESS JAM YUNG ambapo alicheza kama prince Hodong kuna sehemu alitumwa na baba yake DAMUSHIN MUHYOOL ambaye alikuwa ni mfalme wa tatu wa taifa la goguryeo aende Naklang kwa ajili ya kumposa princess lahee kilichotokezea ilikuwa ni shidaa siwahadithii.
2.
PARK JI BIN:
kila mwanadamu amezaliwa na kipaji ila wengine wamezidishiwa vipaji akiwemo mwanadamu huyu ambaye amezaliwa 1995.ameigiza drama nyingi kama
YI SAN,
QUEEN SEONDEOK na
BOYS OVER FLOWER ambapo alicheza kama ni mdogo wake na jan di, hahahahaaaa kiukweli familia yao ilikuwa ni balaaa kuanzia baba mpaka mtoto kwenye BOYS OVER FLOWER, kwa sasa ameamua kwenda kutumikia jeshi.
3. PARK GUN TAE:
amezaliwa 1996,inawezekana sijaangalia drama nyingi sana alizoshiriki ila kwenye
WARRIOR BAEK DONG SOO ushirikiano wake pamoja na YEO JIN GOO ulikuwa ni bora sana na kuifanya drama kuwa ni ya kuvutia tokea mwanzo.pia ameigiza drama kama vile
KIM SO RO,
ORANGE MARMALADE,JUNG YI GODDESS OF FIRE,
PRINCESS JAMYUNG,
THE MERCHANT GAEK JU na
EAST OF EDEN
4.
LEE HYUN WOO:
View attachment 429308
amezaliwa 1993 mara yangu ya kwanza nilimuona kwenye
LOBBYST ambapo alicheza kama harry,baadae nilimuona kwenye
THE GREAT KING SEJONG,
GYE BAEK ,
MOORIM SCHOOL pamoja na
SCHOLAR WHO WALK IN THE NIGHT
5. NO YOUNG HAK:amezaliwa 1993 kwenye THE KINGS DREAM alicheza kama kim yusin ambapo alishinda tunzo ya best child actors,pia ameigiza drama kama vile THE GREAT SEER,TRIANGLE,THE DUO,KING AND I, JINGIBROK:THE MEMORY OF IMJIN WAR.
View attachment 429305
6. LEE MIN HO:usichanganyikiwe wapo wengi nchini korea wenye majina yanayofanana,mara ya mwanzo nilimuona kwenye GUTALE OF THE FOX CHILD (GUMIHO) kusema kweli alinivutia na alinishajihisha nitafute kazi yake nyengine na nilibahatika kumuona kwenye THE MOON THAT EMBRACE THE SUN,SUNGKYUNWAN SCANDAL,HWAJUNG,SWORD AND FLOWER,THE GREAT SEER.
7. JUNG YOON SUK:amezaliwa 2003 nilianza kumuona kwenye JUMONG ambapo alitumika kama prince yuri na alikuwa na miaka 3,mpaka leo amekuwa akitumika kwenye drama nyingi sana kama vile YONG PAL,SIX FLYNG DRAGONS,JEONG DO JEON,FIVE ENOUGH,FLOWER IN PRISON na cha kuvutia Zaidi alitumika kwenye JANG YOUNG SIL ambayo imemkutanisha tena na song il kook baada ya miaka 10 tokea wakutane kwenye jumong.kiukweli ni mmoja kati ya watoto wanaofanya vizuri sana ukilinganisha na umri wake.
View attachment 429309 View attachment 429602
View attachment 429603
8. YOO SEUNG HO:amezaliwa 1993 sijui kama bado anastahili kuwa katika kundi hili kwa sababu jamaa amekuwa hodari sana jambo ambalo limemfanya kupokea ofa nyingi akicheza kama main character tofauti na wengine hapo juu.amecheza drama kama QUEEN SEONDEOK,I MISS YOU,WARRIOR BAEK DONG SOO,YOU ARE BEAUTIFUL,KING AND I,IMMORTAL ADMIRAL YI SOO SHIN.
View attachment 429311 View attachment 429605
9. KIM YOO JUNG:amezaliwa 1999,amebarikiwa kuwa na kipaji kikubwa sana na kiukweli anawakimbiza sana wenziwe na sifikirii kama kuna mtu ambaye anafuatilia drama za korea na akawa hajashuhudia kipaji cha binti huyu.ameshiriki drama kama vile ILJIMAE,ROAD NO 1, CAIN&ABEL, MAY QUEEN,SECRET DOOR,THE MOON THAT EMRACE THE SUN,GUMIHO,na pamoja na drama inayoendelea hivi sasa kupitia KBS tv inayoitwa LOVE IN THE MOON LIGHT akiwa pamoja na PARK BOGUM
View attachment 429312
10. KIM SO HYUN: amezaliwa 1999 nchini AUSTRALIA ila miaka 5 baadae walihamia nchini korea,miongoni mwa drama alizoigiza ni KING OF BAKING,THE MOON THAT EMBRACE THE SUN,I MISS YOU,TRIANGLE,ROOFTOP PRINCE,THE GIRL WHO SEE SMELL,WHO ARE YOU.
View attachment 429354