Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Dramas za Love Triangle nakuwa immersed nazo vibaya hadi nafikia kulia na kuumia mimi badala ya muhusika wa kwenye Drama. (I'm introverted and empathetic by nature)

Haki ya nani zinanipa stress na depression.
Kuna yeyote mwenye ku-relate na hii hali, Wakuu?
jaribu kuitafuta na temperature of love.
 
  1. umefanya kosa kubwa sana na malaika ameshakuandikia dhambi kwa kitendo chako cha kumwita king gwaggaeto na ili dhambi yako ifutwe unapswa ukasujudie ukuta wa gwaggaeto stele. ulipaswa uanze na The great king gwaggaeto a.k.a taewang gwaggaeto, a.k.a go damdeok, a.k.a Broad Expander of Domain, a.k.a peace maker,mwanadamu aliyerudisha heshima ya goguryeo kwa kuwafunza adabu mataifa kama baekje, shilla, japan,khitan,china na maeneo ya urusi na bahati mbaya sana alikufa akiwa na pungufu ya miaka miwili kufikia miaka 40 na laiti kama angeliishi miaka 20 zaidi naamini kwa kutumia jambia lake angelifika hadi nyanda za juu kusini alikotokea babu yake Khantwe.
  2. ni wafalme wawili tu ndio waliopewa heshima ya the great katika eneo la korea na mwengine ni the great king sejong ambaye alikuwa ni mfalme wa nne wa joseon. mnamo mwaka 396 mfalme gwaggaeto aliuteka mji mkuu wa taifa la baekje ambao uliitwa Wiryeseong ambapo kwa sasa ndio panaitwa Seoul ambao ndio mji mkuu wa korea kusini. wakati anaipiga baekje alikuwa na miaka 25 tu.
  3. mnamo mwaka 399 aliongoza kikosi cha wanajeshi 50000 na kuelekea taifa la Silla na aliwasambaratisha wajapan waliokuwa wanaleta fujo nchini shilla, baada ya hapo wajapan na shilla wakaamua kujisalimisha kwa goguryeo.
  4. baadae akawatwanga wachina wa Xianbei na akarudisha eneo la liaodong ambalo kabla ya kuanzishwa kwa goguryeo ilikuwa ni eneo la gojoseon kabla taifa hili halijaangamiza na china (han dynasty)
  5. mnamo mwaka 371 ambapo ilikuwa ni miaka 3 kabla hajazaliwa go damdeok taifa la goguryeo lilipoteza nguvu yake ya kiutawala kwa ndugu zao ambao ni baekje chini ya mfalme wao aliyejulikana kwa jina la geunchogo ambaye ndiye mwanadamu aliyeifanya baekje kuwa ni taifa tishio.mfalme geunchogo alimuua mfalme gogukwon wa goguryeo na kuuteka mji wa pyongyang ambao kwa sasa ndio mji mkuu wa korea kaskazini. mfalme gogukwon ndie mfalme pekee kwenye nchi ya goguryeo kufia vitani na alirithiwa na mwanawe aliyeitwa go gubu (king sosurim).
  6. mfalme sosurim alikufa bila ya kuwa na mtoto ndipo akatawala mdogo wake aliyeitwa go iryeon ambaye ndiye baba wa go damdeok (gwaggaeto)
  7. muigizaji Lee tae gon ndiye aliyeigiza nafasi ya damdeok kwenye drama ya king gwaggaeto lakini umenikera mjr95 uliposema jamaa anamzidi song il kook. Ili amzidi song il kook anapaswa kwanza amzidi choi soo jong na jang hyuk
    Lee-Tae-Gon-14.jpg
  8. link ya king geunchogo drama https://ondramanice.io/drama/king-geunchogo-detail
Mimi mgeni hapa ila Thank you wanajamvi napendaga sana hizi series has ikiwa ya kijiji mjini sina habari nayo.....king gwagwaeto tayari naombeni link ya Empress Ki
 
Mkuu wa hiz kazi nipe maelezo ya kutosha kuhusu hili goma
dae jang geum alikuwa ni msichana aliyetokea katika tabaka la chini wakati wa utawala wa joseon na alikutana na changamoto nyingi sana ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia (mfumo dum) lakini alipambana mpaka kufikia kuingia ikulu na kufanya kazi za upishi na hadi kuwa daktari wa kwanza wa kike wa mfalme katika historia ya joseon.
ni drama ambayo ilikuwa na wastani wa kuangalia nchini korea wa 47% na hadi sasa inabaki kuwa ni miongoni mwa drama zilizoangaliwa zaidi nchini korea.
inakadiriwa bajeti ya drama hii ilikuwa ni usd 15 million ambapo kwa pesa ya kwetu sisi kwa wakati huu ni kama billion 35.
takribani nchi 90 zilinunua haki miliki ya drama hii na inakadiriwa mauzo ya drama hii nje ya korea ni usd million 105 ambazo ni kama billion 230 kwa pesa ya mzee wa chato.
 
Mimi mgeni hapa ila Thank you wanajamvi napendaga sana hizi series has ikiwa ya kijiji mjini sina habari nayo.....king gwagwaeto tayari naombeni link ya Empress Ki
karibu joseon ya tanzania na huduma za vyakula na vinywaji kama makgeoli, kimchi, soju, dumpling,bibimpap (mixed rice ),bulgogi,haemul pajeon vyote vinapatikana.
%EC%A1%B0%EB%A6%AC%EC%82%AC%EC%A7%84.png

http://kissasian.ch/Drama/Empress-Ki
 
karibu joseon ya tanzania na huduma za vyakula na vinywaji kama makgeoli, kimchi, soju, dumpling,bibimpap (mixed rice ),bulgogi,haemul pajeon vyote vinapatikana.
%EC%A1%B0%EB%A6%AC%EC%82%AC%EC%A7%84.png

http://kissasian.ch/Drama/Empress-Ki
Shikamoo baba Damushin hahahaha what a post hapa niko na stick naangalia buffering only 2 hrs remaining hahahah asante Sana na ubarikiwe kaka nimekuja Joseon naomba Kimchii
 
Back
Top Bottom