Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

FB_IMG_1602347235543.jpg

shikamoo Wahenga wa Taifa letu Gogryeo
 
The Gentlemen of Wolgyesu Tailor Shop drama:

lee man sool na falsafa yake:
kwenye hii drama vazi la suit limetumika kama ni alama ya utambulisho wa heshima, nidhamu, haiba yenye kuambatana na Ihsani pamoja na msimamo imara wa mwanaume kwenye kuitafuta furaha ya maisha yake ya kila siku.
mzee lee man sool ametufikishia falsafa hii ya kuitafuta furaha ya nafsi kwa njia ya ushoni (si lazima tumuige mzee lee man sool njia yake bali kina mtu anapaswa abuni au aitafute njia yake itakayompatia furaha ya nafsi pasina kuvunja misingi ya kimaadili hususani ya ubindamu)

msuguano wa kifikra (digital vs analog):
Dong-Jin aliamini tailorshop ni biashara isiopaswa kuendelezwa tena na familia baada ya kudumu kwa takribani miaka 100 (aliamini ya kwamba imeshapitwa na wakati (nani atakayeshona suti kwa fundi makoleo haliyakuwa maduka ya kununulia suti yamejaa tele).....uzuri hii drama iliendelea kutuonyesha the nostalgic and wistful charms ya biashara hii ya ushoni ilioudumu kwa takribani miaka 100. Ndipo hapo tunapopaswa kujiuliza swali
kwenye ulimwengu huu wa digital (modernity), is tradition still relevant?

The bespoke suit (suit za kutengeneza kwa mkono) ni alama kuu ya analog iliotumika humu ndani inayounganisha dhamira kuu ya kuitafuta furaha ya nafsi kupitia njia ya utamaduni zaidi kuliko njia ya kisasa (binadamu anatengeneza suit na suit inamtengeneza mwanadamu mwenye heshima, mwenye kuheshimu muda, mtiifu na mwenye huruma kwa wenzake bila ya kuangalia ni kwa kiwango gani cha mali kinachopatikana kupitia kazi ya mikono na jasho lake). The bespoke suit ni alama kuu ya analog (kumbe bado kuna umuhimu wa kuvithamini vya zamani)

Lee man sool na ukumbusho bora kwa mwanawe (lee dong jin):
ukiangalia mtiririko mzima wa maisha ya Dong jin tulioonyeshwa kwa takribani episode 54 za drama hii yamefupishwa kwenye nukuu hii ya baba yake.

ukubwa wa pua si wingi wa kamasi
meesa company (chaebol) na laurel tailor shop (wolgyesu tailor shop) wote ni wazalishaji wa suti ila wana tofautiana kwenye filosophy nzima ya uzalishaji na mauzo ya bidhaa hiyo na hapo ndipo unapozaliwa mgongano wa kimaslahi na kiutu ndani ya drama.
meesa corporation kwa upande wao suti ni kazi ya sanaa, laurel shop kwa upande wao suti ni kazi inayohitaji ubunifu( ubunifu ndio huzalisa form of art).

Hyo sang hakuwawekea heshima kubwa wolgyesu(aliamini biashara yao itabaki kwenye ule ule wa Mom-and-pop stores).
hata leo hii nje ya drama mabadiliko ya teknolojia na utandawazi yamepelekea anguko kubwa sana kwa biashara ndogo zinazoendeshwa kwa msingi wa familia jambo amabalo pia limeleta athari kuu ya utengano wa kimatabaka, msingi mkuu wa mgawanyiko huu wa matabaka umechangiwa zaidi na kule kutofautiana kwa falsafa za uendeshaji wa biashara kati ya corporation na Mom-and-pop stores kwa kuanzia uzalishazi, usambazaji hadi mauzo ya bidhaa.

in reality it may seem that washonaji nguo kwa njia ya mkono na wale wazalishaji wakuu kupitia mashirika makubwa kwa sasa wanategemea masoko tofauti hii ni kwa sababu mashirika au kampuni kubwa zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuwaibia wateja washonaji wadogo kwa miaka ya karibuni (leo hii ni wachache sana wanaokimbilia kwa mafundi kwa lengo la kutengeneza nguo ukilinganisha na wale wanaokwenda kwenye malls tofauti kununua moja kwa moja)

mwenye nguvu hapishwi bila ya kuandaa mikakati, sera na mbinu za kupambana naye
nimevutiwa na idea aliyokuja nayo dong jin ya kuwaunganisha washonaji wadogo (kwa kuanzisha ushirika) hususani kwa waliokuwa bado hawajamezwa na nguvu mpya ya uwekezaji(lengo ni kuwawezesha kuendelea na biashara zao bila ya khofu ya kupoteza wateja, kuendelea kuwepo kwa wateja wa uhakika ndio muendelezo wa familia zako kupata mahitaji yao ya msingi)

ko family craziness.
teh teh teh nimejikuta naikumbuka sauti ya marehemu kim young ae (ametumia uhusika wa choi gok ji humu ndani)pindi anapomwita mrs koo. episode mbili za mwisho pia zilifocus zaidi upande wa familia ya ko katika harakati zao kuyatafuta maridhiano, kilichonifurahisha zaidi ni kushuhudia kila muhusika getting redeemed kwa njia ilio sahihi na ya amani zaidi hatimaye baada ya vimbwanga vilivyodumu kwa takrabani episode 50 hatimaye familia ikawa ni kitu kimoja.
==========================

laurel tailor shop drama = marks 7.4/10
marry me now drama bado imebaki kuwa ni family drama bora kiupande wangu.
kinachofuata ni kuimaliza father is strange drama
Usisahau unnie is alive nayo ni nzuri pia
 
Currently naangalia Kill me heal me, Backstreet rookie, The royal Gambler na Strong woman Do Bong Soon.

Top 3 ya drama ninazozikubali:
1. Empress Ki, hii ni moja kati ya drama niliyoangalia mwanzo hadi mwisho bila kupepesa macho sababu ya kuwa na mpangalio mzuri wa matukio. Pia characters wamevaa uhusika vizuri sana kiufupi wamezitendea haki nafasi walizocheza wakiongozwa na bi dada Ha ji won pamoja na mtaalamu Ji Chang Wook bila kumsahau mtaalam Wang Yu. Hii hata niirudie mara 100 siwezi ichoka.

2. The land of the wind/ The Kingdom of the wind. Hii ilikua all time favourite drama yangu kabla ya kuangalia Empress Ki. Pia hii ni drama yangu ya pili kuitazama ya kwanza ni Jumong na ndio iliyopelekea mimi kuwa mlevi wa hii burudani adhimu ya wakorea. Kwenye hii drama nimependa jinsi walivyoonesha maisha ya mwanzoni kabisa ya nguli Daemusin Muhyul wa Goguryeo pamoja na mtoto wake Yuri. Hii naikubali zaidi hata ya Jumong yaani kwenye hii drama Song il guk alitisha.

3. Hotel Del luna. Hii nimeimaliza wiki moja iliyopita. Binafsi mimi ni mpenzi wa movies, series na drama za adventure, fantasy au thriller pia napenda drama zenye story yenye kuumiza kichwa kama Kill me heal me na King Eternal Monarch.

Kwenye hii drama kilichonivutia zaidi ni story yake inayomuelezea bi dada Manweol mmiliki wa guest house of the moon na tragedy iliotokea hapo zamani kati yake na Chung Myung iliyopelekea yeye kuwa tied down kwenye Guest house of the moon kwa takribami miaka 1000. Ndani ya hii drama utamuona mtaalam Ku Chan Song pamoja na wa wafanyakazi wengine wa Guest house of the moon. Pia plot twist kati ya Chung Myung na Manweol ilinivutia zaidi pia ilinisikitisha but all in all nilipenda jinsi ilivoisha japo hawakumtendea haki Chung Myung ila ilikua na happy ending.

Kingine OST zake murua kama "Can you see my heart" ya Heinze pamoja na "Done for me" ya Punch...hizi ziliinogesha zaidi hii drama...Hawa wakorea wanajua sana kwenye uandishi wa hizi drama zao sijui lini wabongo tutafikia level hizi.

Honourable mentions: Hapa zinaingia Jumong, Kill me heal me, Queen Seondeok,Iris I,Arthdal Chronicles, Iljmae na Goblin.

Pia honourable mention iende kwa Mr Sunshine...katika drama zote nilizowahi angalia zenye sad ending hii ni ya pili ya kwanza ni Empress Ki. Hizi drama mbili zilijua kunisikitisha aisee.

Hio ndio list ya drama za kikorea nilizoangalia mpaka sasa na nikazikubali zaidi.
 
Hatimaye nimemaliza The Gentlemen of Wolgyesu Tailor Shop. Namshukuru Hyo Won ametuthibitishia kuwa si kila last born ni spoiled brat....
Mtu mwingine niliyempenda sana ni Su Nyeo... Yaani huyu ni malkia wa nguvu, mwanamke na nusu.
Kusema kweli kwenye hii drama hakuna character niliyemchukia aisee kila mtu alinifurahisha kwa sehemu yake.
Na mimi nimejichagulia familia pale naitwa Lee Dong Joo[emoji13][emoji13][emoji13]
 
Family drama nyingine karibu

Fathet is strange

Father I'll take care of you
Hatimaye nimemaliza The Gentlemen of Wolgyesu Tailor Shop. Namshukuru Hyo Won ametuthibitishia kuwa si kila last born ni spoiled brat....
Mtu mwingine niliyempenda sana ni Su Nyeo... Yaani huyu ni malkia wa nguvu, mwanamke na nusu.
Kusema kweli kwenye hii drama hakuna character niliyemchukia aisee kila mtu alinifurahisha kwa sehemu yake.
Na mimi nimejichagulia familia pale naitwa Lee Dong Joo[emoji13][emoji13][emoji13]
 
Dong yi imesifiwa hapo juu iangalie pia kuongeza idadi kwa list ya korean drama nzuri unaweza shusha na flower in prison pia
Currently naangalia Kill me heal me, Backstreet rookie, The royal Gambler na Strong woman Do Bong Soon.

Top 3 ya drama ninazozikubali:
1. Empress Ki, hii ni moja kati ya drama niliyoangalia mwanzo hadi mwisho bila kupepesa macho sababu ya kuwa na mpangalio mzuri wa matukio. Pia characters wamevaa uhusika vizuri sana kiufupi wamezitendea haki nafasi walizocheza wakiongozwa na bi dada Ha ji won pamoja na mtaalamu Ji Chang Wook bila kumsahau mtaalam Wang Yu. Hii hata niirudie mara 100 siwezi ichoka.

2. The land of the wind/ The Kingdom of the wind. Hii ilikua all time favourite drama yangu kabla ya kuangalia Empress Ki. Pia hii ni drama yangu ya pili kuitazama ya kwanza ni Jumong na ndio iliyopelekea mimi kuwa mlevi wa hii burudani adhimu ya wakorea. Kwenye hii drama nimependa jinsi walivyoonesha maisha ya mwanzoni kabisa ya nguli Daemusin Muhyul wa Goguryeo pamoja na baba yake Yuri. Hii naikubali zaidi hata ya Jumong yaani kwenye hii drama Song il guk alitisha.

3. Hotel Del luna. Hii nimeimaliza wiki moja iliyopita. Binafsi mimi ni mpenzi wa movies, series na drama za adventure, fantasy au thriller pia napenda drama zenye story yenye kuumiza kichwa kama Kill me heal me na King Eternal Monarch.

Kwenye hii drama kilichonivutia zaidi ni story yake inayomuelezea bi dada Manweol mmiliki wa guest house of the moon na tragedy iliotokea hapo zamani kati yake na Chung Myung iliyopelekea yeye kuwa tied down kwenye Guest house of the moon kwa takribami miaka 1000. Ndani ya hii drama utamuona mtaalam Ku Chan Song pamoja na wa wafanyakazi wengine wa Guest house of the moon. Pia plot twist kati ya Chung Myung na Manweol ilinivutia zaidi pia ilinisikitisha but all in all nilipenda jinsi ilivoisha japo hawakumtendea haki Chung Myung ila ilikua na happy ending.

Kingine OST zake murua kama "Can you see my heart" ya Heinze pamoja na "Done for me" ya Punch...hizi ziliinogesha zaidi hii drama...Hawa wakorea wanajua sana kwenye uandishi wa hizi drama zao sijui lini wabongo tutafikia level hizi.

Honourable mentions: Hapa zinaingia Jumong, Kill me heal me, Queen Seondeok,Iris I,Arthdal Chronicles, Iljmae na Goblin.

Pia honourable mention iende kwa Mr Sunshine...katika drama zote nilizowahi angalia zenye sad ending hii ni ya pili ya kwanza ni Empress Ki. Hizi drama mbili zilijua kunisikitisha aisee.

Hio ndio list ya drama za kikorea nilizoangalia mpaka sasa na nikazikubali zaidi.
 
Kuna halotel 1500 unlimited(usiku pack)

Kuna toboa night airtel gb 10 sh 1500

Voda kama una laini ya chuo gb 2.5 kwa sh 1000 night pack

Chaguo lako tu hapo na kasi ya mtandao eneo ulilopo
Ooh ahsante sasa hivi ngoja nipumzike kwanza, hivi wenzangu huwa mnatumia bando la mtandao gani kupakua maana mmmh
 
Currently naangalia Kill me heal me, Backstreet rookie, The royal Gambler na Strong woman Do Bong Soon.

Top 3 ya drama ninazozikubali:
1. Empress Ki, hii ni moja kati ya drama niliyoangalia mwanzo hadi mwisho bila kupepesa macho sababu ya kuwa na mpangalio mzuri wa matukio. Pia characters wamevaa uhusika vizuri sana kiufupi wamezitendea haki nafasi walizocheza wakiongozwa na bi dada Ha ji won pamoja na mtaalamu Ji Chang Wook bila kumsahau mtaalam Wang Yu. Hii hata niirudie mara 100 siwezi ichoka.

2. The land of the wind/ The Kingdom of the wind. Hii ilikua all time favourite drama yangu kabla ya kuangalia Empress Ki. Pia hii ni drama yangu ya pili kuitazama ya kwanza ni Jumong na ndio iliyopelekea mimi kuwa mlevi wa hii burudani adhimu ya wakorea. Kwenye hii drama nimependa jinsi walivyoonesha maisha ya mwanzoni kabisa ya nguli Daemusin Muhyul wa Goguryeo pamoja na baba yake Yuri. Hii naikubali zaidi hata ya Jumong yaani kwenye hii drama Song il guk alitisha.

3. Hotel Del luna. Hii nimeimaliza wiki moja iliyopita. Binafsi mimi ni mpenzi wa movies, series na drama za adventure, fantasy au thriller pia napenda drama zenye story yenye kuumiza kichwa kama Kill me heal me na King Eternal Monarch.

Kwenye hii drama kilichonivutia zaidi ni story yake inayomuelezea bi dada Manweol mmiliki wa guest house of the moon na tragedy iliotokea hapo zamani kati yake na Chung Myung iliyopelekea yeye kuwa tied down kwenye Guest house of the moon kwa takribami miaka 1000. Ndani ya hii drama utamuona mtaalam Ku Chan Song pamoja na wa wafanyakazi wengine wa Guest house of the moon. Pia plot twist kati ya Chung Myung na Manweol ilinivutia zaidi pia ilinisikitisha but all in all nilipenda jinsi ilivoisha japo hawakumtendea haki Chung Myung ila ilikua na happy ending.

Kingine OST zake murua kama "Can you see my heart" ya Heinze pamoja na "Done for me" ya Punch...hizi ziliinogesha zaidi hii drama...Hawa wakorea wanajua sana kwenye uandishi wa hizi drama zao sijui lini wabongo tutafikia level hizi.

Honourable mentions: Hapa zinaingia Jumong, Kill me heal me, Queen Seondeok,Iris I,Arthdal Chronicles, Iljmae na Goblin.

Pia honourable mention iende kwa Mr Sunshine...katika drama zote nilizowahi angalia zenye sad ending hii ni ya pili ya kwanza ni Empress Ki. Hizi drama mbili zilijua kunisikitisha aisee.

Hio ndio list ya drama za kikorea nilizoangalia mpaka sasa na nikazikubali zaidi.
Daah, yani Kuna drama umeitaja hapo, niliinunua kwasababu ya kupenda kazi za mhusika mkuu kwenye kazi zake nyingine, Ila nilivyokuwa naitazama season one yote haikunifurahisha kabisa na sikuona sababu ya kuendelea na ya pili.Naizungumzia MR SUN SHINE, au ndo kusema uzuri wake ulianzia season two?
 
Back
Top Bottom