12 Dramas To Look Forward To In Spring And Summer 2018
Suits
imeanza jumatano ya wiki hii kupitia shirika la habari la taifa la korea (kbs 2tv). Suits ni remake ya series ya kimarekani inayozungumzia maisha ya Choi Kang Seok (Jang Dong Gun) ambaye ni mwanasheria mwenye uzoefu mkubwa sana pamoja na Go Yeon Woo (Park Hyung Sik) ambaye ameajiriwa na choi kang seok japokuwa hana leseni wala elimu ya kufanya kazi kwenye vitengo vya sheria.
Starring: Jang Dong Gun,
Park Hyung Sik, Chae Jung An, Go Sung Hee.
Mistress
itaanza kuonyeshwa kupitia OCN siku ya leo (28/04/2018), mistress ni remake ya show iliokuwa ikionyeshwa na kituo cha habari cha uingereza BBC. inazungumzia maisha ya wanawake wanne ambao wanajikuta kila mmoja akihusika na matukio ya mauaji.
Starring: Han Ga In, Shin Hyun Bin, Choi Hee Seo, Goo Jae Yee.
Wok of Love
inazungumzia maisha ya mpishi mashuhuri anayefanya kazi zake kwenye mgahawa unaopika vyakula vya asili ya china. Doo Chil Sung ni kijana anayejighulisha na biashara ya ukopeshaji wa fedha.
Starring: 2PM’s
Junho,
Jang Hyuk,
Jung Ryeo Won
Rich Man, Poor Woman
ni remake ya tamthilia ya kijapan inayozungumzia maisha ya kijana ambaye ni genius programmer na pia ni CEO wa kampuni anayesumbuliwa na tatizo la kutokutambua sura,Kim Bo Ra ni msichana mwenye uwezo mkubwa sana wa kuhifadhi taarifa kwenye ubongo anajikuta anatafuta ajira, unajua kitatokezea kitu gani uanpokwenda kutafuta kazi kwa mtu ambaye ukiondoka tu ameshakusahau?
itaanza kuonyeshwa kuanzia Mei 9.
Starring: EXO’s Suho, Ha Yeon Soo, Oh Chang Suk, Kim Ye Won
Lawless Lawyer
Bong Sang Pil ni mwanasheria maarufu sana na pia aliwahi kuwa member katika magroup ya kihuni,anaamua kutumia ngumi kwa ajili ya kupambana na wale wanaogopwa kuchukuliwa hatua na vyombo vya sheria.itaanza kuonyeshwa mei 12
Starring: Lee Joon Gi, Seo Ye Ji, Lee Hye Young, Choi Min Soo
Partners for Justice
gwenchana gwenchana
ni hadithi inayozungumzia timu maalum ya uchunguzi wa matukio ambapo ndani yake muna daktari anayechunguza miili ya marehemu na mwanasheria asiyekuwa na uzoefu katika kazi.
episode ya kwanza ni mei 14.
Starring: Jung Jae Young, Jung Yoo Mi, Lee Yi Kyung
Miss Hammurabi
inazunguzmia maisha ya majaji watatu wenye tabia zinazotofautiana
episode ya kwanza itaonyeshwa mei 21
Starring: Go Ara, INFINITE’s L, Sung Dong Il, Ryu Deok Hwan, Lee Elijah
About Time
hadithi ya wanadamu wawili wenye tabia za ajabu, mmoja ana uwezo wa kusimamisha wakati na mmoja ana uwezo wa kutambua mwanadamu ataishi muda gani.
episode ya 1 itaonyeshwa mei 21
Mr. Sunshine
kijana mwenye asili ya korea aliyekuwa akiishi marekani anaamua kurudi nyumbani kwao mwaka 1871. episode ya kwanza itaonyeshwa mwezi july
Starring: Lee Byung Hun, Kim Tae Ri, Yoo Yeon Seok, Byun Yo Han, Kim Min Jung
What’s Wrong with Secretary Kim?
hadithi inayowahusu muajiri na muajiriwa ambapo muajiri ni mtu asiyejali kabisa masuala ya kazi hatimaye karani wake anaamua kuacha kazi ili atafute sehemu itakayompa furaha na pia apate mwenza wa kufunga naye ndoa.
mwezi june itaanza kuonyeshwa.
Starring: Park Seo Joon, Park Min Young, Lee Tae Hwan, 2PM’s Chansung
Sketch
hadithi inayozungumzia maisha ya askari aliyempoteza mke wake na hatimaye anaamua kutafuta ukweli juu ya chanzo cha kifo, pia anajikuta akifanya kazi na askari wa kike mwenye uwezo wa kufahamu matukio yatakayotokezea kwa siku tatu zinazofuata.
aigoooo huyu anafaa awe mchumba wangu kwani atanisaidia kujua kama ndani ya siku tatu nitapata pesa au sitapata pesa.itaanzakuonyeshwa mwezi mei
Starring: Rain, Lee Dong Gun, Lee Sun Bin, Jung Jin Young
Life
ni hadithi inayozungumzi migogoro ya kuwania madaraka yanayotokezea kwenye hospitali kubwa nchini korea. itaanza kuonyeshwa july
Starring: Lee Dong Wook, Cho Seung Woo, Won Jin Ah, Moon So Ri