Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Itafute drama inaitwa mask utafurahi kwa roho yako na utanishukuru binafsi najua taste za drama za Wanawake wanazopenda kama uliipenda Penthouse basi hiyo "mask" utaipenda pia.

Kabisa hiyo Vincenzo ni ya hovyo sana nimeangalia episode 1 tu haikunivutia nikaamua niachane nayo angalia hiyo "Mask" ni Kali Sana utanishukuru sana
Mask ya 2015? Nimeiona hiyo..ni nzuri
 
Kabisa na kwa mr queen kuna comedy hasa bifu ya queen na king bado queen na wakwe zake kisha queen na mpishi mkuu😂😂😂
Ina vi comedy sana nayo..nilichoona japo kwa kuchelewa ni kuwa wakorea wana great sense of humor..hata kwa series ya kawaida hutokosa kucheka hapa na pale [emoji1787]
 
Hatmaye Nimeimaliza "The Age of warriors", yenye episode 158. Hii series haikuwaelezea tawala za kijeshi kama ingeelzea zote basi tungekuwa Episode 300 na kuendelea.
Nadhani hakuna series nyingine yoyote iliyojawa na vipaji na masuperstar kuliko hii, toka nimeanza kuangalia Korean Drama, hii imevunja record ya kuwa na mastaa wengi na wenye vipaji vikubwa. Jambo la kufurahisha kwenye episode ya mwisho nipale baada ya msimulizi wa history anatupa summary ya kule tulipoanzia mpaka hapo mwisho, kisha anafanya Tathmini juu ya watawala wa kijeshi hao na Yi songgye( founder of Joeson) wanautofauti gani why walikuwa na uwezo wa kuwa Wafalme lakini waliiuacha ukoo wa Wang Madarakani kama puppet Kings wakati nguvu Mamlaka ilikuwa mikononi mwa Wanajeshi Hao, Lakini masomo tuliyopata kwenye historia ya watu hao. Kwahiyo niseme hii series ilipikwa kitaalam sana. Iliandaliwa na KBS.
List ya watawala wa Kijeshi(Goryeo )
1.Yi ui Bang (muda wa utawala miaka 5)
Aliuwawa na Jeong Jung Bu
2. Jeong Jung Bu (miaka 5), aliuwawa na Kyeong Dae Seung aliyekuwa na umri wa miaka 26.
3. Kyeong Dae Seung( miaka 4)
Alikufa kwa Maradhi baada ya kupewa sumu na mlinzi wake( Kim Ja kyuk) ambaye alikuwa Rafiki yake wa karibu. Baada ya kifo Chake Yi ui min ambaye alikuwa mlinzi wa Yi ui Bang ali - conquer Mji mkuu na kuchukua Madaraka.
4. Yi Ui Mini( miaka 13) aliuwawa na Choi cheong heon
5.Choi cheong heon(miaka 24) alirithisha madaraka kwa Mwanae( Choi woo)
Drama yetu( Age of warriors)iliishia kwa Choi Cheong heon.
6. Choi woo(miaka 30) alirithisha kwa mwanae Choi Hang
7. Choi hang( miaka 8) akarithi mwanae Choi Ui
8. Choi Ui(mwaka 1) akawauwawa na Kim Jun
9. Kim Jun( miaka 10) akauwawa na Im yeon ambaye alijiadaptisha kwa Kim Jun, na Kumuita Baba.
10. Im yeon(miaka 2) mtoto wake akarithi( Im yu mu
11. Im yu mu( mwaka 1) kisha akakonkwa na Mongol Dynasty ambayo muda wote ilikuwa na Vita dhidi ya Korea( Goryeo Dynasty)Tangu zama za Mwisho wa Utawala wa Choi Cheong heon. Hawa jamaa walipigana kwa miaka mingi hatmaye Goeyeo wakaenda chini ya Mongols and Yuen Dynasties.na ndio ulikuwa mwisho wa zama za utawala wa kijeshi. Miaka karibu 80 ilipopita ndipo General Choi Young na Yi Songgye walipoanza mapambano na Mongols na Yuan waliposhinda vita na kuikomboa Koryeo toka mikononi mwa wa wamongoli na wayuan.
View attachment 1809922
NOTE; Yi Songgye mwanzilishi wa Joseon Dynasty alikuwa ni zao la familia ya Yi In, ambaye alikuwa ni mdogo wa General Yi ui Bang. Huu ukoo wa kina Yi ui bang ulikuwa wa Mageneral, maana Baba yao pia alikuwa General, hata Yi Songgye kabla ya kuwa mfalme alikuwa ni General wa Goryeo.
Nampenda sana mwanae Yi Bang Won.Yaani ni genious na akiamua kitu lazima kitimie.But kwangu mm naonaga founder wa Joseon alikua Jeong Do Jeon Maarufu kama Sambong.General was just a first King.Ila bro umeelezea vizur mno
 
Inshaallah kitakachofuata baada ya hapo
  1. operation so ji sub
  2. operation ji sung
wote hao sikuwahi kuwapa heshima inayostahili kupitia kazi zao, nitailazimisha nafsi yangu izipende project za hao wanadamu bila ya kujali mwaka husika wa projects zao.
waswahili wana msemo wao "mtoto umleavyo ndivyo akuavyo"
Ji sung this man is awesome kama ukiona Kim So Roo,Kill me heal me na innocent deffendant he did wonderful work.
 
Unajua hili dude mwaka jana sikulifuatilia
nakumbuka niliishia episode za 90 baada ya archfield Yi Ui Mini kurudishwa mji mkuu na bwana mfalme
acha niangalie schedule itakavyokuwa nipate kushitua kiporo.
wale jamaa zake waliokuwa wanamtia ujinga alifufue taifa la shilla sijui waliishiaje.
wana mkakati wengine wanafurahisha sana,
unataka kuirudisha dola ya chagga ndani ya Tanzania inayochechemea
utapigwa mpaka uchakae
Unaambiwa Kwenye Revolt ya mwaka 1170 Yi Ui mini ndiye aliyeweka rokodi ya kuuwa watu wengi. Hata ile mishkaji yake Yi Ui Bang kina Yi Ko na Chewaon hawakumzidi Yi Ui Min, pamoja na ubabe wote waliokuwa nao. Yi ui mini walikuwa wakimuita The Killing Machine na wakati wa uongozi wa ulipelekea kuitwa the Prime minister of Devils.
Kina Master Dudul walikuwa wanampotosha.
 
na itakuwa series ndefu sana itakayobeba kwa mtiririko historia ya wafalme watano.
Nitafurahi sana kama watatuletea wanaume waliolelewa jeju, busan, pyeongyang ndio waziongoze hizo chronicles.
hawa waliozaliwa seoul watuache kwanza wenye jambo letu.
Hahaha Pyongyang Jiji la Nyumbani, kuna mengine kama Ansiseong, Gungneseong, Yodongseong, mokjeoseong, Gwanmmseong na zingine nyingi. Dah! Gogryeo nimepamiss sana.
Ukweli ni kwamba hata hawa Goryeo walikuwa si wazembe kama Joseon
 
Nampenda sana mwanae Yi Bang Won.Yaani ni genious na akiamua kitu lazima kitimie.But kwangu mm naonaga founder wa Joseon alikua Jeong Do Jeon Maarufu kama Sambong.General was just a first King.Ila bro umeelezea vizur mno
Yi Songgye anatajwa sababu ya kulinda hadhi ya Mfalme, ni sawa ilivyo kwa Goryeo aliyeanzisha ni King Gung Ye, kisa tu udikteta wake uliwafanya wanahistoria wamtenge, na heshima kapewa Wang Gun, ambaye aliongoza mapinduzi ya kumpindua Gung ye.
 
Ji sung this man is awesome kama ukiona Kim So Roo,Kill me heal me na innocent deffendant he did wonderful work.
Ji sung mara nyingi nimekuwa nikimuepuka ndio maana nimeamua kumweka tena kwenye list ya waigizaji nitakaoangalia project zao papo kwa papo. Project zake nilizoziangalia ni
  • swallow the sun drama
  • doctor john drama
  • innocent defendant drama
 
Back
Top Bottom