- katikati ya wiki simba walikunyima furaha ila manchester united walikupa furaha
- leo hii nasikia simba wamekupa furaha ila manchester united wamekunyima furaha
kama ni mtihani wa darasani alama zako ni 50%.
yap nimejikuta napata mapumziko ya kuangalia korean drama bila ya kutarajia, wiki inamalizika nimeangalia episode 6 tena kwa siku moja jambo ambalo ni nadra kutokezea.
natamani hii hali ninayokumbana nayo wiki hii iendelee kiupande wangu japo kwa wiki moja nyegine.
dah huwezi amini nimeamua kufukua makaburi muda huu humu ndani ila bahati nzuri marehemu wote wamebaki vile vile na harufu yenye kuvutia, inaonekana safari yao ni mapumziko ya peponi kama wafiwa wa mv nyerere.
july 5 / 2017 ndio ilikuwa ni mara ya kwanza kusoma comment zako, daebak. Ni mwaka mmoja na miezi 2 tokea nikufahamu japo kwa maandishi ila umekuwa zaidi ya rafiki ambaye tunaonana kila siku.
unazikumbuka hizi comment zako?
- Yaani naomba uangalie iyo Queen of Seven days ni Nomaaa yaani utaichoka inasisimua balaa,Na ina Ost nzuri sana kam ni mpenzi wa zile nyimbo
- Hivi na lee seung gi naye bado ajatoka ???
- Uyo alocheza kwenye bridal Mask si ndo anacheza now kwenye My sassy girl....
- Naombeni Muangalie FIGHT FOR MY WAY Hii drama kama kurelax na kuenjoy yaani apa ndo mahala pake, Ina vichekesho sana na ni nzuri pia, Forever Korean Drama
kupitia comment ya mwanzo ulinifanya na mimi niitafute hii
drama ya queen for seven days na sikujutia maamuzi yangu.
naomba uondoe khofu kwenye nafsi yako,namshukuru Mungu ni mzima wa afya mpaka muda huu
ahsante sana kwa kuwa zaidi ya rafiki dada yangu.
utabaki kuwa ni malikia wa kila siku tofauti na yule malikia wa siku 7
jeongmal gomabseubnida