Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Huelewi uigizaji wao ila umeelewa kuwa wakorea wanaiga...hii nayo kali
Ni kweli wakorea wanaiga wajapan japo mie sio mpenzi wa movie za wajapan ila movie nyingi tu huwa wanaiga hao wajapan,we fuatilia hilo sio lazima uwe mfuatiliaji wa movie za wajapan ndio uweze kujua.

Nimetoa mfano wa Liar game ambayo baada ya kuicheki ya kikorea nikataka kujaribu kuitizama na ya wenyewe wajapan,japo wakorea wamecopy na kupaste ila ya wajapan ilinishinda maana kama nilivyosema huigizaji wao siuuelewi na pia nilijaribu Liar and his lover pia ilinishinda.
 
Daah leo nimeshinda na hawa watoto kuanzia kwenye page ya baba yao insta, page za mashabiki YouTube huko yaani acha tu
hahahaaa mimi tokea episode ya 34 walivyojiunga na show ya return of superman mpaka episode ya 116 ambayo ilikuwa ya mwisho kwao wao nilizifuatilia na kuziangalia bila ya kunichosha.
kwa sasa kbs tv wameamua kuzirejea tena special episode kwa ajili yao tu basi bado nazifuatilia hususan ninapokuwa na njaa. Noona tafadhali usije ukampindua mwanamama jung seong yeon
 
Ni kweli wakorea wanaiga wajapan japo mie sio mpenzi wa movie za wajapan ila movie nyingi tu huwa wanaiga hao wajapan,we fuatilia hilo sio lazima uwe mfuatiliaji wa movie za wajapan ndio uweze kujua.

Nimetoa mfano wa Liar game ambayo baada ya kuicheki ya kikorea nikataka kujaribu kuitizama na ya wenyewe wajapan,japo wakorea wamecopy na kupaste ila ya wajapan ilinishinda maana kama nilivyosema huigizaji wao siuuelewi na pia nilijaribu Liar and his lover pia ilinishinda.
Angalia release year
 
hahahaaa mimi tokea episode ya 34 walivyojiunga na show ya return of superman mpaka episode ya 116 ambayo ilikuwa ya mwisho kwao wao nilizifuatilia na kuziangalia bila ya kunichosha.
kwa sasa kbs tv wameamua kuzirejea tena special episode kwa ajili yao tu basi bado nazifuatilia hususan ninapokuwa na njaa. Noona tafadhali usije ukampindua mwanamama jung seong yeon
Omo omo siwezi kumpindus bhana ila nitaenda kuomba kazi nyumbani kwao niwe nashinda nao sipati picha
 
Mwaka ambao zilitoka
Liar game ya wajapan:
Release Date: April 14 - June 23, 2007.

Liar game ya wakorea:
Release Date: October 20 - November 25, 2014.

Hivyo utaona wajapan ndiyo wakwanza kurelease,hata hivyo mie naipenda korean version.
 
  1. popote pale alipo mwanamme mwenye mafanikio ya kimaisha basi nyuma yake yupo mwanamke, ni kauli yenye ukweli ila kiupande fulani ni kauli dhaifu. Mwanamke mrembo pekee ndiye mwenye uwezo wa kumfanya mwanamme kuwa na mafanikio makubwa ya kimaisha yatakayomfanya atimize malengo yake aliyojiwekea.Nakusudia urembo wa kuwa na maarifa makubwa yatakayomsaidia mwenza wake na kuwa naye bega kwa bega mpaka kufikia malengo makubwa walioyakusudia na si urembo wa sura yake.laiti kama mafanikio ya mwanamme yanatokana na mwanamke mwenye sura nzuri na si maarifa yake basi mama zetu wangedharaulika.
  2. kama huna tamaa ya kufanikisha jambo fulani katika maisha basi katu kwenye maisha hutofanikiwa, haijalishi hali yako ya kimaisha ni nzuri au ni mbaya basi jipe moyo kuwa kuna siku utafanikiwa. Maisha yetu ya kimasikini tuliokulia udogoni yanatufanya tusahau malengo yetu ni yepi ambayo tunataka kuyakamilisha tunapokuwa wakubwa hali ambayo inatufanya tuwe tunahangaika na kuteseka kwenye maisha yetu ya ukubwani.
  3. bado hatujachelewa kufanikisha malengo yetu haijalishi una miaka 40 na huna hata shilingi 500 ya hakiba mfukoni mwako, ifufue sasa ndoto yako ambayo uliizika ulipokuwa mtoto hata kama umesahau kaburi ulioizika ndoto yako au tengeneza ndoto mpya unayotaka kuitimiza kwenye maisha yako kabla hujaonana na muumba wako kama unamuamini yupo.
  4. nikushukuru tena sana mbelwaz kwa kushare nasi taarifa mbali mbali za korean drama, strongest deliveryman ndio drama yangu bora kwa mwezi huu kiukweli imenifunza mengi sana.
 
ni takriban miezi miwili imepita tokea SBS tv wakatae pendekezo la muandishi mashuhuri wa korean drama mwanamama kim eun sook la kutaka kazi yake mpya ya MR SUNSHINE (2018) iwe chini ya usimamizi wa kituo hicho cha televisheni, sababu kubwa ni gharama za uzalishaji wa drama hiyo ni kubwa sana ambapo inakadiriwa bajeti ya episode moja tu ya MR SUNSHINE ambayo muigizaji mkuu atakuwa ni LEE BYUNG HUN ni won billion 1.5 ambapo kwa episode 20 gharama zitakuwa ni won billion 30(usd million 27).

lakini kwa upande wa pili shirika la utangazaji la korea (KBS tv) siku nne zilizopita wameamua kutangaza kuisimamia drama mpya ya kipelelezi ya mwaka 2018 inayoitwa Prometheus: War of Fire ambayo bajeti yake inakadiriwa kuwa ni won billion 30.
ni gharama kubwa sana ukilinganisha na gharama zilizotumika kwenye descendent of the sun ambayo iligharimu won billion 13 kwa epidose 16.

Ni drama ambayo itazungumzia maisha ya mwanasayansi aliyebobea katika masuala ya nyuklia wa korea kaskazini aliye na taarifa nyeti za nchi yake zinazohusu uzalishaji wa makombora ya masafa marefu aliyekimbia nchi yake na kujificha jambo linalosababisha takribani nchi tano zenye nguvu kumfatilia ili waweze kumtumia kwa ajili ya maslahi ya nchi zao.
takribani nchi tano zitatumika kama ni film location ya drama hii ambayo mpaka sasa hakuna muigizaji hata mmoja aliyetangazwa wala hakuna hata director na muandishi aliyetangazwa.

kampuni ya JL Media Group ndio ambayo imepewa haki ya usimamizi wa drama hii, kampuni hii ndio pia ilisimamia drama kama vile IRIS, PRINCESS MAN, SLAVE HUNTER.
 
Khantwe na aminas hawa jamaa zenu wasinifanye niwe mjinga,
  1. kwenye while you were sleeping muna watu watatu wenye uwezo wa kuona yatakayotokezea mbele kwa kutumia ndoto wanazoziota
  2. kwenye drama ya Black muna msichana ana uwezo wa kuona kivuli cha kifo cha mtu.
  3. sasa si wanifanyie mipango na mimi nione maisha yangu ya baadae na ikiwezekana kama yatakuwa mabaya basi wayabadilishe angalau niwe na utajiri japo wa trillion 200. pumbavu zao.
2017092001001626100118061.jpg

The main character is Black, a Grim Reaper who inhabits a human body ( a detective ) and falls in love with a woman, Ha-Ram, who can see shadows of death. These two struggle to save the lives of people. His love will break the rules of the heavens, and the grim reaper will be erased from the memories of everyone on Earth.

Black Episode 1 EngSub
 
strongest deliveryman ndio drama yangu bora kwa mwezi huu kiukweli imenifunza mengi sana.
Mimi niliishia ep 8 na kuamua kuachana nayo!
Can you imagine? Nimetazama hadi ep 8 lakini bado sioni muelekeo wa drama.. aaah sipendi kuharibiwa bando langu.
Damushin sunbae-nim, hebu ni-convince nikaiendeleze (bila ya kutoa spoilers).
 
Ha!ha! The strongest deliveryman ni the best kwasababu hauwezi kutabiri kile kitakachotokea wakati unaona group hili limeshikilia biashara baada ya Siku kadhaa wanafanyiw fitina wanaanza tena na hayo ndiyo maisha yalivyo kuna kupanda na kushuka na kila MTU anapambana ili mkono uende kinywani

sent using TV ya chogo
 
Ha!ha! The strongest deliveryman ni the best kwasababu hauwezi kutabiri kile kitakachotokea wakati unaona group hili limeshikilia biashara baada ya Siku kadhaa wanafanyiw fitina wanaanza tena na hayo ndiyo maisha yalivyo kuna kupanda na kushuka na kila MTU anapambana ili mkono uende kinywani

sent using TV ya chogo
Huenda na hii ilikuwa 1 ya sabubu zilizofanya niishie ep 8.

Kwangu nilihisi kama vile drama haisongi mbele na ina-bore kutoka na kila ep kuwa na events zenye kujirudia & scenes ambazo niliona hazina ulazima kuwepo.

Nilihisi kama vile naibiwa ilimradi tu kurefusha stori ya drama na kukamilisha episodes..
Ukija kwenye chemistry ya hao main actors ndio kabisaaaa.. (utadhani wamelazimishwa) aaaaargh!

Storyline yake kwangu haisisimui & yakawaida sana! SIJUI NIKO PEKE YANGU, wakuu?
 
Dramas nyengine ambazo nimeishia nazo njiani ni hizi:-

While You Were Sleeping x E10
Andante x E01
 
Back
Top Bottom