Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Bila shaka ni drama nzuri. Drama za mjini za kipindi kile zilikuwa hazichoshi kama za siku hizi.

Achana nae huyo Daemushin anashabikia timu za kurithishwa( Thimba na Yanga) toka kwa babu yake.
siwezi kushabikia timu ambazo ndio kwanza zimetoka usingizini, leo hii vilabu hivi viwili ndio vimeshitukia mpango wa kuuza vifaa vyenye nembo zao ili wajitengenezee kipato kitakachowawezesha kuachana na tabia dhaifu ya kuomba omba.

ukitaka unikere mpaka nitamani nikupige mpaka uchakae niwekee mpira wa afrika kwenye televisheni.

mabeberu waliojificha kwenye kivuli cha demokrasia wameshaniathiri tokea nilipokuwa sijaingia kwenye umri wa ujana mpaka muda huu nimeshaingia kwenye umri wa uzee mwisho chalinze
 
je wajua takribani asilimia 90 ya screen writers nchini korea ni wanawake?

je wajua ni asilimia 27 tu ya wanawake nchini marekani
ndio wanabeba kundi lote la directors, writers, producers, executive producers, editors pamoja na photography directors.

nimemkumbuka yule bwana kiongozi aliyewambia wanawake uchumi mnao lakini bahati mbaya sana mumeukalia.
jamani nimekusudia uchumi wa fikra chanya zitakazowawezesha kuwa level moja kiheshima na jinsia ya kiume kwenye ishu zote muhimu za kijamii,.
haitowezekana kwa wanawake kuondoa utegemezi kwa wanaume a.k.a mfumo dume ikiwa watashindwa kuitumia vizuri rasilimali muhimu tuliopewa jinsia zote mbili bila ya ubaguzi (rasilimali maarifa).

nimeona niweke list ya waandishi maarufu wa kike nchini korea ambao bada wanaendelea kuleta ushindani kwa wanaume.​

Kim Young Hyun : huyu mwanamama aliyezaliwa mwaka 1966 nikimpa heshima ya ugenius nitakua nimekosea?
kabla hajaanza kushirikiana na bwana park sang yeon huyu mwanamama aliandika project mbili za hatari zilizoebeba maudhui ya kihistoria nazo ni jewel in the palace pamoja na song of the prince a.k.a ballad of seodong drama.
huo ulikuwa ni mwanzo tu wa moto wake wa gesi usiozimika, kwa kushirikiana na bwana park sang yeon wamefanikiwa kuandika project bora kama vile tree with deep root, arhthdal chronicles, six flying dragons pamoja na the great queen seondeok drama, hivi nikimpa heshima ya queen wa uandishi nitakuwa nimekosea?

kim eun seok : ameandika drama nyingi zilizojibebea umaarufu mkubwa sana ndani na nje ya korea. Miongoni mwa drama zilizoandikwa na huyu mwanamama ni pamoja na mr sunshine, goblin, secret garden, The gentlemen's dignity, descendent of the sun, love in paris, the heirs pamoja na drama ijayo ya mwaka 2020 inayoitwa the king: the eternal monarch ambayo itamkutanisha tena na muigizaji lee min ho pamoja na mwanadada kim go eun.

kim eun hee:
rafiki wa karibu sana wa mwanamama kim eun seok, ukweli utaendelea kubaki vile vile milele huyu mama amejijengea sifa kubwa sana za uandishi wa hadithi zinazokufanya muda wote utamani uwepo kwenye televisheni upate kufahamu kinachojiri mbeleni,
project yake ya kwanza kuiona ilikuwa ni signal ambayo ilifanya vizuri sana mnamo mwaka 2015, pia ameandika drama inayoitwa 3 days kwa aliyebahatika kuiangalia atafahamu ubora wake, huyu ahjumma pia ndiye muandishi wa drama inayoonekana kupitia netflix naikusudia historical drama inayoitwa kingdom wazee wa zombie ambayo kwa sasa ipo kwenye maandalizi ya season 2. Huyu mwanamama pia ameandika medical drama inayoitwa sign pamoja na phantom a.k.a ghost drama

noo hee kyung
: genius mwengine aliyezaliwa mwaka 1966, ameandika drama nyingi sana tokea mwaka 1996, drama zake maarufu ni pamoja na that winter the wind blows, live, the most beautiful good bye, padam padam, dear my friend pamoja na its ok, this is love drama.

song ja jung :
huyu mama ndiye muandishi mkuu wa drama inayoitwa memories of alhambra ambayo ilinifanya baadhi ya nyakati niugue ugonjwa wa wazimu wa kupenda technology kwa kile nilichokuwa nakishuhudia mule ndani, pia ameandika W: two world drama, queen in hyeons man, three musketers n.k

Lee Kyoung Hee: miongoni mwa drama alizoandika ni pamoja na a love to kill, unontrollably fund, innocent man pamoja na upcoming drama inayoitwa chocolate itakayowakutanisha ha ji won(empress ki) na yoon kye sang (road no 1)

Park Ji Eun: mtaalamu wa super natural drama project zake nilizofanikiwa kuziona ni pamoja the legend of blue sea, my love from another star pamoja na the producers.

HONG SISTERS :
ni muunganiko wa ndugu wawili wawili wanaojuwa kucheza na sanaa ya uandishi wa hadithi zenye kuvutia wameshafanikiwa kuandika drama nyingi sana ambazo zimeshuhudiwa kufanya vizuri. miongoni mwa drama walizoandika ni pamoja na korean odyssey (hwayugi), master's sun, hong gil dong, you are beautiful, my girlfriend is gumiho na hotel del luna drama inayoendelea kuonyeshwa na kituo cha tvn.

park hye run: kwa aliyebahatika kuangalia while you were sleeping, pinoccio, i can hear your voice ambazo zote kwa pamoja muigizaji alikuwa ni lee jong suk atafahamu ubora na ubunifu aliojaaliwa kuwa nao huyu mwanamama.pia ameandika drama inayoitwa dream high.

1564932520549.png
pichani: mwanamama kim young hyun akiwa pamoja na muandishi park sang yeon.
nimeshindwa kuweka picha za waandishi wengine kwa kuhofia kujaza picha nyingi ndani ya comment moja.

hivi bongo tuna waandishi wangapi mashuhuri kwa kuangalia jinsia zote wanaofahamika nje ya mipaka ya nchi yetu?
 
Shukran,hii imekubali kwa kutumia torrent ila nayo baadhi ya projects haina mfano the great seer. Ila vikorea vitamu sijui nani kaivuruga dramania mpaka tukakosa uhondo
upo sahihi baadhi ya nyakati inazingua sana hususani kwa zile episode mpya zinazowekwa ila kwa project za zamani ipo vizuri sana.
jaribu kutumia kissasian.sh
 
Shukran,hii imekubali kwa kutumia torrent ila nayo baadhi ya projects haina mfano the great seer. Ila vikorea vitamu sijui nani kaivuruga dramania mpaka tukakosa uhondo
ndio udhaifu wake hiyo website, project nyingi za kizamani utazipata dramanice au dramacool.
chengine nilichokigundua ni kwamba tovuti nyingi sana wanaitegemea dramanice, kama itatokezea dramanice wameshindwa kuweka subtitle ya drama basi na tovuti nyengine nazo zitafuata nyayo zake
 
je wajua takribani asilimia 90 ya screen writers nchini korea ni wanawake?

je wajua ni asilimia 27 tu ya wanawake nchini marekani
ndio wanabeba kundi lote la directors, writers, producers, executive producers, editors pamoja na photography directors.

nimemkumbuka yule bwana kiongozi aliyewambia wanawake uchumi mnao lakini bahati mbaya sana mumeukalia.
jamani nimekusudia uchumi wa fikra chanya zitakazowawezesha kuwa level moja kiheshima na jinsia ya kiume kwenye ishu zote muhimu za kijamii,.
haitowezekana kwa wanawake kuondoa utegemezi kwa wanaume a.k.a mfumo dume ikiwa watashindwa kuitumia vizuri rasilimali muhimu tuliopewa jinsia zote mbili bila ya ubaguzi (rasilimali maarifa).

nimeona niweke list ya waandishi maarufu wa kike nchini korea ambao bada wanaendelea kuleta ushindani kwa wanaume.​

Kim Young Hyun : huyu mwanamama aliyezaliwa mwaka 1966 nikimpa heshima ya ugenius nitakua nimekosea?
kabla hajaanza kushirikiana na bwana park sang yeon huyu mwanamama aliandika project mbili za hatari zilizoebeba maudhui ya kihistoria nazo ni jewel in the palace pamoja na song of the prince a.k.a ballad of seodong drama.
huo ulikuwa ni mwanzo tu wa moto wake wa gesi usiozimika, kwa kushirikiana na bwana park sang yeon wamefanikiwa kuandika project bora kama vile tree with deep root, arhthdal chronicles, six flying dragons pamoja na the great queen seondeok drama, hivi nikimpa heshima ya queen wa uandishi nitakuwa nimekosea?

kim eun seok : ameandika drama nyingi zilizojibebea umaarufu mkubwa sana ndani na nje ya korea. Miongoni mwa drama zilizoandikwa na huyu mwanamama ni pamoja na mr sunshine, goblin, secret garden, The gentlemen's dignity, descendent of the sun, love in paris, the heirs pamoja na drama ijayo ya mwaka 2020 inayoitwa the king: the eternal monarch ambayo itamkutanisha tena na muigizaji lee min ho pamoja na mwanadada kim go eun.

kim eun hee:
rafiki wa karibu sana wa mwanamama kim eun seok, ukweli utaendelea kubaki vile vile milele huyu mama amejijengea sifa kubwa sana za uandishi wa hadithi zinazokufanya muda wote utamani uwepo kwenye televisheni upate kufahamu kinachojiri mbeleni,
project yake ya kwanza kuiona ilikuwa ni signal ambayo ilifanya vizuri sana mnamo mwaka 2015, pia ameandika drama inayoitwa 3 days kwa aliyebahatika kuiangalia atafahamu ubora wake, huyu ahjumma pia ndiye muandishi wa drama inayoonekana kupitia netflix naikusudia historical drama inayoitwa kingdom wazee wa zombie ambayo kwa sasa ipo kwenye maandalizi ya season 2. Huyu mwanamama pia ameandika medical drama inayoitwa sign pamoja na phantom a.k.a ghost drama

noo hee kyung
: genius mwengine aliyezaliwa mwaka 1966, ameandika drama nyingi sana tokea mwaka 1996, drama zake maarufu ni pamoja na that winter the wind blows, live, the most beautiful good bye, padam padam, dear my friend pamoja na its ok, this is love drama.

song ja jung :
huyu mama ndiye muandishi mkuu wa drama inayoitwa memories of alhambra ambayo ilinifanya baadhi ya nyakati niugue ugonjwa wa wazimu wa kupenda technology kwa kile nilichokuwa nakishuhudia mule ndani, pia ameandika W: two world drama, queen in hyeons man, three musketers n.k

Lee Kyoung Hee: miongoni mwa drama alizoandika ni pamoja na a love to kill, unontrollably fund, innocent man pamoja na upcoming drama inayoitwa chocolate itakayowakutanisha ha ji won(empress ki) na yoon kye sang (road no 1)

Park Ji Eun: mtaalamu wa super natural drama project zake nilizofanikiwa kuziona ni pamoja the legend of blue sea, my love from another star pamoja na the producers.

HONG SISTERS :
ni muunganiko wa ndugu wawili wawili wanaojuwa kucheza na sanaa ya uandishi wa hadithi zenye kuvutia wameshafanikiwa kuandika drama nyingi sana ambazo zimeshuhudiwa kufanya vizuri. miongoni mwa drama walizoandika ni pamoja na korean odyssey (hwayugi), master's sun, hong gil dong, you are beautiful, my girlfriend is gumiho na hotel del luna drama inayoendelea kuonyeshwa na kituo cha tvn.

park hye run: kwa aliyebahatika kuangalia while you were sleeping, pinoccio, i can hear your voice ambazo zote kwa pamoja muigizaji alikuwa ni lee jong suk atafahamu ubora na ubunifu aliojaaliwa kuwa nao huyu mwanamama.pia ameandika drama inayoitwa dream high.

pichani: mwanamama kim young hyun akiwa pamoja na muandishi park sang yeon.
nimeshindwa kuweka picha za waandishi wengine kwa kuhofia kujaza picha nyingi ndani ya comment moja.

hivi bongo tuna waandishi wangapi mashuhuri kwa kuangalia jinsia zote wanaofahamika nje ya mipaka ya nchi yetu?
Hapo zamani, wahenga waliwahi kusema; "Akili ni mali" na pia wakajitokeza tena na kusema; "Akili ni nywele, kila mtu ana zake".

Lakini haitoshi tu mtu kuwa na akili kichwani bila kuitumia ipasavyo ili iweze kuleta mafanikio kwake na pia iwe faida kwa jamii inayomzunguka.

Nimepata kuzitazama Projects kadhaa kati ya hizo zilizoandikwa na hao wanawake kama vile;
  • The Heirs
  • Queen In Hyun's Man
  • Six Flying Dragons
  • The Great Queen Seon Deok
  • Tree With Deep Roots
  • Legend Of The Blue Sea
  • W: Two Worlds
  • Descendants Of The Sun
  • Innocent Man
  • Master's Sun
  • I Can Hear You Voice
  • Pinocchio n.k.
Kiukweli ni 'akili nyingi' pamoja na utulivu wa hali ya juu uliotumika kuziandaa hasa katika uandishi wa Scripts ama Screenplays zake.

Hakika wanastahili pongezi za hali ya juu kutokana na akili na mawazo yao (Ideas) kwa sababu uandishi ni moja ya kazi kubwa sana katika uandaaji wa filamu au sinema na bila hivyo sidhani kama tungeweza kuzifurahia.

Bila kazi yao kubwa pengine tusingewaona akina Lee Mun Sik, Jun Ji Hyun, Rain, Shin Min Ah na wengineo wakiwa Confident ama wakijinafasi mbele ya kamera ama tungeshuhudia wakiigiza vitu visivyoeleweka.
 
Hapo zamani, wahenga waliwahi kusema; "Akili ni mali" na pia wakajitokeza tena na kusema; "Akili ni nywele, kila mtu ana zake".

Lakini haitoshi tu mtu kuwa na akili kichwani bila kuitumia ipasavyo ili iweze kuleta mafanikio kwake na pia iwe faida kwa jamii inayomzunguka.
sina cha kuongeza kwenye andiko lako na kama ni mtihani umeramba 10.
huo msemo wa akili ni nywele kila mtu ana zake nauchukia sana, ina maana sisi tuliojaaliwa na nywele kipilipili ndio uwezo wetu wa kufikiri utaendela kuwa mdogo kama nywele zetu?
 
Hilo swala limeleta mjadala mkubwa sana kwamba 'wahenga' walifikiria nini kufananisha akili na nywele?

Labda wao walikuwa na 'manywele' marefu na mengi kiasi kwamba waliona ni kitu cha kujisifia.
 
kama unatumia PC jaribu kutembelea link nilioiweka hapo juu baadae utachagua try internet download manager for free.

utaifanyia installation setup yako ndipo baadae utaianza kuitumia kwa siku 30 lakini kabla ya siku hizo kufika wataanza kukuletea ujumbe wa kukutaka ufanye usajili wa software yako.
Ili kuepusha hayo jaribu kuwatafuta wajuzi zaidi wapate kukusaidia kupata idm software iliokuwa cracked.

unaweza kutembelea link hii ukawaomba wajuzi wakupe msaada au unaweza kutembelea jukwaa la teknolojia wapo wataalamu zaidi wasiokuwa na chembe ya roho mbaya.

usisahau kuwa na browser mfano wa chrome, mozilla au brave browser.​
Mkuu anaweza kutumia torch browser maana haihitaji idm,ni nzuri
 
Jamani ebu jaribu kuangalia hizi series za kikorea za town ni noma na utajuta kuangalia
1.innocent dependent
Tukea nianze kuangalia series zote za kizungu,kichina,Korea zijaona series Kali Kama hii inaubunifu story Safi na matukio ambayo hayatabiliki hii ni zaidi ya prison break,lost n.k ndo nikajiita hii jina nitawadithia kifupi;
Kuna familia moja ya kitajiri ilikuwa na watoto mapacha waliofanana mkubwa na mdogo,mkubwa alikuwa anapendwa Sana na alikuwa very smart ndio alipewa jukumu la kusimamia hiyo company huku mdogo alikuwa sio smart na wazazi wake walikuwa hawampendi.Na kitu pekee kilichowatofautisha ni tabia zao na life style yao.Mkubwa alikuwa mpenda wanawake lakini pia alikuwa mpole wakati mdogo alikuwa mkorofi na anayependa Sana kupigana.kuna siku moja mdogo aliweza kufanya mauaji kwa mwanamke mmoja lakini baadae aligundulika na polisi lakini polisi wakishindwa kujua aliyeua alikuwa pacha mkubwa Hama mdogo kutokana na kufanana kwao.Pacha mkubwa alijua pia mdogo wake ameua baada ya pacha mdogo kujua kaka amejua alichokifanya nimsukuma kutoka ghorofani mpaka chini ili amuue na pia kutengeneza mazingira ili ionekane kaka yake ndio alimuua yule msichana ili yeye asiende jela lakini yule pacha mkubwa hakufa pale pale aliwaishwa hospital muda mfupi baada ya tukio Hilo kutokea lakini aliyemtupa hakuonekana baada ya kufikishwa hospital polisi mmoja akata kumuhoji ambaye ndio star wa series hii before hajafa akaita jina la mdogo wake huku akimuangalia kitu ambacho kilimshangaza yule polisi na kwanini ajiite jina lake huku akimuangalia pacha wake kumbuka kwamba pacha mdogo amechukua nafasi ya kaka yake kwahiyo jina la kaka amelifanya lake na kila kitu Cha kaka yake ili watu wamjue Kama pacha mkubwa baada ya pacha kuita jina la pacha wake akafanya moja kwa moja kutokana na mashaka aliyoingia kwa huye polisi akabidi aanze kufatilie hii case Ili ajue ni kweli huyu pacha aliyehai ni pacha mkubwa?.Tukiacha upande wa pacha tuje upande wa polisi huyu polisi alikuwa ana familia yake ambayo alikuwa anaipenda Sana ila Kuna siku moja akajikuta yupo jela wakati akiamka akaanza kushangaa lkn sisi watazamaji hatukuoneshwa alifikaje jela wakati yule polisi anashangaa amefikaje polisi wafungwa wenzake wanamwambia upo humu jela miaka mitano Hadi Sasa na umeukumiwa kwa kosa la kuuwa familia yako na ukizingatia hule polisi Hana hata kumbukumbu yalichotokea.swali je yule polisi ni kweli ameua? Je Kama ameua familia yake amewaua kwa sababu zipi? Je vipi kuhusu yule pacha mdogo anaejifanya yeye ni pacha mkubwa je ataweza kumaintain status ya pacha mkubwa na challenge zipi atazokutana nazokutana nazo je ataweza kuzishinda maana si rahisi kuiba style ya maisha ya kaka yake pamoja na kuiongoza company ya kaka yake.Ili kujua yote itafute hii series hii Kali kupata kutokea na hatujuta kupoteza bando lako
2.last
Nayo hii nzuri kwel kweli pia hii nayo ni ya kikorea Ina episode 16.
Hizi series mbili nilizokutajia hapo ukiziangalia tu hautakuwa na hamu tena ya kuangalia series za kikorea za vijijini mnazozinadi humu jamiiforum.
 
Back
Top Bottom