je wajua takribani asilimia 90 ya screen writers nchini korea ni wanawake?
je wajua ni asilimia 27 tu ya wanawake nchini marekani ndio wanabeba kundi lote la directors, writers, producers, executive producers, editors pamoja na photography directors.
nimemkumbuka yule bwana kiongozi
aliyewambia wanawake uchumi mnao lakini bahati mbaya sana mumeukalia.
jamani nimekusudia uchumi wa fikra chanya zitakazowawezesha kuwa level moja kiheshima na jinsia ya kiume kwenye ishu zote muhimu za kijamii,.
haitowezekana kwa wanawake kuondoa utegemezi kwa wanaume a.k.a mfumo dume ikiwa watashindwa kuitumia vizuri rasilimali muhimu tuliopewa jinsia zote mbili bila ya ubaguzi (rasilimali maarifa).
nimeona niweke list ya waandishi maarufu wa kike nchini korea ambao bada wanaendelea kuleta ushindani kwa wanaume.
Kim Young Hyun : huyu mwanamama aliyezaliwa mwaka 1966 nikimpa heshima ya ugenius nitakua nimekosea?
kabla hajaanza kushirikiana na bwana park sang yeon huyu mwanamama aliandika project mbili za hatari zilizoebeba maudhui ya kihistoria nazo ni jewel in the palace pamoja na song of the prince a.k.a ballad of seodong drama.
huo ulikuwa ni mwanzo tu wa moto wake wa gesi usiozimika, kwa kushirikiana na bwana park sang yeon wamefanikiwa kuandika project bora kama vile
tree with deep root,
arhthdal chronicles, six flying dragons pamoja na t
he great queen seondeok drama, hivi nikimpa heshima ya queen wa uandishi nitakuwa nimekosea?
kim eun seok : ameandika drama nyingi zilizojibebea umaarufu mkubwa sana ndani na nje ya korea. Miongoni mwa drama zilizoandikwa na huyu mwanamama ni pamoja na
mr sunshine, goblin, secret garden, The gentlemen's dignity, descendent of the sun, love in paris, the heirs pamoja na drama ijayo ya mwaka 2020 inayoitwa
the king: the eternal monarch ambayo itamkutanisha tena na muigizaji
lee min ho pamoja na mwanadada
kim go eun.
kim eun hee: rafiki wa karibu sana wa mwanamama kim eun seok, ukweli utaendelea kubaki vile vile milele huyu mama amejijengea sifa kubwa sana za uandishi wa hadithi zinazokufanya muda wote utamani uwepo kwenye televisheni upate kufahamu kinachojiri mbeleni,
project yake ya kwanza kuiona ilikuwa ni
signal ambayo ilifanya vizuri sana mnamo mwaka 2015, pia ameandika drama inayoitwa
3 days kwa aliyebahatika kuiangalia atafahamu ubora wake, huyu ahjumma pia ndiye muandishi wa drama inayoonekana kupitia netflix naikusudia historical drama inayoitwa
kingdom wazee wa zombie ambayo kwa sasa ipo kwenye maandalizi ya season 2. Huyu mwanamama pia ameandika medical drama inayoitwa
sign pamoja na
phantom a.k.a
ghost drama
noo hee kyung : genius mwengine aliyezaliwa mwaka 1966, ameandika drama nyingi sana tokea mwaka 1996, drama zake maarufu ni pamoja na
that winter the wind blows, live, the most beautiful good bye, padam padam, dear my friend pamoja na its ok, this is love drama.
song ja jung : huyu mama ndiye muandishi mkuu wa drama inayoitwa
memories of alhambra ambayo ilinifanya baadhi ya nyakati niugue ugonjwa wa wazimu wa kupenda technology kwa kile nilichokuwa nakishuhudia mule ndani, pia ameandika
W: two world drama, queen in hyeons man, three musketers n.k
Lee Kyoung Hee: miongoni mwa drama alizoandika ni pamoja na
a love to kill, unontrollably fund, innocent man pamoja na upcoming drama inayoitwa
chocolate itakayowakutanisha
ha ji won(empress ki) na
yoon kye sang (road no 1)
Park Ji Eun: mtaalamu wa super natural drama project zake nilizofanikiwa kuziona ni pamoja
the legend of blue sea, my love from another star pamoja na
the producers.
HONG SISTERS : ni muunganiko wa ndugu wawili wawili wanaojuwa kucheza na sanaa ya uandishi wa hadithi zenye kuvutia wameshafanikiwa kuandika drama nyingi sana ambazo zimeshuhudiwa kufanya vizuri. miongoni mwa drama walizoandika ni pamoja na
korean odyssey (hwayugi), master's sun, hong gil dong, you are beautiful, my girlfriend is gumiho na hotel del luna drama inayoendelea kuonyeshwa na kituo cha tvn.
park hye run: kwa aliyebahatika kuangalia
while you were sleeping, pinoccio, i can hear your voice ambazo zote kwa pamoja muigizaji alikuwa ni lee jong suk atafahamu ubora na ubunifu aliojaaliwa kuwa nao huyu mwanamama.pia ameandika drama inayoitwa
dream high.
pichani: mwanamama kim young hyun akiwa pamoja na muandishi park sang yeon.
nimeshindwa kuweka picha za waandishi wengine kwa kuhofia kujaza picha nyingi ndani ya comment moja.
hivi bongo tuna waandishi wangapi mashuhuri kwa kuangalia jinsia zote wanaofahamika nje ya mipaka ya nchi yetu?