Kwanza lazima uelewe kuwa wapinzani wote wameshinda majimbo ambayo yalikuwa ya wabunge wa CCM.
Hoja zilizowafanya wapinzani kushinda hayo majimbo ni kuwaahidi wananchi wataleta kile ambacho wabunge wa CCM walishindwa kuleta (hospitali, barabara, maji, shule, nk).
Jiulize, kama Mbunge wa CCM ameshindwa kuleta vitu hivyo wakati serikali niya chama chake, huyo Mbunge wa upinzani atakuwa na ''magic'' gani ya kuweza kuishawishi serikali hiyo?
Kibaya zaidi, wanapoomba kura huwa hawasemi wataenda KUISHAWISHI serikali ILI ILETE bali husema WATALETA.
Nadhani unajua tofauti ya KUISHAWISHI serikali ili ILETE na KULETA.
Kuhusu kutafuta msaada kutoka nje, Nadhani unajua ni jukumu la serikali kisheria kujua hiyo msaada aliyopewa mbunge kuleta kwa wananchi ina manufaa kwa wananchi au la. Hata aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Makonda alileta vifaa vya mashuleni lakini serikali ikakataa kuviingiza bure kwa kisingizio kuwa vitatumika kwenye mashule ya serikali.
Sijui kwanini huelewi, tambua hoja hii; serikali iliyoshindwa kupeleka maendeleo kwa wananchi wake IMEFELI.
Tangu lini jukumu la kupeleka maendeleo kwa wananchi likawa la mbunge? kwanini unaficha udhaifu wa serikali ya Magufuli makusudi?
Wapinzani walitumia hoja hizo ulizoonesha hapo juu kwa sababu ndio ukweli, hilo ni jukumu la serikali, na hata kama wabunge waliokuwepo kabla walikuwa ni wa CCM,nao walifelishwa na serikali yao ya CCM, huu ni udhaifu wa serikali iliyopo na zilizokuwepo kabla, zote za CCM, usijaribu kuonesha udhaifu huo ni wa wabunge wa upinzani, hoja yako itakuwa ya uongo.
Makonda alishindwa kutoa maelezo, vipi Lema na Zitto nao walishindwa kutoa maelezo? na kama waliyatoa nani ataamini maamuzi na fair wakati refa ni msajili aliepewa kazi na Magufuli ili kuilinda CCM mpaka wanatunga sheria za ajabu kubana vyama pinzani?
Hebu nipe mfano wa mbunge wa CCM alieenda kutafutia wananchi wake misaada nje akaahidiwa kupewa, halafu serikali yake ya CCM ikamkatalia kwa yeye kushindwa kutoa maelezo?
Hizi ni siasa tupu.
Unapozungumzia suala la kuishawishi serikali ilete maendeleo unamaanisha nini? unataka wapinzani wakampigie magoti Magufuli kama anavyoonesha kila siku anavyopenda kusujudiwa?
Wacha siasa zako za kitapeli. Magufuli ana OBLIGATION ya kupeleka maendeleo majimboni kote bila kujali itikadi za vyama, not an OPTION kama mnavyolazimisha iwe, na kama hawezi aondoke ikulu kazi imemshinda. Ndio maana wapinzani husema WATALETA, coz wanajua hilo ni jukumu la serikali na sio kubembelezana kama Magufuli anavyotaka.
Kuhusu suala la serikali kutaka maelezo ya misaada wanayopewa wapinzani toka nje kuwa lipo kisheria, hizo ni mfano wa sheria kandamizi zilizopitwa na wakati, sio kila sheria ina manufaa kwa jamii; huwezi kuwa na sheria inayokataza wananchi wa eneo fulani wasipelekewe msaada wa maendeleo kisa umetoka nje, ni siasa tu zinazosababisha kukataa hiyo misaada kwa kuegemea kivuli cha sheria chakavu za kioga zilizopitishwa bungeni na wabunge wengi wa CCM kujilinda kisiasa.
Mfano mwingine wa hizo sheria kandamizi ni ile inayokataza vyama pinzani wasipate misaada toka kwa vyama rafiki vya nje, mpaka msajili apate maelezo.
Hii imetungwa makusudi ili CCM iendelee kufanya siasa bila ushindani kwasababu wao wana ruzuku kubwa, na bado wanakwapua toka sehemu nyingine, hivyo kusema kuna sheria inayotaka misaada toka nje ikaguliwe/kutolewa maelezo wao CCM wakipata misaada toka nje huwa wanatoa maelezo kwa nani? msajili anaweza kuwaadhibu CCM wakionekana kuvunja hizo sheria?