binafsi niliishia episode ya 2.
inaonekana time travel ndio zinakuzingua unapoiangalia au stori yake hujaipenda?
voice season 2 ipo vizuri kama ni mpenzi wa criminal drama na wiki hii inaendelea episode ya 5, 6.
hivi huku kwetu tuna shirika linalofanya uchunguzi wa matukio ya kihalifu kisayansi?
hivi huku kwetu idara yetu ya ulinzi inaweza kutatua matatizo ya kihalifu kwa kutumia special customer service za njia ya mawasiliano?
nakusudia kusema ya kwamba nchi yetu tuna uwezo wa kumtrack muhalifu taarifa zake zote zinazomuhusu, kwa mfano kufahamu DNA za muhalifu, kufahamu taarifa za kifedha za muhalifu na kuweza kuzizuia, kufahamu taarifa za usafiri za muhalifu, anapoishi n.k
pia jaribu kuiangalia drama inayoitwa
life on mars.
nayo pia inahusu masuala ya utatuaji wa matatizo ya kihalifu, ni remake ya program ya kituo cha BBC.
- jamaa anajikuta anarudi nyuma mwaka 1988 ambapo ni sawa na miaka 30 iliopita baada ya kupigwa risasi
- jinsi hiki kikundi cha polisi wanavyotatua matatizo wewe muangaliaji wa hii drama utapenda ukitaka usitake, hamuna cctv camera, hamuna computer, hamuna database kwa ajili ya kuhifadhi taarifa za watu mbali mbali,hamuna shirika lolote linalihusiana na kufanya chunguzi za kisayansi, ni mwendo wa kutumia akili mwanzo mwisho.
- location, music, uvaaji wao,usafiri wao na vyenginevyo vinakushajihisha uamini ya kwamba hii drama matukio yake ni ya miaka 30 iliopita.
- wakati huku kwetu unaangalia filamu yenye kuzungumzia matukio ya kizamani yaliotokea kipindi cha utawala wa machifu wakuu cha ajabu pembeni yake unakuta nyumba imejengwa kwa matofali na wanatumia vyombo vya plastic. Tuna safari ndefu sana.