- ndiye muanzilishi wa taifa la goryeo mnamo mwaka 918 hadi 943 alipofariki na alipewa heshima ya Taejo.
- aliingia madarakani baada ya kumpindua mfalme Gung ye wa taifa la Taebong ndipo akalibadilisha jina taifa hilo na kuliita Goryeo wakati huo alikuwa ni general.
- chimbuko la ukoo wao ni wakimbizi kutoka Goguryeo ambao walikimbilia nchi ya Shilla na ndipo wakaanza kujishughulisha na biashara za baharini zilizowapa utajiri mkubwa sana wa mali.
- kabla ya kuwa mfalme na hata alipokuwa mfalme alifunga ndoa nyingi sana za kisiasa, koo nyingi sana ziliamua kuanzisha mahusiano na ukoo wa WANG kwa dhumuni la kuanzisha umoja na mshikamano na waliamini njia pekee ya kutimiza ahadi walizokubaliana kati ya pande mbili hizo ni kuanzisha undugu wa damu kwa kufunga ndoa.Inakadiriwa Wang guhn alioa wanawake 30 kutoka makabila tofauti ndio maana alikuwa na watoto wengi.Ukiangalia drama ya scarlet heart ryeo ndio utapata kugundua baadhi ya watoto aliokuwa nao.
- Wang gun ndiye aliyeziunganisha tawala tatu za baadae za korea (later goguryeo, later baekje na shilla)
- pia baada ya utawala wa Balhae kuwa legelege baada ya kushindwa na Khitan wang guhn aliamua kuwapokea wabalhae wote kwenye utawala wake wakiongozwa na crown prince na kuwapa ardhi na maeneo ya kuishi nchini goryeo.Ukiangalia drama ya shine or go crazy utagundua ya kwamba Shin Yool (oh yeon soo) alikuwa ni last princess wa balhae apmoja na kaka yake ambaye alikuwa ni mlinzi wa yuhwa ambaye ni mke wa wang soo, pia shin yool alijikuta akiwa kwenye mahusiano na wang soo ambaye ni mtoto wa nne wa mfalme wang guhn.
ukiziangalia drama zote mbili utakutana na wahusika wakuu
wang guhn = muanzilishi wa goryeo
wang moo = alikuwa mtoto wake wa kwanza na ndiye mfalme wa pili wa goryeo, hapa ndipo zilianza power struggle kati ya watoto zikiongozwa na wang soo na jeong jong.Wang moo alikaa madarakani kwa miaka miwili akafariki.
jeong jong : kwenye shine or go crazy uhusika wake ulioonyeshwa kama mfalme dhaifu ila kwenye scarlet heart ryeo alikuwa ndiye mfalme mkorofi, pia alikuwa mtoto wa tatu wa Taejo .
wang soo :mfalme wa nne wa goyeo, alikuwa na kaka watatu, ndugu wa kiume 12 na dada 7 kupitia mama tofauti. Ili kuepusha kuongezeka kwa nguvu kwa baadhi ya makabila aliamua kuwa tofauti na baba yake ambaye alioa wanawake wa makabila tofauti.Wang soo aliamua kufunga ndoa na mdogo wake pamoja na mtoto wa kaka yake.Ukiangalia drama zote mbili utakutana na haya matukio.
hwang bo yeo won : alikuwa ni mke wake wa kwanza prince wang soo kutoka uzao wa malikia kutoka ukoo wa hwang bo.
Choi Ji-Mong : alikuwa ni mtaalamu sana wa masuala ya nyota na utabiri, ukiangalia drama ya
emperor wang gun utaona jinsi gani alivyokutana na wang gun na kupewa nafasi ya kufanya kazi ikulu.
hivi sheria za hizi dini pendwa zinaruhusu ndugu walioungana kwa damu ya mzee mmoja kufunga ndoa?