baada ya kuimaliza The Gentlemen of Wolgyesu Tailor Shop hatimaye nimeigeukia DONG YI (nimechoka kusifiwa)
kama kawaida yake director lee byeong heon na style yake ya kututengenezea shujaa mwenye chembe chembe za uzembe
=============
ji jin hee
jamaa ana umbile zuri la kusimama uhusika wa mfalme, mpaka sasa nimeona waigizaji watatu wenye umbile zuri la kusimama uhusika wa mfalme nchini korea (hata mavazi yanawapendezesha zaidi)
- lee tae gon = king gwanggaeto (bonge la mtu)
- song il kook = jumong na kingdom of the wind (bonge la mtu, handsome zaidi)
- ji jin hee = bonge la mtu
navutiwa na uwezo wake wa kuigiza comedy anapokutana na dong yi (huwa nacheka sana, mfano walipokuwa wanatembea kitaani),
lakini
ananikera na ananikera zaidi kwenye screen za kimapenzi hususani zile za kuongea uso kwa uso na dong yi, jamaa amenyimwa body language fulani (huwa natamani niingie kwenye computer yangu nimtoe mpemba mimi)
nilipokuwa naangalia YI SAN nilikuwa na tatizo hili kutoka kwa muigizaji mkuu (muda mwingi lee seo jin alikuwa anacheka ovyo kama ameona sahani ya pilau la pichori pindi anapokutana na han ji min), alikuwa ananiboa mpaka nikaitupa ile drama.
=====================
sijui ni mapenzi au ni ugonjwa wa kupenda ujinga ndio ulionikumba, nimeshaangalia sana kazi za wakorea ila kwenye eneo hilo sijaona kama song il kook, jamaa yupo more comfortable, ana relax, goi goi wa kuzaliwa haswa na si wa kuigiza, akiongea utafikiri demu anamtongoza kweli (mwili wote unaongea, full burdani walllah)
hawa wengine wanakwama wapi?
wanaojitahidi kidogo labda kwa hawa vijana ni ji chang wook, kim soo hyun na lee min ho
=====================
mwenye bando lake
video 1: anza dakika ya 6 mpaka 8:27
video 2: anza dakika ya 2 (anapoongea na mopalmo)
achana na
emperor of the sea na kingdom of the wind, huko ndio balaa
ndio maana yule mpenzi wa
ARSENAL ni king'ang'anizi