yes, muda huu najiona kama natoka kifungoni baada ya takribani wiki mbili zilizojaa harakati za kuyafanya maisha yangu yawe kwenye mstari sahihi ila namshukuru mungu nimemaliza kwa amani kimwili na kiroho.
bila ya kusahau nilijiwekea mwaka huu nipunguze ulevi angalau kwa asilimia 50 ili nirudishe mind yangu kama ilivyokuwa mwanzoni nilipokuwa sijawafahamu hawa wazee wa lipstick kike na kiume.
mwaka 2019 nimeuanza kwa kufuatilia drama zifuatazo:
- romance is a bonus book drama (jumamosi na jumapili) : love story kati ya mwanaume wa seoul na single mother
- haechi drama (jumatatu na jumanne) : historical drama inayoangazia vita ngumu ya siasa kati ya pande mbili zinazokinzana (kaskazini na kusini), kabla na baada ya kifo cha mfalme sukjong joseon ilijikuta ikizidi kudumbukia kwenye political power struggle ambapo wote kwa pamoja walitaka kuwaweka madarakani watoto wanaowataka wao, alikuwepo prince anayeitwa Yeoning-gun ambaye hakukuwepo upande wowote unaomuunga mkono kwa sababu mama yake alikuwa ni kijakazi (dong yi), ilikuwaje mpaka jamaa akawa mfalme hapo baadae na kupewa jina la mfalme yeongjo, huyu yeongjo ndiye babu yake yi san ambapo historia ilimuandika kama ni mwanadamu aliyemuua mwanawe aliyeitwa crown prince sado. Yeongjo alikuwa ni miongoni mwa watawala waliojijengea heshima kubwa sana.
- item drama (jumatatu na jumanne) : super natural power ni nzuri sana kwa anayetaka kuifuatilia
- touch your heart drama (jumatano na alhamisi) : love story kati ya mwanasheria na muigizaji wa kike aliyepoteza nguvu kwenye soko la sanaa baada ya skendo.
- the fiery priest drama ( ijumaa na jumamosi): kwa waumini wa dini ya kikristo hivi priest ndio nani?, humu ndani yumo kim nam gil (bidam) amekuwa muhubiri kichaa si wa akili bali ni wa kushindwa kudhibiti hasira zake.
kama nipo sahihi ni takribani siku 70 zimeshapita tokea tuuanze mwaka huu na hizo ndio drama ninazozifuatilia kila wiki, daebak daebak kama nitaendelea na style hii basi malengo yangu nitaweza kuyafikia.
napenda going on drama kwa sababu hazinipotezei muda mkubwa sana ukilinganisha na zile ambazo zipo completed, kwa ujinga wangu mimi ninapotizama drama ambayo ipo completed kama ipo vizuri naweza kuangalia episode 10 kwa siku ndio maana najaribu kuzipuuzia compeleted drama ili nibane muda wangu.
24 hrs * 7 days = 168 hrs / 10 episode per week = 16.8
nafikiria kuingiza drama nyengine moja iliokuwa compeleted kwa mara ya kwanza tokea uanze mwaka 2019
sielewi kwa nini
wendy ana sauti nzuri kila ost anayoimba
sielewi kwa nini
yoo in na ana sauti ya kitoto kila drama yake ninayoiangalia wakati umri wake ni miaka takribani 36.