Da'Vinci
JF-Expert Member
- Dec 1, 2016
- 35,812
- 107,628
Nakuelewa sana mkuu.. Hongera[emoji120]jibu langu kwa ufupi baada ya muda mrefu kukaa kimya kana kwamba sijaiona comment yako tokea tarehe 22 December.
mkuu hakuna anayependelea kufuatilia sanaa za nchi nyengine bali nchi zetu ndio zinatulazimisha kufuatilia sanaa za nje tena kwa bakora kama ng'ombe.
Serikali nyingi za kiafrika zinatamani mafanikio lakini hazipendi kufuata njia zitakazowawezesha kupata mafanikio, hao wote waliofanikiwa msingi mkuu wa mafanikio ulianzishwa na serikali ndipo wakafuata wananchi na matajiri pamoja na wasanii lakini leo hii nchi zetu serikali haziithamini sanaa ndio maana hatusogei mbele.
Miaka mingi iliopita sote ni mashahidi nakumbuka binafsi nilikuwa naangalia movies za wahindi, amerika na wachina peke yao, ina maana sikuwa na habari na wakorea sasa jiulize wakorea wamefikaje kuwa ni nchi inayotambulikana kwenye sanaaa mpaka na mimi ninayeishi dunia ya mwisho nikawafahamu?
unafikiri ni samsung na makampuni mengineo ndiyo yameifanya sekta ya sanaa isonge mbele nchini kwao bila ya nguvu ya serikali?
Serikali za kiafrika ziache kujificha kwenye kivuli cha mchicha huku wakitegemea miale ya jua haitagonga ngozi zao na kuziathiri.
chengine kuiga mambo mazuri ya kigeni si vibaya ila ubaya inakuwa pale unapoiga mambo yanayokwenda kinyume na utamaduni wetu ambayo yataleta athari kama unavyozungumza muheshimiwa, Hivyo basi unapaswa ufahamu si kila jambo la kigeni ni haramu ndio maana hata viongozi wetu wanatumia magari kwa ajili ya safari zao na si punda kama ulivyo utamaduni wetu.
halafu mkuu umesahau kama watanzania pia ni waumini wa ubepari, sina uelewa mkubwa sana ila naamini unapofuata misingi ya ubepari pia unapaswa ufuate misingi ya demokrasia, kwa kutumia GPA yangu ya 50 demokrasia haipo kwenye siasa tu bali hata kwenye maswala mengine ya kila siku ikiwemo JF, hivyo basi naomba utuvumilie kama wewe tunavyokuvumilia pindi unapofuatilia stori za kuvunja korosho kwa kutumia jeshi la wananchi.
Economic impact analysis : examines the effect of an event on the economy in a specified area, ranging from a single neighborhood to the entire globe. It usually measures changes in business revenue, business profits, personal wages, and/or jobs.
injinia soma hizi link ukipata muda upate kufahamu wenzetu walitokea wapi na wanaelekea wapi kupitia sanaa
"Bae Yong Joon, through the drama Winter Sonata drama 2002, created an economic value of about 3 trillion won.
nchi ambayo viongozi wake wanapitisha sheria halafu siku chache zijazo wanaifuta ina faida gani kufuatilia habari zake kila siku?
- BTS’s 10-Year Economic Impact To Korea Expected To Reach Over 56 Trillion Won
- Korean Wave (Hallyu) - Rise of Korea's Cultural Economy & Pop Culture
- Drama Series Gives Boost to Korean Economy
kuliko kujipa stress acha tuwafuatilie wachina tambi na drama zao ambao wameiona sanaa kama njia moja wapo ya kujikwamua na umasikini.
kumbuka ya kwamba sanaa ni rahisi sana kuliko siasa ndio maana leo hii BTS wanapata kiki mpaka nchini marekani na wanachoimba hata wamarekani hawakifahamu.
Ndio maana leo hii diamond platnumz ni maarufu kuliko great thinker zitto kabwe duniani.
bado hamujanishawishi kurudi nyumbani kwa sanaa hii inayoelea kama maiti.
Sent from my GT-I9300 using Tapatalk