Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naweza kukwambia nzuri halafu ikaja kuwa mbaya,ngoja kwanza ianze ndiyo ntakuwa na jibu sahihi. Ila mie siku hizi nimekuwa na tabia mbaya yani naweza kuacha kuangalia drama nzima kisa mtu mmoja tu au kitu kimoja tu kikiwa kinaniboa kwenye hiyo drama.Hahaaa kweli leo umepatikana haswaa. Vp ni nzuri ili niongeze katika lisiti yangu pia.
Huyu mwana dada namkubali sana,yani wakorea wanavyopenda kuweka comedy kwenye drama zao basi huyu huwa anatendea haki hadi huwa natamani nimuone kwenye maisha ya kawaida huwa yukoje.muigizaji jun ji hyun siku ya jana amefanikiwa kujifungua (kuzaa) mtoto wake wa pili ambaye ni mwanamme.
mtoto wake wa kwanza ambaye pia ni mwanamme alifanikiwa kumzaa mwezi february 2016.
![]()
NB:
hili neno kuzaa nahisi ni kali sana kulitamka.
aigooooo mkewe damushin kazaa mtoto wa kike, hahahahaaha natania tu jamani usingizi umeniruka nimeamua niwe mlinzi wa JF
Chukahe...Mola Kamvusha Salama Uzazi Si Mchezomuigizaji jun ji hyun siku ya jana amefanikiwa kujifungua (kuzaa) mtoto wake wa pili ambaye ni mwanamme.
mtoto wake wa kwanza ambaye pia ni mwanamme alifanikiwa kumzaa mwezi february 2016.
![]()
NB:
hili neno kuzaa nahisi ni kali sana kulitamka.
aigooooo mkewe damushin kazaa mtoto wa kike, hahahahaaha natania tu jamani usingizi umeniruka nimeamua niwe mlinzi wa JF
Mrs Ju mong,baada ya takribani miaka 4 mwanadada anayejulikana kwa kina la han hye jin hatimaye amerudi tena kwenye ulimwengu wa uigizaji baada ya kukubali ofa ya kuwa muigizaji mkuu wa kike kwenye drama inayoitwa “Let’s Look at the Sunset Holding Hands" ambayo itaonyeshwa na shirika la MBC
![]()
Ni drama inayozungumzia simulizi nzuri yenye kuvutia inayowahusu wanandoa wawili ambao wanaamua kurudisha upendo wao waliokuwa nao baada ya kukabiliana na kifo (confronting the matter of death).
Nam Hyun Joo ni msichana aliyetokezea kumpenda mvulana tokea walipokuwa chuo kikuu, katikati ya maisha yao ya ndoa anaamua kuachana na mume wake na kuamua kwenda kutafuta upendo sehemu nyengine kwa ajili ya kutumia siku zake za mwisho wa uhai wake akiwa kwenye hali ya furaha na utukufu.
drama hii itakuwa ni ingizo jipya kwa mwezi Machi.
Nimehangaika kuitafuta kwa kuandika Jingbirok wakati naelekea kukata tamaaa nimeikuta.... KUMBE PALE JUU JINA KWA kIINGEREZA LIPO. HAHAHAAAA NASHUKURU KWA HIIhttps://ondramanice.io/drama/the-book-of-corrections-jingbirok--detail
- @mjr95,EMPTY dongsaeng mukipata nafasi baadae muitafute na hii inayoitwa jingbirok the memoir of imjin war.hadithi yake inafanana na tutakachokiona kwenye admiral yi soon shin drama. ila ndani ya drama hii anazungumziwa ryu seong ryeong na harakati zake za kuifanya joseon inakuwa na amani kwa kujiandaa kijeshi dhidi ya uvamizi wowote utakaotokezea lakini bahati mbaya baadhi ya mawaziri na mfalme seonjo walimpuuza. aigooo siwamalizii kuwahadithia
- jingbirok maana yake ni kitabu cha kujisahihisha na kimeandikwa na msomi ryu seung ryong ambaye kwenye comment yangu ya juu nimemuelezea kama ni mtu wa karibu wa yi soon shin ambaye kwenye vita ya imjin ndio alikuwa muhusika mkuu wa masuala ya kijeshi na pia aliwahi kuwa waziri mkuu.Aliandika kitabu hiki baada ya kuachana na harakati za siasa chini ya utawala wa mfalme seonjo.kitabu hiki kimekuwa ni moja kati ya chanzo muhimu kinachotumika kuelezea uhusiano wa mgogoro kati ya china,korea na japan.
- mwaka 1969 serikali ya korea ilikichaguwa kitabu hiki kama ni miongoni mwa hazina 132 bora za utawala wa korea (National Treasures of South Korea)
- Ryu Seong-ryong aliandika Jingbirok ili kuwa kama ni ukumbusho wa kuzuia uvamizi wa vita kama ya imjin (1592-1598) usitokee tena, kutafakari juu ya makosa walioyafanya ya kupuuzia taarifa za japan kujianda na uvamizi,jambo ambalo lilipelekea joseon kupoteza miji yake mitatu na kusababisha vifo vya maelfu ya wananchi wasio na hatia na wengineo kutumikishwa utumwani nchini japan na hata china.
- kim sang joong ndiye ameigiza uhusika wa ryu seong ryeong na kim tae woo ndiye ameigiza uhusika wa mfalme seonjo
![]()
- hadithi ya drama hii inaanza kabla ya vita ya imjin na vita ya noryang ambayo ilipelekea kifo cha admiral yi soon shin
- kama si juhudi kubwa za kidiplomasia na za kivita alizozichukua ryu seong ryeong basi tungelishuhudia joseon ikitawaliwa na japan na ming china, na pengine kwa wakati huu taifa la korea lisingelikuwepo.
- wakati vita ilipozodi mfalme seonjo aliamua kuikimbia nchi yake kwa kupitia mto yalu na kujificha nchini china (ming), cha kushangaza wafuasi wake wengi walikubaliana na maamuzi ya mfalme lakini ryu seung ryong alimshauri mfalme seonjo asifanye hivyo kwani kitendo hicho kingeliwafanya japan na ming (china) kuigawa joseon,licha ya kuwa ming walikuwa wakiisaidia joseon kwenye vita hiyo lakini kwenye mali hakuna udugu wala urafiki wa kudumu.
- ryu seung ryeong binafsi ndio alikuwa akiwaongoza yi soon shin na general kwon yun kwenye vita ya ardhini dhidi ya wajapan. ukiangalia admiral yi soon shin kuanzia episode ya 4 watatu hawa wanakuwa marafiki sana tokea udogoni mwao.
- baada ya vita kumaliza wapinzani wake wa kisiasa walimshinda kwenye vita chafu ya kiutawala na ndipo akavuliwa nyadhifa zote na kuamua kuondoka kwenye mji mkuu wa hanyang na kuelekea Hahoe Village, North Kyungsang Province, kwenye mji mkuu hakurudi tena ndipo akaandika kitabu hiki cha jingbirok.
- jina lake la utotoni aliitwa Igyeon, shuleni alikuwa akiitwa Seoae, kwenye drama ya admiral yi soon shin kwon yun anapenda kumuita yi seong ryeong jina la bookworm kwa sababu anapenda kusoma vitabu.
- Lee Kwang Ki (ameigiza nafasi ya Ha Ryun ndani ya Jeong Do Jeon drama) ameigiza nafasi ya konishi yukinaga na Kim Kyu Cheol ameigiza uhusika wa tayotomi hideyoshi, kwenye admiral yi soon shin ameigiza uhusika kama ni rafiki wa yi soon shin
![]()
- Lee Jung Yong ameigiza nafasi ya kato kiyomasa na cha kufurahisha kwenye admiral yi soon shin drama pia ameigiza nafasi ya kato kiyomasa.hahahahahaaa bonge la zari
![]()
- kwangu mimi namfananisha ryu seung ryong na jung do jeon kutokana na harakati zao za kisiasa na kuwa na uchungu na maisha ya wananchi kutokana na mateso wanayokutana nayo wakati wa vita, nadhani tofauti yao ni kwamba ryu seung ryong alipambana peke yake ila jung do jeon baadae alizunguukwa na watu kama yi seong gye, yi bangwon ambapo kwa pamoja walifanikiwa kuuangusha utawala a goryeo ulioanzishwa na mfalme wang guhn ambaye naye alianzisha taifa la goryeo baada ya kumpindua goong yae.
Tununue bonge la keki tukateKwaiyo Sasa Tuaze Kufanya kampeni.
aigoooooo nimeanza kukuogopa kama ninavyomuogopa swahiba wako wa karibu mjr95 yaani mimi kuweza kuandika maelezo kama ya kwako wewe itanipasa nifikirie siku nzima.najihisi nina upungufu mkubwa sana wa maneno, kiukweli najiona kila siku maneno yangu hayabadiliki kuanzia kuzungumza kwangu hadi kuandika.NB. Yeyote Uliye,Unayeyaptia Labda Yasiwe Kama Haya au Yawe Kama Haya Katika Ngazi Yoyote Ya Maisha Unayoyapitia, Usivunjike Moyo Mpaka Kukupelekea Ukshindwa Kupigania Maisha Yako. Ukisimama Wewe Leo Vizuri Na Kuwa Strong Utatengeneza Kizazi Kizuri Sana Kijacho Kupitia Wewe. Furahi Kila Unapopata Sababu Ya Kufurahi Na Lia Kila Unapopata Sababu Ya Kulia, Kujikwaa Kusiondolee Safari Yako,Nyanyuka Na Ukaze Mwendo.
duh hii post yako imenifanya nikumbuke ya kwamba nina kiporo changu cha moonlight drawn by clouds drama, kuanzia episode ya 10 hadi 18.Na Mm leo acha nimtaje binti anae nivutia katika kiwanda cha Korea Drama. Baadhi yetu hapa mmekuwa mkiwataja wale wanao wavutia kwa namna moja ama nyingine. Nami leo nahitaji kulitoa la moyoni kabisa ili mfamu kuwa kuna binti navutiwa nae kwa jinsi alivyo.
KIM YOO JUNG ndie mwana Dada anae nivutia kunako kiwanda cha kutengeneza Drama bora kabisa dunia, namaanisha Korea Drama. Binti huyu kwa mara ya kwanza nilimfaham katika Drama ya Dong Yi kipindi hicho alikuwa binti mdogo sana.
omo kkamjagg, kwa mujibu wa list yako kama ni idadi ya madeni basi nadaiwa 13.Zile Drama Ndo Hizi kwa Ninazozikumbuka.
Jumong
The Land of Wind
Emperor of The Sea
Gu Family Book
Empress Ki
Kings 2 Hearts
Night Watch Man
Scholar who Walks The Night
DOTS
Blood
Doctors
Faith
Personal Taste
The Heirs
Healer
K2
City Hunter
The Legends of the Blue Sea
Criminals Mind
Six Fly Dragon
Suspicious Partner
Remember
The King In Love
Moorim School
Cheese In The Trap
Goblin
Uncontrollably fond
My Love from Another Star
It's OK,This is Love
Warrior Baek Dong So
Rebel.Thief who stole the People
Ruler Master of the Mask
Moon Lovers Scarlet Heart Ryeo
Queen 4 7 Days
While You Were Sleeping
W
My Sassy Girl
Entertainment
Reunited World
You're All Surrounded
SCHOOL 2017
Cinderella & 4 Knights
Money flower - Ongoing
Black
Hwayugi - Ongoing
My Girlfriend Is Gumio
I'm Not A robot - Ongoing
Black Knight - Ongoing
Hahaaa Mkuu leo ndio unaliona hilo bandiko? Pongezi kwako kwa kila ufanyalo katika khaki.duh hii post yako imenifanya nikumbuke ya kwamba nina kiporo changu cha moonlight drawn by clouds drama, kuanzia episode ya 10 hadi 18.
aigoooooo ngoja nianze kutafuta kuni ili nikipashe moto
![]()
Hahaaa Mkuu leo ndio unaliona hilo bandiko? Pongezi kwako kwa kila ufanyalo katika khaki.
Vp drama yetu uko namba ngapi?
* Hahaaa sishangai ndugu ata mm hali hiyo hunitokea, unakuta tu sina cha kuandika.
- admiral yi soon shin nipo episode ya 20.
- hili andiko nimeliona zamani ila baadhi ya wakati huishiwa maneno ya kujibu. hahahahahahhaha usishangae