Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

The Gentlemen of Wolgyesu Tailor Shop drama:

lee man sool na falsafa yake:
kwenye hii drama vazi la suit limetumika kama ni alama ya utambulisho wa heshima, nidhamu, haiba yenye kuambatana na Ihsani pamoja na msimamo imara wa mwanaume kwenye kuitafuta furaha ya maisha yake ya kila siku.
mzee lee man sool ametufikishia falsafa hii ya kuitafuta furaha ya nafsi kwa njia ya ushoni (si lazima tumuige mzee lee man sool njia yake bali kina mtu anapaswa abuni au aitafute njia yake itakayompatia furaha ya nafsi pasina kuvunja misingi ya kimaadili hususani ya ubindamu)

msuguano wa kifikra (digital vs analog):
Dong-Jin aliamini tailorshop ni biashara isiopaswa kuendelezwa tena na familia baada ya kudumu kwa takribani miaka 100 (aliamini ya kwamba imeshapitwa na wakati (nani atakayeshona suti kwa fundi makoleo haliyakuwa maduka ya kununulia suti yamejaa tele).....uzuri hii drama iliendelea kutuonyesha the nostalgic and wistful charms ya biashara hii ya ushoni ilioudumu kwa takribani miaka 100. Ndipo hapo tunapopaswa kujiuliza swali
kwenye ulimwengu huu wa digital (modernity), is tradition still relevant?

The bespoke suit (suit za kutengeneza kwa mkono) ni alama kuu ya analog iliotumika humu ndani inayounganisha dhamira kuu ya kuitafuta furaha ya nafsi kupitia njia ya utamaduni zaidi kuliko njia ya kisasa (binadamu anatengeneza suit na suit inamtengeneza mwanadamu mwenye heshima, mwenye kuheshimu muda, mtiifu na mwenye huruma kwa wenzake bila ya kuangalia ni kwa kiwango gani cha mali kinachopatikana kupitia kazi ya mikono na jasho lake). The bespoke suit ni alama kuu ya analog (kumbe bado kuna umuhimu wa kuvithamini vya zamani)

Lee man sool na ukumbusho bora kwa mwanawe (lee dong jin):
ukiangalia mtiririko mzima wa maisha ya Dong jin tulioonyeshwa kwa takribani episode 54 za drama hii yamefupishwa kwenye nukuu hii ya baba yake.


ukubwa wa pua si wingi wa kamasi
meesa company (chaebol) na laurel tailor shop (wolgyesu tailor shop) wote ni wazalishaji wa suti ila wana tofautiana kwenye filosophy nzima ya uzalishaji na mauzo ya bidhaa hiyo na hapo ndipo unapozaliwa mgongano wa kimaslahi na kiutu ndani ya drama.
meesa corporation kwa upande wao suti ni kazi ya sanaa, laurel shop kwa upande wao suti ni kazi inayohitaji ubunifu( ubunifu ndio huzalisa form of art).

Hyo sang hakuwawekea heshima kubwa wolgyesu(aliamini biashara yao itabaki kwenye ule ule wa Mom-and-pop stores).
hata leo hii nje ya drama mabadiliko ya teknolojia na utandawazi yamepelekea anguko kubwa sana kwa biashara ndogo zinazoendeshwa kwa msingi wa familia jambo amabalo pia limeleta athari kuu ya utengano wa kimatabaka, msingi mkuu wa mgawanyiko huu wa matabaka umechangiwa zaidi na kule kutofautiana kwa falsafa za uendeshaji wa biashara kati ya corporation na Mom-and-pop stores kwa kuanzia uzalishazi, usambazaji hadi mauzo ya bidhaa.

in reality it may seem that washonaji nguo kwa njia ya mkono na wale wazalishaji wakuu kupitia mashirika makubwa kwa sasa wanategemea masoko tofauti hii ni kwa sababu mashirika au kampuni kubwa zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuwaibia wateja washonaji wadogo kwa miaka ya karibuni (leo hii ni wachache sana wanaokimbilia kwa mafundi kwa lengo la kutengeneza nguo ukilinganisha na wale wanaokwenda kwenye malls tofauti kununua moja kwa moja)

mwenye nguvu hapishwi bila ya kuandaa mikakati, sera na mbinu za kupambana naye
nimevutiwa na idea aliyokuja nayo dong jin ya kuwaunganisha washonaji wadogo (kwa kuanzisha ushirika) hususani kwa waliokuwa bado hawajamezwa na nguvu mpya ya uwekezaji(lengo ni kuwawezesha kuendelea na biashara zao bila ya khofu ya kupoteza wateja, kuendelea kuwepo kwa wateja wa uhakika ndio muendelezo wa familia zako kupata mahitaji yao ya msingi)

ko family craziness.
teh teh teh nimejikuta naikumbuka sauti ya marehemu kim young ae (ametumia uhusika wa choi gok ji humu ndani)pindi anapomwita mrs koo. episode mbili za mwisho pia zilifocus zaidi upande wa familia ya ko katika harakati zao kuyatafuta maridhiano, kilichonifurahisha zaidi ni kushuhudia kila muhusika getting redeemed kwa njia ilio sahihi na ya amani zaidi hatimaye baada ya vimbwanga vilivyodumu kwa takrabani episode 50 hatimaye familia ikawa ni kitu kimoja.
==========================

laurel tailor shop drama = marks 7.4/10
marry me now drama bado imebaki kuwa ni family drama bora kiupande wangu.
kinachofuata ni kuimaliza father is strange drama
Umeimalizia eeh? Mimi nimefika ep 44 nimeweka pause kwanza
 
niliamua kuingia vitani kwa siku 5 mfululizo
Ok good.. Usinimalizie uhondo[emoji16][emoji16]
Hadi hapa nilipofikia nimehitimisha hii drama ina couple nyingi kuliko drama zote nilizowahi kuzitazama halafu zote zipo on hakuna inayosinzia[emoji16][emoji16][emoji16]. Ila imenivutia zaidi couple ya Hyo Won na mwenzie....dogo ana energy ya kutosha
 
Ok good.. Usinimalizie uhondo[emoji16][emoji16]
Hadi hapa nilipofikia nimehitimisha hii drama ina couple nyingi kuliko drama zote nilizowahi kuzitazama halafu zote zipo on hakuna inayosinzia[emoji16][emoji16][emoji16]. Ila imenivutia zaidi couple ya Hyo Won na mwenzie....dogo ana energy ya kutosha
Capture.PNG

haya fanya umalize kiporo chako(tupo kwenye wiki ya mwanzo ya ndoa yetu) 🚶‍♂️ 🚶‍♂️ 🚶‍♂️ 🚶‍♂️ 🚶‍♂️
 
Gu family book
The moon embracing the sun
Flower in prison
Hwarang
The king in love
Moonlovers
Dong yi
Queen for seven days
Illjimae
Numbisa hebu nipe recommendation ya movie za kikorea zile za kiporipori niingie nazo mzigoni. Dae unaweza pia kusaidia Kama hautojali, Ile W-Two worlds ndo nimeimaliza Sasa hivi tu, ilikuwa nzuri. 🙏
 
Gu family book
The moon embracing the sun
Flower in prison
Hwarang
The king in love
Moonlovers
Dong yi
Queen for seven days
Illjimae
Moyo unanambia nianze na moja Kati ya The moon embracing the 🌞,au Flower in prison. Ungekuwa wewe ungeanza na ipi. Sorry,usichoke na maswali yangu mengi (Naogopa kuchoma MB)😃
 
Back
Top Bottom