Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Hapana mkuu! Na sijajua ni kwanini unasema hivyo!

Mimi na mkuu Daemusin ni watu wawili tofauti. Ama niseme ni ID's mbili zenye watu wawili tofauti.

Nilikuwaga 'Mhudhuriaji' mzuri wa huu uzi kipindi fulani ila ghafla nikaanza kuwa 'Mtoro'.

Huu 'Utoro' kwakweli kama ndiyo ingekuwa 'Bunge' fulani hivi katika nchi fulani kule kusini mwa jangwa la Sahara, ningekuwa nimeshafukuzwa zamani.

Kwa sasa nadhani nitajitahidi kuwepo humu na kufuatilia maoni na taarifa mbalimbali za wadau katika Tasnia ya Burudani hususan Korean Dramas.
Duh haya bwana sijui kwa nini moyo wangu bado hautaki kuamini
 
Mara Ya Mwisho Kuangalia Kdrama Ilikuwa 2015, Naomba Kuuliza Hivi Wakorea Wamefanikiwa Kutengeneza Historical KDrama Kali Kuliko JUMONG?? Sijafanikiwa kuiona SIX FLYING DRAGONS ila sidhani kama ni kali kuliko JUMONG
Six flying dragon ni kali balaa kila nikitafuta korean drama nkajua itafanana na Jumong au six flying dragon siiendelezi.
 
Hivi hii IRIS huwa inaonyeshwa siku gani hadi siku gani? Maana hadi sahv nimeganda tu hawajaonyesha
ITV mnatakiwa muheshimu matakwa ya Wateja wenu.Sasa hivi mlitakiwa muonyeshe IRIS lakini sijui mnarusha kipindi gani.Hebu acheni uswahili basi!
 
Uandishi mkuu unashabihiana sana
Uliposema kuwa kuna mshabihiano wa kiuandishi nikasema 'isiwe tabu' ngoja niurudishe huu uzi nyuma ili kupata kuyashuhudia mwenyewe hayo unayoyasema mkuu maana kuna msemo unasema; "Lisemwalo lipo na kama halipo, linakuja na kama bado halijafika basi huenda limepotea njia".

Baada ya kurudi nyuma na kuzisoma vyema taarifa na mabandiko kadhaa ya ndugu Daemusin na aina ya uwasilishaji wake, naweza kusema kwamba; You have a point! na huenda kweli kuna mshabihiano wa kiuandishi kutokana na matumizi ya aina fulani hivi ya uwasilishaji taarifa yenye burudani ndani yake.

Lakini hii nadhani ni aina fulani ya uwasilishaji wa taarifa utakaomvutia msomaji kukifuatila na kukielewa kile kilichoandikwa bila kujali msomaji yuko katika hali gani; hasira, furaha, huzuni, msongo wa mawazo, kukosa fedha, kukosa chakula, kukosa mke au mume, kukosa usingizi n.k.

Katika maisha sikuzote ni jambo jema sana mtu kuwa ni mwenye furaha wakati wote na moja ya kazi kubwa za Tasnia ya Burudani ni kuhakikisha kwamba watu wanaburudika ikiwemo pia kuwafanya wawe na furaha ili waishi maisha marefu (kwa mujibu wa tafiti za kisayansi) na ndio dhumuni pia la kuitumia aina hii ya uandishi katika jukwaa hili la Burudani ama Entertainment.

Nimezipitia taarifa na mabandiko yaliyopita hivi karibuni katika kipindi ambacho sikuingia katika huu uzi hususan mabandiko ya ndugu Daemusin bin Koroshow bin Makinikiyya (bin ziko kama mia hivi) na nimpongeze kwa aina yake ya uwasilishaji taarifa na jinsi gani unavyoweza kumfanya msomaji akaifuatilia taarifa na kuielewa huku akibaki kucheka mwenyewe kama 'chizi'.

Nimalizie hivi;
Maisha yamebadilika sana na ukitaka kuamini hilo, hapo kabla kulikuwa na kamsemo 'wahenga wa kisasa' walioko humu wanakakumbuka kanasema "Hata uoge vipi, mjini huendi". Ila siku hizi kuna mpya; "Kama hujaoga, usije mjini". Kweli maisha yamebadilika sana.

Nimemaliza.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Siku yangu imeanza vizuri barikiwa
 
Naomba nikujibu kama ifuatavyo:

Kuna msemo wa zamani ila naweza kuutumia hata hivi sasa na wala si vibaya na wewe msomaji 'kuuiba' ukautumie mahala pengine unasema;

"Beauty is in the eye of the beholder"

Unapouzungumzia ukali wa Filamu/Movie/Drama fulani unaweza usifanane kimtazamo na 'Mtazamaji' mwingine ingawa kuna msemo mwingine wa 'Mitaani' unasema;

"Chema chajiuza, kibaya chajitembeza"

Na tukienda na huo msemo No.2 kwamba kuna Drama ambayo 'huenda' ni kali kuliko hiyo 'Jumong' tunaweza tukajikuta tunarudi palepale kwenye ule msemo wa kwanza.

Anyway! Ngoja Nijaribu;

1) Hapo zamani za kale palitokea msichana mmoja ambaye alikuwa na 'tuakili twingi' kiasi kwamba hata Mfalme wa wakati huo katika hiyo nchi ijulikanayo kwa jina la 'Joseon' alikuwa akikapenda hako kabinti kwa jinsi kalivyokuwa jasiri na pia kutumia kipaji chake kutetea wanyonge a.k.a. 'Mtetezi wa Wanyonge' hasa katika maswala ya kisheria.

Sijatunga hadithi hapo, la hasha, bali hiyo ni Drama 'kali' kabisa iliyopewa jina la Flower in Prison ambamo humo ndani, huyo binti alizaliwa humo humo yaani Gerezani na akakulia humo mpaka kufikia 'utu uzima' (Kiswahili hicho) na kujifunza mambo mengi humohumo ndani ya Gereza ikiwemo ujasusi (na wizi vilevile).

Duniani kuna misemo mingi na mwingine huu hapa unasema; "Wanawake wakiwezeshwa wanaweza".

Hiyo Drama ni nzuri na ukitaka kujua ni kwanini basi nitakujibu kuwa; "Nimetumia ule msemo wa kwanza pale juu".

Humo ndani utakutana na Ok-nyeo, ambaye ndiye huyo msichana nafasi hiyo ikichezwa na Jin Se-hyun. Pia kuna Characters wengine kama; Yun Tae-won, Queen Munjeong na wengine wengi bila kumsahau Mzee Jun Kwang-ryul aliyeigiza kama Mfalme Geuma katika Jumong lakini huku akiigiza kama Park Tae-su

Nadhani nimeielezea vya kutosha na niishie hapo ila itafuteni hiyo ni nzuri, ya kusisimua na kuvutia pengine kuliko zile 'sauti za watu fulani' zilizovuja.

2) Maisha ni safari ndefu sana ukizingatia toka kipindi cha Bidam sorry! huyo Jumong, mpaka kipindi cha mwanamke shupavu na 'mkorofi' aitwaye Sungnyang a.k.a. The Jackal ama kama hayo majina ni mabaya kwako basi tumia hili lenye mvuto zaidi; Empress Ki.

Yeah! namzungumzia huyo, Empress Ki katika miaka hiyo ambayo 'wewe msomaji' hujazaliwa (hata wale waliosikika kwenye zile sauti zilizovuja walikuwa bado pia hawajazaliwa).

Ni miaka ya 1300 huko kipindi cha Ufalme wa Yuan, Uchina kama sijakosea maana hata mimi mwenyewe sikuwepo.

Huyo alikuwa 'Mkoryeo' yaani mzaliwa wa taifa la Goryeo na alipelekwa Yuan kipindi hicho kama mtumwa pamoja na ndugu zake wengine na alipitia mambo mengi sana mpaka kufika huko Yuan.

Hiyo Drama inafahamika sana kwa hilo hilo jina, Empress Ki na inaelezea harakati zake huyo 'Empress Ki' ama 'Lady Ki' mpaka anapokuja kuwa Malkia katika taifa hilo la ugeni.

Humo ndani ya hiyo Drama utawakuta magwiji kama vile; Ha Ji-won akiigiza kama Sungnyang ama Empress Ki bila kumsahau Ji Chang-wook akiigiza kama Ta hwan.

Ni Drama kali kuliko 'kisu' ila kwa kutumia ule msemo wa kwanza kabisa niliyoutoa, utaamua mwenyewe baada ya kuitazama kama hiyo Jumong inasimama hapo ama la.

3) Kwenye 'Point' yangu namba mbili hapo juu nilimtaja mtu mmoja aitwaye 'Bidam' kimakosa lakini ndiyo huko huko ninakoelekea.

Kipindi cha miaka ya 500 mwishoni mpaka katikati ya miaka ya 600, Dunia ilikuwepo kama kawaida.

Katika vitabu vya Historia ya huko Mashariki ya Mbali vinatuambia kuwa, alikuwepo mwanamke maarufu sana kipindi kile kutokana na maarifa, hekima na busara bila kusahau 'ujasiri' aliokuwa nao dhidi ya 'Mabeberu' na 'Mafisadi' ya kipindi kile. Hapa namaanisha Great Queen Seon Deok wa Shilla (Silla).

Alifahamika kama Deokman, jina lake la utotoni na kipindi anakuwa....Dah! nimeenda mbali sana.

Nirudi kidogo; Deokman alizaliwa katika familia ya Kifalme na hakuzaliwa peke yake bali alizaliwa na pacha wake. Waswahili mnapenda kusema "Kulwa na Doto".

Kutokana na 'utabiri' uliokuwepo toka zamani katika taifa la Silla ama (Shilla) ni kwamba endapo Mfalme atapata watoto mapacha wakike katika uzao wake basi uzao wa kiume wa Kifalme utakoma na Mfalme anaweza kuupoteza Ufalme wake na hata Malkia pia kuondolewa katika nafasi hiyo bila kuurithisha huo Ufalme.

Kutokana na hilo la uzao wa kiume, na pia kutokana na Mfalme kuhofia kupotea kiti chake cha Ufalme, kwa amri yake Mfalme, mtoto mmoja (huyo Deokman) alifichwa na kisha kutoroshwa na kijakazi wake aitwaye Sohwa, ambaye alienda kumlea kama mtoto wake wa kumzaa huko 'mafichoni'.

Samahani, huko mafichoni namaanisha sehemu ya mbali ambayo ilikuwa ni sehemu ya jangwa lililoko mbali sana na Silla. Hilo jangwa linafahamika kama 'Taklamakan' huko pande za Kaskazini Magharibi mwa Uchina.

Kizaazaa kinaanza pale Deokman (ambaye ndiye yule mtoto aliyetoroshwa) anapofikisha umri wa kujitambua na kuanza kuitafuta 'asili' yake (Origin) jambo ambalo linapelekea kurejea kule alikozaliwa (Silla) akiwa na maswali lukuki kichwani mwake ikiwemo pia kumtafuta mzazi wake wa kiume yaani baba yake.

Niishie hapo kwa leo maana nahisi namaliza uhondo wote humu. Ila tuu itafute hiyo Drama inayokwenda kwa jina la The Great Queen Seon Deok na kisha uitazame.

Kwa kweli hii naweza kusema ni moja wapo ya Filamu za Kikorea ambazo ni "Chema kimejiuza" na si "Kibaya kimejitembeza" kama usemavyo ule msemo wa pili kule juu.

Nimesahau kitu, huyo Bidam utamkuta humohumo kama Character aliyechezwa na Mtaalamu Kim Nam-gil kuanzia Episode ya 20/21 kama sijakosea.

Pia utawakuta Characters wengine kama vile Misil, Kim Yu-sin, Al-cheon bila kuwasahau Jukbang na Godo.

Ahsante. Na karibu kwa Maswali!
Flower in prison ni kali balaa nimeifatilia had episode ya 10 youtube duh!
 
Back
Top Bottom