MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,185
- 24,055
Kwa hali jinsi ilivyo, sio rahisi kwa Mbunge wa Upinzani Bara ambaye ameshinda Ubunge wa Jimbo kwa vipindi viwili kushinda tena kipindi cha tatu katika Jimbo hilohilo.
Ukiangalia kwa sasa, majimbo ambayo wabunge wa upinzani wana wakati mgumu ni yale majimbo ambayo wamekuwa wabunge kwa vipindi viwili (Miaka 10) mfululizo.
Zitto Kabwe aliujua mchezo mapema ndio maana mwaka 2015 aliamua kubadilisha Jimbo na kwenda kugombea Jimbo jingine la Kigoma Ujiji. Mwaka 2005-2015 alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini.
Wabunge wa CHADEMA ambao wamekuwa wabunge wa Jimbo kwa miaka kumi mfululizo ni Godbless Lema, Halima Mdee, Freeman Mbowe, Peter Msigwa na Joseph Mbilinyi.
Tatizo ambalo linawaangusha wabunge wa upinzani ni hoja zinazowafanya wachaguliwe kuwa wabunge! Hili tatizo la hoja sio la wapinzani peke yake bali la wabunge kwa ujumla. Tofauti ya wabunge wa upinzani na chama tawala ni chama kuwa madarakani.
Unakuta mbunge anawaambia wapiga kura wakimchagua ataleta barabara, maji, hospitali, shule, ataongeza mzunguko wa pesa katika Jimbo, atatoa mikopo na mengine mengi ambayo kiuhalisia hutolewa na serikali.
Ahadi za Mbunge zinawafanya wananchi wamini Mbunge huleta barabara, maji, hospitali, shule, mzunguko wa pesa, mikopo. Wananchi wanapowachagua hawa wabunge hutegemea wataletewa walichokuwa wanaambiwa na mgombea.
Baada ya miaka mitano bila kutimiza ahadi, wapiga kura wanaweza kukubali sababu ambazo mbunge huzitoa lakini baada ya miaka 10 sio rahisi wananchi wakaendelea kukubali uwongo. Kwa maana nyingine, wabunge hujikaanga kwa ahadi zao wenyewe!
Ukichunguza kwa sasa wabunge hao niliowataja wana hali ngumu sana katika majimbo yao na kuna uwezekano mkubwa watajikaanga kwa ahadi zao wenyewe!