Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Screenshot_2019-05-15-23-15-48.png

😂😂 Sasa huyu mzee hapo anafanya Tafakuri au vipi, dooh! Mbwembwe hizi!!
 
Hivi kuna mtu alishawahi kufikiria hii. Laiti Kama CCCM ingekuwa na Fitina na Figisu Kama za wakorea ingekuwaje Tanzania hii. Maana washikaji kukupa kesi ya treason tena ushahidi wa kutosha Ni rahisi sana yaani.
 
Hivi kuna mtu alishawahi kufikiria hii. Laiti Kama CCCM ingekuwa na Fitina na Figisu Kama za wakorea ingekuwaje Tanzania hii. Maana washikaji kukupa kesi ya treason tena ushahidi wa kutosha Ni rahisi sana yaani.
Mbona hata Tanganyika figisu zinafanyika/zimefanyika sana mkongwe..!
 
  1. doctor prisoner drama : imemaliza wiki iliopita ipo vizuri sana, ukiondoa the fiery priest kwa mwaka huu naipa nafasi ya pili kiubora, kuna bwege mmoja anaitwa doctor na yi je ukiwa mpinzani wake jiandikie maumivu, wakati wewe unapanga karata X basi yeye ameshapanga W, X,Y,Z
  2. different dreams : spy drama inaturudisha nyuma nyakati ambazo korea ipo chini ya ukoloni wa Japani
  3. the banker : ina maana hujavutiwa na professor assad humo ndani na lafudhi yake ya kishamba?. halafu imeshamaliza tokea wiki iliopita
  4. her private life : nilifika episode ya 2 nikaiacha kuifuatilia lakini ukitembelea kwenye mitandao imekuwa gumzo kwa sababu ya love chemistry kati ya park min young na mashoto kim jae wook.
  5. the nokdu flower: historical drama inayojaribu kuzungumzia uasi ulioanzishwa na walala hoi dhidi ya serikali ya joseon (donghak peasant revolution). Ndugu wawili waliozaliwa na mama tofauti wanaotofautiana social status wanajikuta wanakuwa tofauti kimtazamo juu ya hayo mapinduzi.
the secret life of my secretary + voice season 3 + Abyss + save me season 2 + my absolute boyfriend drama = hizi zote sizifuatilii hivyo basi siwezi kutoa mawazo yangu mfu na zimeanza mwezi May.
Hizi zote itabidi nizitengee muda,,,,,asante kwa kunipa mwanga.
 
hongera mkuu kwa kutimiza mwaka mmoja
hongera sana mkuu kwa kuendeleza gurudumu la walevi wa korean drama.

unaonaje ukarithi mikoba yenye mizimu ilioachwa na member anayeitwa kazz0?

ngoja niwasilishe rasmi barua yangu ya kung'atuka, si unajua nimeshika kijiti cha bwana kazz0 kwa takribani miaka mitatu na nusu, na sisi humu ndani ni waumini wa domolakrasia
<>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Mimi Daemusin bin makinikiyya bin noah bin koroshow bin balimi serengeti bin vipigo vya shangazi zenu, bila ya kutishwa au kuvamiwa na wazee wa teleza kutoka kigomasha, nimeamua rasmi kuachia ngazi nafasi yangu ya mkuu wa idara ya ubuyu na bagia unaotoka korea ya kusini.

sijajua baada ya kustaafu nafasi hiyo nitajishughulisha na jambo lipi litakaloendelea kuniongezea furaha mpaka kufa kwangu, lakini kiukweli nimefikiria kazi ya kufuga panya na mende, nimesikia wana soko kubwa sana maeneo ya kinondoni anapotokea Khantwe kwa sababu wanatibu nguvu za kiume.
🏇 🏇 🙁
Naomba mkuu urithi madaraka yangu bila ya pingamizi yoyote.

nitaachia rasmi madaraka yangu ifikapo tarehe 01/06/2019​
😂😂 Usije ukawa kama Lee bangwon abaye aliachia madaraka wakati jeshi bado analiongoza.
 
EMPEROR WANG GUHN DRAMA
imenichukua miaka takribani mitatu kuiangalia hii drama and finally usiku wa jana nimeimaliza, drama kama hizi zinaangaliwa zaidi na wale binadamu wabishi, watemi na vichwa maji kama damushin ambao kwa kiasi kikubwa muda wao mkubwa huutumia kwa ajili ya kuangalia televisheni kuliko kufanya kazi mpaka anayaletea athari macho yake aliyopewa na muweza wa yote ulimwenguni.

jumla ya episode 200 na kila episode inachukua wastani wa dakika 48- 53, kilichonivutia ni kwamba 85% ya matukio yalioigizwa humu ndani yamerikodiwa kwenye vitabu vya historia na kwa kuwa washindi walikuwa ni goryeo basi kivyovyote maandishi ya kihistoria yaliorekodiwa yatakuwa upande wa kuisifu Goryeo.
Neno goryeo(koryeo) ndio msingi wa neno korea.
  1. wang gun amezaliwa na kufariki (31 January 877 – 4 July 943)
  2. ni mzaliwa wa shilla lakini chimbuko la ukoo wao ni watu kutoka goguryeo ya zamani, ukoo wao ulikuwa na heshima kubwa sana na utajiri uliotokana zaidi na biashara walizokuwa wakizifanya kwa njia ya bahari.
  3. kwa mujibu wa drama na maandishi ya kihistoria aliwahi kuwepo muhadhiri wa imani ya buddhism aliyeitwa dosun ambaye aliwahi kutabiri ya kwamba wang guhn atakuja kuwa mtawala mwenye nguvu kwenye hizi nchi tatu za baadae (laer goryeo+ later baekje +shilla)
  4. wang guhn alitawala goryeo kwa miaka 25,ndipo madaraka yake yakarithiwa na mtoto wake wa kwanza ambaye ni wang mu lakini alifariki baada ya miaka miwili ya kuwa madarakani
  5. wang guhn alioa wanawake takribani 30, kwa kiasi kikubwa alifunga ndoa zaidi za kisiasa kwa dhumuni la kuunganisha damu dhidi ya koo tofauti ambazo ziliamua kujisalimisha kwa wang guhn.
  6. upande wa pili alikuwepo jamaa anayeitwa gong ye ambaye alizaliwa na mfalme wa shilla lakini kupitia kwa mwanamama amabye ni concubine, huyu jamaa alikutana na mitihani mingi sana uddogoni mwake alipokuwa shilla ikiwemo kupoteza jicho lake na alishuhudia kifo cha mama yake jambo lililopelekea aikimbie nchi yake na kuwa MONK.
  7. Gong yae baadae alipata nguvu kubwa sana na kufanikiwa kuanzisha taifa lake ni kulipa jina la Taebong, ukoo wa wang guhn waliamua kujisalimisha kwa gong yae na hatimaye akapewa cheo cha general, mfalme gong yae alivutiwa sana na wang guhn kiasi ambacho alifikia hatua ya kumtangaza wang guhn kama ni mdogo wake.
  8. miaka ilizidi kusogea huyu jamaa akawa na chembe chembe za kidikteta, miongoni mwa vitendo vyake vya ovyo ni kuisambaratisha familia yake mbele ya hadhara, baadae gong yae akamua kulibadilisha jina la taifa lake kutoka Taebong kuelekea Majin.
  9. mwaka 918 takribani wanajeshi wanne wenye nguvu nchini Taebong waliamua kumfuata wang guhn nyumbani kwake kwa dhumuni la kumshauri ashiriki kwenye kampeni yao ya kutaka kumpindua mfalme gong yae ambaye alikwisha vuka mipaka kwa matendo yake maovu, wang guhn alikataa mpango huo lakini baadae baada ya kubembelezwa na mke wake hatimaye akaongoza kampeni ya kumuondoa madarakani mfalme gong yae kwa njia ya mapinduzi.
  10. mfalme gong yae aliuawa pamoja na wafuasi wake na hatimaye wang guhn akabeba ufalme na kutangaza rasmi utawala wa goryeo(goguryeo mpya).
  11. alikuwepo general aliyeitwa kyu hwon kutoka shilla, huyu general nayeye alifanya mapinduzi kwa kuivamia shilla maeneo ya mujinju na hatimaye baadae akaanzisha taifa lake ambalo ni HUBAEKJE ( baekje mpya)
  12. wenye lugha yao wanadai ya kwamba kama utashindwa kuiongoza familia yako haijalishi wewe ni shujaa unayeogopeka basi pia utashindwa kuiongoza tawala yako kwa amani na ndicho kilichomkuta huyu mfalme.
  13. alitokezea kumpenda sana sana mtoto wake wa mwisho huku akimchukia mnoo mtoto wake wa mwanzoni kupitia kwa mke wa mwanzoni, jamaa aliipa mafanikio makubwa sana hubaekje ikiwemo kampeni yake ya kuivamia shilla na kumuua mfalme wa shilla huku akimweka mfalme mwengine aliyekuwa akiendana na maamuzi yake lakini vita ya familia ilipelekea anguko la nchi yake.
  14. mtoto wake wa kwanza aliitwa shin guhm ambaye aliamua kufanya mapinduzi kwa kumuondoa madarakani baba yake na pia aliamua kumuua ndugu yake wa kambo aliyeitwa keum gang na hatimaye akawa mfalme wa pili baekje.
  15. kyu hwon hatimaye akaamua kukimbilia goryeo ili apate hifadhi kutoka kwa wang guhn ambaye ni adui wake wa muda mfrefu ambaye wameshakutana mara kwa mara vitani, mzee aliona ni bora ajisalimishe kwa wang guhn kuliko kumuunga mtoto wake wa kumzaa awe mfalme.
  16. vita ya mwisho hatimaye hubaekje wakajisalimisha kwa goryeo na baadae shilla pia wakajisalimisha kwa goryeo, bila ya kusahau taifa la balhae ambalo lilianzishwa na general daejoyong kutoka goguryeo nao pia walijisalimisha kwa goryeo.
  17. hawa balhae utawala wao uliangushwa na wahuni wanaoitwa KHITAN, hatimaye goryeo wakafanikiwa kuziunganisha kingdom tatu na wang guhn kupewa heshima ya emperor.
  18. shilla waliziunganisha tawala tatu kwa kutumia msaada zaidi kutoka nchi za kigeni hususani Tang.
  19. wang guhn hakutegemea nguvu za nchi za kigeni kuziunganisha three kingdom za baadae.
maisha ya emperor wang guhn na baadhi ya watoto wake pia yameelezewa kupitia drama zifuatazo
scarlet heart ryeo
shin or go crazy


huyu wang guhn kwa vipindi tofauti alizungukwa na wanadamu wenye akili zaidi kuliko binadamu wengineo kama mimi.

choi ung= aliingia madarakani akiwa na miaka 14 nyakati za utawala wa gong yae, alikuwa ni zaidi ya genius na alifariki akiwa na miaka 35
choi jimong = huyu jamaa alibobea mnoo kwenye elimu ya nyota
View attachment 1098969
Hii drama inautofauti wowote ule na ile ya Dae Jo Young??? Ama tofauti ni majina tu?
 
Jodong Jeong( Sambong) nipo ep 10, even SIX FLYING DRAGON haiufikii huo moto wa Sambong hata kwa chembe, kifupi hawa jamaa walimaliza kila kitu hivyo sidhani kama Great Seer inaufikia.
Nimefanikiwa kuangalia zote Six Flying Dragon na Jeong Do Jeon naweza sema Sambong wa kwenye Six Flying amefanya Vizuri zaidi kuliko wa Jeong Do Jeon. Sambong kwenye Jeong hakuwa na ushawishi mkubwa au strategist Kama Sambong kwenye six flying.
 
Nimefanikiwa kuangalia zote Six Flying Dragon na Jeong Do Jeon naweza sema Sambong wa kwenye Six Flying amefanya Vizuri zaidi kuliko wa Jeong Do Jeon. Sambong kwenye Jeong hakuwa na ushawishi mkubwa au strategist Kama Sambong kwenye six flying.
Hapana mzee Sambong wa Jeong do jeon ni great thinker, pia amechorwa katika uhalisia na changamoto alizokutana nazo katika harakati zake za kuanzisha Taifa jipya. Kule kwenye Six Flying Dragon Harakati zake hazikuwa na milima mikubwa.
 
Upi moto wa kuotea mbali kati ya hizo mbili? Mi nimetizama King Gwangaetto pekee nataka kushuka na Dae Jo Yeong baada ya kuisaka kwa mda mrefu sana bila mafanikio.
Ila Dae Jo young ndio ya kwanza kutoka 2006-2007, Gwanggaetto imetoka 2011-2012.
 
Back
Top Bottom