Uliposema kuwa kuna mshabihiano wa kiuandishi nikasema 'isiwe tabu' ngoja niurudishe huu uzi nyuma ili kupata kuyashuhudia mwenyewe hayo unayoyasema mkuu maana kuna msemo unasema; "Lisemwalo lipo na kama halipo, linakuja na kama bado halijafika basi huenda limepotea njia".
Baada ya kurudi nyuma na kuzisoma vyema taarifa na mabandiko kadhaa ya ndugu Daemusin na aina ya uwasilishaji wake, naweza kusema kwamba; You have a point! na huenda kweli kuna mshabihiano wa kiuandishi kutokana na matumizi ya aina fulani hivi ya uwasilishaji taarifa yenye burudani ndani yake.
Lakini hii nadhani ni aina fulani ya uwasilishaji wa taarifa utakaomvutia msomaji kukifuatila na kukielewa kile kilichoandikwa bila kujali msomaji yuko katika hali gani; hasira, furaha, huzuni, msongo wa mawazo, kukosa fedha, kukosa chakula, kukosa mke au mume, kukosa usingizi n.k.
Katika maisha sikuzote ni jambo jema sana mtu kuwa ni mwenye furaha wakati wote na moja ya kazi kubwa za Tasnia ya Burudani ni kuhakikisha kwamba watu wanaburudika ikiwemo pia kuwafanya wawe na furaha ili waishi maisha marefu (kwa mujibu wa tafiti za kisayansi) na ndio dhumuni pia la kuitumia aina hii ya uandishi katika jukwaa hili la Burudani ama Entertainment.
Nimezipitia taarifa na mabandiko yaliyopita hivi karibuni katika kipindi ambacho sikuingia katika huu uzi hususan mabandiko ya ndugu
Daemusin bin Koroshow bin Makinikiyya (bin ziko kama mia hivi) na nimpongeze kwa aina yake ya uwasilishaji taarifa na jinsi gani unavyoweza kumfanya msomaji akaifuatilia taarifa na kuielewa huku akibaki kucheka mwenyewe kama 'chizi'.
Nimalizie hivi;
Maisha yamebadilika sana na ukitaka kuamini hilo, hapo kabla kulikuwa na kamsemo 'wahenga wa kisasa' walioko humu wanakakumbuka kanasema "Hata uoge vipi, mjini huendi". Ila siku hizi kuna mpya; "Kama hujaoga, usije mjini". Kweli maisha yamebadilika sana.
Nimemaliza.