Gwanggaeto the Great
JF-Expert Member
- Apr 14, 2018
- 831
- 1,792
Huyo mzee anajua, na Hajawahi kutoa Project mbovu.zimesimamiwa na legendary director lee
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo mzee anajua, na Hajawahi kutoa Project mbovu.zimesimamiwa na legendary director lee
Basi pitia tena historia duniaHahah Haya mambo ni sehemu ya Historical Drama tunazotazama.
Halafu hili ndilo jukwaa langu pendwa na wala sijawahi kwenda wala kupita kwenye majukwaa mengine.
Kinachovutia na kufundisha ni namna aliyotumia kuwavuta kwake ili wampende( endelea nayo ) ni nzuri kuliko Mary me nowmarry me now na what happened to my family zote hizi nilianza kuzifuatilia siku moja ila ilifika wakati niliamua kuitelekeza what happened to my family (niliishia episode 15), hii project ya what happened to my family ni ya mwaka 2014 lakini kilichokuwa kinanistaajabisha kupitia macho yangu nilikuwa namuona mzee yoo dong geun kama amedhoofu kiafya tofauti na nilivyokuwa nikimouna ndani ya marry me now drama (project ya mwaka 2018).
huenda macho yangu yana ukungu mweusi au pengine ule uhusika wake uliokuwa umezungukwa zaidi na changamoto kubwa alizokuwa akizipitia kutoka kwa watoto wake ndio zilipelekea awe na afya dhaifu iliyoambatana na ukosaji wa furaha, msongo wa mawazo na tabasamu la kweli....
kitendo cha kujaaliwa kuwa na familia bora yenye afya ni baraka kubwa sana ulizopewa na Muumba haijalishi awe amewanyima maisha bora yenye kuambatana na upataji wa hitaji lolote la nafsi munalohitaji (umasikini) au ufukara,
wapo wengine waliojaaliwa mali na umiliki wa assets (current and non current) tofauti lakini walijikuta wakikosa furaha ya nafsi kwa sababu ya kukosa upendo, au kutokuwa karibu na wazazi wao ili wapate kufaida matunda ya mafanikio (sidhani kama ronaldo anajisikia furaha kwa kumkosa baba yake kipindi hiki cha kula matunda ya mti unaoitwa mafanikio, hata kama baba yake angelikuwa bado ana tabia ya ulevi bila ya shaka angelijisikia furaha japo kishingo upande kuliko kutokuwepo kabisa kwa baba yake)
pia matukio ya kila siku yanatokozea ndani ya dunia yetu ni mwalimu mzuri sana wa kutufunza na hata kutukosowa pindi tunapokwenda kinyume na matendo ya asili, hivyo basi Mungu anapokupa baraka ya wazazi bora waliojawa na huruma, utu, ihsani na uadilifu ndani ya nafsi zao unapaswa ushukuru kwani ni mara ngapi tumeshasikia na kushuhudia matukio ya kinyanyasaji yanaongozwa na wazazi dhidi ya watoto wao wa kuwazaa na kuwalea
unapobarikiwa kuwa na wazazi wanaojitolea kukupa mahitaji yote muhimu bila ya bughudha kama chakula, mavazi, elimu, makazi bora kama mtoto unapaswa uzidishe heshima na thamani kwa wazazi wako, hufahamu ni jinsi gani wazazi wako wanavyopigana huko barabarani, ofisini kwa lengo la kukutengenezea maisha yenye ubora kutokana na kipato chao.
hakuna mtoto mwenye uwezo wa kumlipa mzazi kutoka na wema aliofanyiwa japokuwa ni wajibu wa mzee kufanya hivyo, tusisubiri wazee wetu ni wagonjwa, wameshazeeka au wameshafariki ndio tuongoze kampeni ya upendo, heshima na kuwashukuru kwa yale waliotufanyia.
natumai wale wajinga watatu watajifunza na watajisahihisha mbeleni ya drama ile.
Kama six ni ya mwanamke basi kajitahidi japo hizi drama ya kihistoria ni mambo yaliyo kwenye historia ya Korea hivyo Jung do jeon ni muasisi WA mfumo bora WA siasa na umiliki WA ardhi kama inavyoelezwa humo. Inawafunza vijana na wanasiasa wa ulimwengu namna siasa inavyofanya kazi, mabadiliko yanavyopaswa kufanya na sadaka kutolewa inapohitajika bila kuathiri lengo husika licha ya lust of power.Yisan drama,bado sijapata tiba sahihi itakayonifanya niwe na morali ya kuiangalia hiyo project nikiwa na furaha, hamu, ari ya kutaka kufahamu kinachojiri mbeleni.
nakumbuka niliishia episode 21 mwaka uliopita (mfalme anapata ugonjwa wa ghafla baada ya kutoka kwenye ziara ya kuwatembelea wananchi wake).
huenda sababu kuu ni kutokuvutiwa na muigizaji mkuu (Lee seo jin), daemusin anasumbuliwa na ugonjwa wa wivu na roho mbaya.
halafu pia kuna Dong Yi (hii nakumbuka niliikuta kwa jirani wanaangalia, nyakati hizo daemusin ni fala fulani (dummy) kwenye ulimwengu wa korean), nayo kila siku naipigia kalenda ya kutaka kuiangalia.
===========================
tuacheni utani hawa wakorea wamejaaliwa waandishi na directors wenye ueledi, ubunifu na nidhamu kubwa sana kwenye kazi zao, inafika nyakati unashindwa kutofautisha ubora wa kazi inayoandaliwa na mwanaume au mwanamke (zote unaziona ni bora).
Kwa mujibu wa Center for the Study of Women in Television and Film wanasema ya kwamba nchini Marekani ni asilimia 27 tu ya wanawake ndio hushiriki kwenye shughuli za utengenezaji wa project hizi za sanaa ya maigizo (ndani yake kuna directors, writers, producers, executive producers, editors na photography directors).
Nchini korea wanawake wanabeba asilimia 90 ya screenwriters..............
kwa akili ya kawaida ikiwa umezowea mfumo dume basi inakuwa ni vigumu sana kuamini ya kwamba project hizi za kibabe (historical) zimeandikwa na mwanamke mmoja tu (kim yi young)
Yisan, Hwa Jung, The King’s Doctor (horse doctor), Dong Yi, Haechi........ (nilizozibold kwa wino mwekundu ndio nimeziangalia)
Dong Yi + Yisan + horse doctor = zote hizi zimesimamiwa na legendary director lee byung hoon
Nilifikiri mwanamama kim young hyun (ameandika arthdal chronicles, queen seondeok, jewel in the palace, six flying dragons, tree with deepo roots, ballad of seodong ) ndiye malikia pekee wa kuandika historical drama kumbe yupo mpinzani wake anayemfukuzia kwa kasi.
kongole kwako mwanamama Kim Yi Young.....
heshima kwenu wanawake wote wachapa kazi (mulioweza kufanikiwa na wenye ndoto au malengo ya kufanikiwa ),
pia heshima kwenu wanawake wote musiofanya kazi lakini maarifa yenu yakabaki kuwa msaada kwa wanaume
CIA na FBI kila mwaka wanatoa ripoti za pelelezi zilivyofanikiwa na zilizoshindwa kufanikiwa hasa FBI kwani sharia ya upelelezi marekani mwisho ni miaka 15 hivyo wakishimdwa, jalada linafungwa na kueleza namna walivypshindwa. Kesi nyingi hasa za mauaji na wizi zilishindikana kuwapata wahusika hata evidence za kutosha kuspeculate ukweli.ahsante sana, nitajaribu kuiendeleza mpaka nifahamu mwisho wake (pia nataka nifahamu vita kati ya secretary na mtoto wa bosi kubwa inamalizika vipi, nimeanza kunusa harufu ya upendo kati yao huko mbeleni, teh teh teh drama za korea ndivyo zilivyo)
dah! sikuwa nafahamu kama umeshaingia kwenye ulimwengu wa kuitwa baba(natumai ni kwa njia ya ndoa safi)......hongera sana kaka mkubwa.......sisi wengine tunasubiria muuaji wa karume Snr afahamike ndio tuingie kwenye ulimwengu wa ndoa rasmi.
sijui itakuwa ni mwaka gani
Eeh! Mfalme Daemusin utanipa kibali ili nipinge upotoshaji huu?!, au nitakuwa naenda kinyume na Kanuni za Nchi yetu?Mashariki ya kati na mbali ili wafanikiwe kama si viongozi WA nchi au makampuni ya kiuchumi yamesomesha watu ulaya, yameiba teknolojia ulaya marekan, wamewanunua wazungu waishi huko ili wawape uzoefu.
marry me now (shall we live together)
kilichonivutia na kujifunza
kilichonichukiza:
- mapenzi hayana muda maalum wala ukomo wa umri (the power of love)
- fanya kazi kwa bidii yenye kuambatana na nidhamu ili ujitengezee msingi bora wa maisha, wajapani wanasema mbora wao ni yule anayeanguka mara saba lakini mara ya nane akainuka tena, kwenye maisha hutakiwi kukata tamaa, (kongole kwake jang mi hee ahjumma, inaniwia vigumu kuamini ya kwamba huyu mama amezaliwa miaka 63 iliopita kwa umri wa korea)
- Muombe mungu akujaalie kwenye maisha yako uzungukwe na watu waliojawa upendo, utu dhidi yako kwa sababu hata kama utazungukwa na changamoto ngumu za kimaisha kama ugonjwa, anguko la kiuchumi basi upendo wao usio mithilika dhidi yako, imani yao kwako, matumaini yao dhidi yako yataweza kukuinua tena juu na kukufanya uendelee na safari yako ya kimaisha (endelea kuangalia hiyo drama ndipo utakapogundua nilichomaanisha)
wakorea wanavyo tuchukulia Waafrika........
najua waafrika tuna matatizo yasiohesabika ndani ya bara letu yanayosababishwa zaidi na ukosefu wa elimu ya utambuzi (kujitambua) kuanzia kwa raia wa kawaida kama mimi hadi viongozi wetu wakubwa tuliowapa mamlaka makubwa ya kutulinda na kuzisimamia rasilimali zetu zinazohamishika na zisizohamishika, bahati mbaya elimu hii ya utambuzi haipatikani ndani ya chumba cha darasa kwa sababu wapo waafrika waliobahatika kuwa na elimu kubwa sana ya darasani lakini matendo yao na utu wao ukizidiwa kwa kiwango kikubwa sana na wengineo wakiwemo hao waliokimbia darasani
kupitia drama hii nimeendelea kutofurahishwa na tabia hii ya kuendelea kutuchukulia waafrika wote ni watu dhaifu mno kwa kila jambo (na huu ugonjwa si mara ya kwanza kuushuhudia kupitia vipindi vya wakorea nilivyobahatika kuviangalia), mara nyingi sana wanapoizungumzia Afrika huoainisha kama ni sehemu moja yote (yenye matatizo, yenye watu wasiojielewa, wapenda vita, wasioweza kuishi bila ya kupatiwa msaada, sehemu ambayo ukitembelea lazima usafiri na choo chako na maji ya kujisafishia) jambo ambalo si sahihi kwa mtazamo wangu kwa sababu afrika si muunganiko wa nchi moja na pia hatufanani kiutamaduni, kiuchumi na hata kimatatizo licha ya kwamba tunatokea bara moja hivyo basi si sahihi kutuhukumu sote kama ni species tegemezi isiyo na faida yeyote.........
Wanapoandaa project zao basi ingelipendeza zaidi kama wangelibase zaidi na eneo maalum na si kutuangushia mzigo waafrika wote
kama wanashindwa kufanya hivyo basi watengeneze japo eneo la kubuni pindi wanapotengeza project zao kama walivyofanya descendent of the sun drama (walibuni eneo lisilo rasmi kwenye dunia yetu linaloitwa Urk ambalo tulishuhudia lead actors wakiongozwa na song hye kyo wakienda kujitolea kutoa huduma za kiafya)
Halafu hizi nchi zilizoendelea kama zinaongozwa na nia ya kweli ya kutaka kutusaidia sisi waafrika tusiojielewa (kama wanavyotuchukulia wengi wao) basi zipo njia njema zaidi ya hii ya kujitolea kutoa huduma husika kama za kiafya, elimu au tafiti (voluntary works) kwa muda maalumu
Haya matendo wanayoyafanya hayana utofauti wowote na yale yanayotekelezwa na wazee waliojaalia kipato cha fedha (utamkuta mzee anampa mwanawe kiwango cha fedha taslimu kila baada ya muda, au mwengine anampa credit card) wakati alikuwa na uwezo wa kumpa nyenzo mtoto wake zitakazomuwezesha kujiongoza mwenyewe kupata pato lake la halali ili kuepukana na utegemezi na si kusubiria kila siku suruali ya mzee itanuke.
kwa mfano wanatupa huduma za kiafya kama madawa na hata wataalamu kwa muda maalumu, misaada ya kifedha, wanatuletea walimu wanatufundisha kwa muda maalum, wanatuletea wataalamu kupitia sekta nyenginezo na wao pia kwa muda maalumu n.k
kivyovyote kwa mfumo huu sisi waafrika tutaendelea kuwa wategemezi kwao (Ingelipendeza zaidi kama wangelikuja kuwekeza moja moja huku kupitia sekta zote muhimu wakiongozwa na moyo safi wenye kuambatana na uadilifu wa kutufunza ili kupeukana na utegemezi pamoja na kuheshimu rasilimali zetu zilizopo na si kutuonjesha keki zao kwa muda mfupi then wanakimbia (msaada wa muda mfupi hauwezi kuondoa tatizo sugu)
kwa mfano hawa mabwana kama wanatupenda kweli basi waje japo kutumia ardhi yetu kwa ajili ya film location, tumejaaliwa mito, maziwa, misitu ya kuigiza hata filamu za kivita, Mungu ametupa zawadi ya milima (basi wawatumie celebrities wao kutangaza utalii ili kigwangwala apumzike kulialia twitter, pia tumejaaliwa hoteli na visiwa vilivyojaaliwa mandhari nzuri hata kwa wanandoa wanaohitaji kupumzika (wasiishie kwenda jeju, japan, Bali indonesia, america) bila ya kusahau population ya vijana waliotayari kufanya kazi kwa bidii kwenye mazingira yeyote ilimradi wapate gawio linaloendana na matumizi ya nguvu zao ..........
kwa kuwa serikali zetu ni sikivu basi naamini suala la kodi linaweza kuzungumzika na kupatiwa ufumbuzi wenye kunufaisha pande zote mbili
Kudos to all volunteers who sacrifice themselves and their families for the good of humanity
favorite couple: Yeon Da Yeon + Park Jae Hyung

Woo Do Hwan Shows Off Duality By Portraying 2 Contrasting Characters In “The King: Eternal Monarch”
Woo Do Hwan portrays Jo Young, chief imperial bodyguard and Emperor Lee Gon’s best friend, as well as Jo Eun Seob, a public service worker at the National Police Agency’s civil service office.
Woo Do Hwan commented, “It’s difficult because it’s my first time portraying two characters, but I’m having fun filming.”
View attachment 1420332
Palipo na mashindano pana Majivuno, ila penye maelewano pana Maarifa.zipo baadhi ya vita unaweza kushinda kwa kurudisha nyuma jeshi lako, hivyo basi hakuna ulazima wa kuendeleza mapambano yasiohitajika kama alivyopendekeza muheshimiwa hapo juu.
nyote ni washindi
Hata kwenye ITAEWON CLASS napo kuna ubaguzi wa Rangi (mtu mweusi) ambao ulinikera nikajitahidi tu kuimalizia mule kuna jamaa flani black alikuwa anabaguliwa mpaka unamwonea huruma sijui nani alimwambia akajichomeke mule ku act Daaaah pamoja nakuwa walionyesha kumtetea wengine lakini bado utaskia kauli "sawa we mkorea Lakini kwetu hatunaga Mkorea Mweusi we Rudi kwenu tu Guinea" Yanipaka nahisi kuacha kizipenda hizi series Dah.
Sent using Jamii Forums mobile app
K-news reported that "The King" already got back the production fee by selling the rights. The profit is over 30%.
============================
A son of Davao, Jack Cruz is a professional stylist for 10 years now who frequents fashion weeks, A list photoshoots and brand campaigns outside the Philippines. Currently, in Korea, Jack never thought that he would add styling for several TV series in his already colorful journey in the fashion industry.
Jack Cruz styled this iconic outfit of Lee Min Ho on horseback, which fans went crazy fo
When asked about what it's like to work with the cast, Jack shares that they all have been very encouraging towards him. He even mentions a particular moment when Lee Min Ho backed up his idea:
"The whole cast was amazing and they were very supportive of what I let them wear—no complaints whatsoever. There was a picture that kinda went viral, the one with Lee Min Ho was riding a horse.
Originally, he was supposed to wear an equestrian hat because the director really wanted him to wear one, although I was totally opposing it (there was a bit of commotion onset) because I envisioned LMH on that horse with matching wind blowing through his hair (swoon moment). I won that argument because LMH took my side. Minutes after, the photo went viral and fans liked it."
matarajio ya hiyo drama kufanya vizuri ni makubwa sana si tu kwa sababu ya uwepo wa Lee Min Ho bali pia kuna nguvu kubwa ya muandishi kim eun seok, project zake zote zilizopita zimefanya vizuri sana.
inawezekana hiyo project ikawa ni mbaya kwetu sisi mashabiki ila sidhani kama italeta athari kubwa sana kwa makampuni yaliofanya uwekezaji kuanzia media ya (SBS) na wazalishaji wakuu (Hwa & Dam Pictures) naamini watatengeneza faida kubwa sana.
ngoja tuone kitakachojiri kuanzia leo.
Drama nyengine alizoandika kim eun sook ni pamoja na:
- Mr sunshine
- the descendant of the sun
- goblin
- the heirs
- gentleman dignity
- secret garden
- n.k
View attachment 1421429
Tatizo jamii ya weusi inataka kujichomeka kila kona. Itaewon sikutaka kuiangalia ila machungu ya kuifuta bila kuiangalia ikanibidi niangalie. Jamaa alinishangaza halafu story yake wala haikua na mashiko.
The King eternal monarch nimeanza kwenda nayo sambamba episode ya kwanza. Who is with me[emoji39][emoji39]