Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Asante
Huwa napita pita sana huko majukwaa mengine.
Si unajua kuzurura muhimu, waweza okota ๐Ÿฅญ chini ya mwarubaini....๐Ÿค“๐Ÿค“๐Ÿค“
Karibu sana madam ๐Ÿ˜๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜
 
Kazi mpya
Screenshot_20240416-162946.jpg
 
Love In Flames Of War[emoji440]

Episodes:43

Kwa wapenzi wa Cdrama I think hii ni kati ya zile Chinese Dramas nzuri sana nilizowahi kutazama muda wote.

Ni love story ya Xiao Beichen na Lian Hangjing ambao Baba zao ni makamanda wa jeshi na walikutana baada ya Hangjing kuwa adopted na Xiao family,mwanzo uhusiano wao ulikuwa mbovu kutokana na ukorofi na tabia za kitoto za Beichen.

Baada ya muda mrefu kupita na circumstances kadhaa wanakuja kuoana ila ndoa yao inapitia magumu kutokana na misunderstandings zinazotengenezwa na Zheng Fengqi mwanamke ambaye alikuwa anampenda Beichen ila kutokana na wivu na hasira za kumkosa anatumia kila njia kuwatenganisha huku akiwa nao karibu na hawajui kama ni adui yao.

Mbaya zaidi Fengqi anakuja kufanya unyama zaidi kusababisha ujauzito wa Hangjing kutoka wakati huo Beichen na Hangjing wamegeuka maadui kutokana na hila zinazotengenezwa ili kuwatenganisha,na baadae inakuja kusemekana Hangjing kafariki katika ajali ya moto na Fengqi akiwa nyuma ya hilo tukio,incident hii inafanya Beichen aishi na upweke na majonzi kwa miaka 5.

Mbaya zaidi furaha yao huwa haidumu hata walipokutana kwa mara nyingine unfortunately inaibuka vita baada ya uvamizi wa Japan katika Second Sino-Japanese war ambayo inamfanya Beichen kutumia nguvu kubwa kutengana na Hangjing ambaye kwa wakati huo ana ujauzito kwa kumsafirisha kwenda London kinyume na matakwa yake hadi hali itapotulia.

Beichen anaingia katika majukumu kama kamanda wa kikosi cha ulinzi kuhakikisha analinda taifa ila vita ilikuwa kali na ilikuwa ngumu kumshinda Mjapan huku akipoteza marafiki zake wote na yeye ikawa hajulikani kama yupo hai ama alifariki.

Baada ya miaka kama 6 Hangjing akiwa London anaona picha ya wanaharakati wapigania uhuru wa Kichina katika gazeti na Beichen akiwa kati yao kitu kinachoibua matumaini kwake maana aliishi muda wote huo akiwa na maumivu na huzuni,anaamua kufunga safari kurudi China kumtafuta Beichen.


Hii drama ina stress na maumivu kwa sana,vita imeibuka episodes 2 za mwisho but hizo stress zinasababishwa na love story ya Xiao Beichen & Lin Hangjing na waliyokuwa wanapitia tangu mwanzo wa drama.
Kwenye episode ya mwisho dk za mwishoni kuna hii part Hangjing alipomuona Beichen katika gazeti akaanza kulia na baada ya mwanae mdogo kumfuata kushangaa analia nini akamuonesha ile picha ktk gazeti na kuwambia kuwa huyu ndio Baba,hii part imefanya nielewe nini maana ya kushindwa kucontrol machozi[emoji1316][emoji38]

007ulRcHly1gfxcwg5b7cj31900u04qz.jpg
 
Back
Top Bottom