Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Msaada jamani siku hz nashindwa kupakua series kupitia drama nice au dramacool ilihali zamani nilikuwa naweza kama kawaida ,,,,sielewi tatizo nn shida ina anzia kwenye kidude kilichochini upande wa kulia kile cha Ku download ia uki click kinaleta vitu havielewekeki ..msaada jamani bila shaka wazoefu mmenielewa
 
eti mfalme,
muda mrefu nimeshindwa kukuona mitaa yako ya kujidai, au ndio maandalizi ya ubingwa wa premier league,
sitaki jezi ya liverpool, naomba uninunulie jezi ya yanga, baadae nitamtumia aminas a.k.a mshabiki wa zamani wa UD songo ya msumbiji
Si unajua parade yetu huwa inatisha sana japo Corona haijatutendea haki maana sina hakika kama parade itakuwepo hususan kipindi hiki
 
Tatizo hapo itakua ni tangazo.

Ukigoogle chagua ile dramacool.movie ukishindwa jaribu kutumia kissiassian.
Msaada jamani siku hz nashindwa kupakua series kupitia drama nice au dramacool ilihali zamani nilikuwa naweza kama kawaida ,,,,sielewi tatizo nn shida ina anzia kwenye kidude kilichochini upande wa kulia kile cha Ku download ia uki click kinaleta vitu havielewekeki ..msaada jamani bila shaka wazoefu mmenielewa
Pia jaribu browser mbali mbali mfano anka browser
 
umegundua kitu gani?
kiupande wangu nimeiona sura ya mwanaume yenye kufanana na lee min ho na si sura ya mwanamke yenye kufanana na kim go eun.

Parallel world and time travel?
ukiangalia kwa umakini tukio la uokoaji liliofanywa na mwanadamu aliyevaa mask unagundua ya kwamba alikuwa na uelewa mkubwa sana wa eneolililotokezea mauaji ya mfalme (kiuhalisia kwa ambaye ni mgeni ingelimuwia vigumu sana kuifahamu ikulu kiundani) na jengine zaidi kwenye lile tukio alikuwa akimtafuta sana lee rim ili amuue.

Muandishi ametuaminisha ya kwamba aliyemuokoa lee gon ni mwanamke kwa sababu ya ushahidi wa kitambulisho chenye jina la Jung Tae Eul lakini ukiliangalia lile tukio kwa umakini unagundua ya kwamba aliyemuokoa lee gon mdogo ni mwamamme anayefanana na lee gon wa baadae (Lee min ho), ina maana lee gon amejiokoa mwenyewe...

ukirudi kuliangalia tena lile tukio kuna wakati muokoaji aliushikilia mwili wa adui kwa lengo la kujikinga dhidi ya silaha, laiti kama muokoaji angelikuwa ni mwanadada Jung Tae eul basi kivyovyote kwa umbile lake asingeliweza kujikinga na risasi zitakazopigwa juu kwa sababu ni mfupi ndio maana najiaminisha yule muokoaji ni mwanaume anayefanana na lee min ho mwenyewe.

  • je huyu mwanadamu aliyefanana lee gon ni yupi na anatokea wapi?
  • je ni yule bwana mdogo aliyepo jamhuri ya korea?
  • je lee gon amesafri na muda (nikimaanisha lee gon mkubwa amejiokoa mwenyewe dhidi ya kifo chake akiwa mdogo na kama ni hivyo ametumia power gani), tukumbuke lile tukio limetokezea mwaka 1991.
  • je kuna uwezekano wa uwepo wa third parallel world?

View attachment 1425890
View attachment 1425891

hii sura ni ya lee min ho mwenyewe kwa uzoefu wangu wa kuangalia drama....sijui wenzangu mumegundua jambo gani?
au wenzangu ndio mumeingia kwenye mtego wa muandishi?
teh teh teh
Mkuu we kiboko leo nimeangalia ep ya 13 aisee aliyejiokoa ni lee Gon mwenyewe.Watu mnafatilia mambo.Supa sana mkuu.
 
My best drama for this year so far ni hospital playlist... Huyo mama writer na director wake wanajua kucheza na hisia
kwa atakayejaaliwa uhai hospital playlist season 2 huenda itarudi mwaka 2021, muda huu nimesoma mahojiano ya mwanadada jeon do mi anasema kuna uwezekano wa shooting kuanza tena mwezi November.

nawakilisha team ikjun na Song hwa
bila ya kusahau Chairman Ju Jung Su na Madame Rosa
sijui episode 12 imeishiaje


hawa wakorea makeup zao ni balaa, huyu binti anakaribia miaka 40 lakini sura yake kama mtoto wa kidato cha 4...
sasa umkute mwanamke wa buza ameweka makeup.......mama weeee uso manjanoo kama amepaka unga wa dengu na binzari ya kupikia kachori za bifatuma kibuno

hii project ya hospital playlist imezidi kumuongezea umaarufu huyo binti,
  • pia ni televisheni project yake ya kwanza kushiriki kama muigizaji mkuu​
  • ni televisheni project yake ya pili kushiriki baada ya mother drama (alikuwa part ya waigizaji wengineo)​
  • amebeba tuzo za best actress takribani mara mbili kwenye upande wa musical actress and theaters.​



========================
sina uhakika ila huenda sanaa ya musical and theaters pia inalipa sana huko kwa wenzetu kama utakuwa una fanbase kubwa sana, waimbaji wengi wa kpop wanaperform kwenye musical, hata baadhi ya waigizaji wa drama baadhi yao wamejikita sana upande huo (mfano cho seung woo ana project nyingi sana eneo hilo) na wengineo pia walianzia huko (mfano ji chang wook).

nimeona hata song il kook project zake nyingi miaka ya karibuni zimeegemea upande huo wa musical (live performance),ndoto yake ya muda mrefu naye ilikuwa ni kuigiza na kuimba theaters)
  • I am you
  • Broadway 42nd Street :2018
  • god of carnage
  • Broadway 42nd Street:2020 kwa mara nyengine tena
View attachment 1463953
 
Tatizo hapo itakua ni tangazo.

Ukigoogle chagua ile dramacool.movie ukishindwa jaribu kutumia kissiassian.

Pia jaribu browser mbali mbali mfano anka browser
Hiyo anka browser inapatikana wapi play store ama maana hizo zingine zinaleta maluwaluwa yaleyale
 
Hivi hawa writers wa hizi kdramas wanakua na theme ya kutungia drama kila mwaka au?

Kwa mfano sasa hivi nmeona drama
nyingi zimejikita kwenye psychiatry/mental health,kuna

-dinner mate
-fix u
-Team buldog
-Nmeona na Kim soo Hyun anakuja na drama ya hivi hivi (its okay not to be okay)
-find me in your memory
-Born again
-sweet munchies

Au ni coincidence tu???
 
eti mfalme,
muda mrefu nimeshindwa kukuona mitaa yako ya kujidai, au ndio maandalizi ya ubingwa wa premier league,
sitaki jezi ya liverpool, naomba uninunulie jezi ya yanga, baadae nitamtumia aminas a.k.a mshabiki wa zamani wa UD songo ya msumbiji
Ni Bora Unipe Ya UD Kuliko Ya Yanga.

Bogoshipseyo Chingu.

IDD MUBARAK.
 
Nimeiokota playstore.

Nyingine kama zipi mkuu?maana mie huwa natumia uc mini saiv nimeanza na hii anka zipo vizuri tu
Jamani tatizo nn ,,,nmetumia hiyo anka still nikitaka Ku download naletewa matangazo.....yaaan baada ya step hiyo chini then Niki click naletewa cha kwenye picha ya pili .....
Screenshot_20200531-230600.jpg
Screenshot_20200531-230543.jpg
 
Aah kumbe ni hii. Hii huwa lazima kuipitia kwa hapo dramanice na dramacool ila kissassian haipo hio. Bonyeza hapo am not a robot kisha fata step za kubonyeza picha watakazo kama ni ya gari au reli etc ukifika mpaka mwisho inaondoka.
Jamani tatizo nn ,,,nmetumia hiyo anka still nikitaka Ku download naletewa matangazo.....yaaan baada ya step hiyo chini then Niki click naletewa cha kwenye picha ya pili .....View attachment 1465049View attachment 1465052
 
Back
Top Bottom