0_0
....
Kungine tumeanza kuzungumza ya 'uono na Ufikirifu Mifumo'; jambo hili kwa sasa tunalisema kama 'jambo la kubidi' ili kuikwamua jamii na 'ujuzi hafifu wa mawasiliano' na 'lugha za kuchanganyana' kwenye kuzungumzia masuala mbali mbali ya kijamii. Sanaa ya mawasiliano na umma, kati ya viongozi/watendaji wa jamii na umma, kwa siku za leo--miaka hii ya mwanzo muongo wa pili katika karne ya 21, yamegubikwa ukosefu wa umahiri ama/na kutokuwa na ukweli na uwazi katika ufafanuzi wa mambo yenye kuhitaji majibu -- pale penye swali.
. Mnadai watanzania Ni wachache nje kisa Ni lugha Siyo kweli. Watanzania hawapo nje wengi siyo kwa sababu ya Kiingereza. Wasomali wanawazidi watanzania walioko Marekani. Jee wasomali wapo wengi Marekani kwa kuwa wanajua Kiingereza? Hoja hapa ni kwamba Jee ni kweli haiwezekani kuwapatia...
www.jamiiforums.com
Kungine tumepata kuzungumza 'elimu elimu na elimu'; kwamba, jamii ya Watanzania ni yenye uhitaji wa elimu bora na ya viwango vya kuridhisha ili kukidhi sura ya mabadiliko na maendeleo yanayojitokeza kote duniani. Na basi, lilisemwa: Mzee Edward Lowasa, wakati mmoja alipokuwa akizindua kampeni yake ya kugombea nafasi ya kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, JMT, kipaumbele chake kwa serikali ilikuwa iwe ni ELIMU ELIMU ELIMU.... Sasa, >
tulimulika hili< kuwa haijalishi kwamba yeye hakufanikiwa kuwa Rais wa Tano wa JMT.... Lile alilolikamia kipindi kile, ni kama vile lilikuwa ni la kwake, lakini kuna namna fulani hili 'lipo tu mahala'... Kama halikudhahirika moja kwa moja kupitia jitihada zake, litapitia kwa wengine na hivi kuja kudhahirika.
Elimu ni jambo mtambuka katika kubaini 'uwezo' na 'vikomo vya kiutendaji' katika nyanja zote za ustaarabu na maendeleo ya watu. Tathmini kwa kheri ya shughuli ya elimu katika jamii inazingatia vigezo vya 'ukiasi' na pia 'hadhi' vifanyayo chachu ya ustawi wa wanajamii husika. Kama vile tulivyomulika kuhusu nukuu ya aliyekuwa Rais wa 44 wa Marekani, Barack Obama, wakati wa kampeni zake za kugombea urais kwa mara ya kwanza, >
khotuba alipokuwa Cooper Union huko New York, March 27, 2008<:
“...there was one thing that Jefferson and Hamilton agreed on: that economic growth depended upon the talent and ingenuity of American People; that in order to harness that talent, opportunity had to remain open to all; and that through education in particular, every American could climb the ladder of social and economic mobility and achieve the American dream. In the more than two centuries since then, we've struggled to balance the same forces that confronted Hamilton and Jefferson: Self interest and community, markets and democracy, the concentration of wealth and power and the necessity of transparency and opportunity for each and every citizen.”
"... kuna jambo moja ambalo Jefferson na Hamilton waliunga mkono: kwamba ukuaji wa uchumi unategemea talanta na ubunifu wa Wamarekani; kwamba ili kuvuna matunda ya hizo talanta, fursa haina budi kuwa wazi kwa wote; na kwamba kupitia hasa elimu, kila Mmarekani angaliweza kukwea ngazi ya ujongeaji wa kijamii na uchumi na kuifikia Ndoto Amerika. Katika kipindi cha zaidi ya karne mbili tangu hapo, tumekuwa kwenye harakati za kumizanisha nguvu zile zile ambazo Hamilton na Jefferson walikabiliana nazo: maslahi binafsi na jamii, masoko na demokrasia, 'kukoleza utajiri na nguvu' na 'ulazimu kwa uwazi na fursa kwa kila raia mmoja'."
Sasa hili la Rais Mstaafu Obama, litukumbushe kitu; Japo elimu imekuwepo huko Amerika kwa miaka mingi tangu kuzaliwa kwa nchi-taifa, mbona hili halijaleta ile suluhu hasa ya 'kumizanisha nguvu' kwa: 'maslahi-binafsi na jamii' ama 'masoko na demokrasia' ama pia ''kukolezea utajiri na nguvu' na 'ulazimu kwa uwazi na fursa kwa kila raia mmoja'?
Jambo hili, katika kule kujiuliza uliza na kujipatia majibu(urazini), ni lenye kushahibiana na fikra aliyekuwa Rais wa Kwanza wa JMT, Ndugu Kambarage Julius Nyerere, katika mkusanyiko wa mashauri yake yaliyotokana na hotuba na sanaa ya uandishi--kuwekwa katika kijichapisho kwa 'Introduction to Freedom and Unity (Utangulizi kwa Uhuru na Umoja)'.
...
Katika kijichapisho hichi cha 'Introduction to Freedom and Unity'; Mwalimu Nyerere alikuwa akiwasilisha mashauri juu ya dhana za 'Uhuru na Umoja' kama utangulizi kwa kuakisia na kuijenga Afrika katika misingi ya Ujamaa--Usoshalisti wa Kiafrika.
Usoshalisti wa Kiafrika ni jumuisho la mitazamo, fikra na mawaida juu ya sura ya maendeleo ya jamii ya watu wakiafrika kadri wanavyonasibika kahama kutoka kwenye ustawi na ustaarabu wao awali, na kuendea sura ya nchi-taifa lenye kuwa na demokrasia, maendeleo na utu. Kwa mujibu wa mtazamo na fikra za Mwalimu, jamii za Kiafrika zimekuwa na muktadha wa utaratibu wa kujiamulia mambo yake, uzalishaji na umiliki wa mali wa pamoja kulingana na mipangilio ya kimajukumu na ya kiwajibu katika kaya za zake za asili. Kwa hivyo Mwalimu, alikuwa akidadavua muktdha, kriteria, mtizamo na kukadiria mapana ya ustawi; na kutetea zile namna jamii za asili zilidumu pamoja katika umoja wa 'hali na mali'.
Kwa yeyote atakayepitia habari za kijitabu hicho, kwa hakika ataona ya kwamba Mwalimu, aghalabu nyuma miaka ya 1960+, alikuwa anadadavua masuala yale yale ambayo Obama aliyataja katika ile nukuu ya khotuba ya Cooper Union, mwaka 2008; ila tofauti ni kuwa Mwalimu alikuwa akidhamirisha muongozo wa kuepusha mawezekano ya kutokea kwa adha kama hizo tatu za Obama kwa pendekezo la Usoshalisti wa Kiafrika. Yumkini, ndiyo yawa pia ni kwa nini >
Obama alikuwa anaonekana kama ni Msoshalisti< aliyekuwa akitafuta kujificha katika mwamvuli wa 'ukuu wa katiba' na 'utumishi wa kiserikali' ili kuhakikisha kila Mmarekani anapata huduma za msingi na tena akija kama mtetezi wa jamii ya kawaida --ya walio wengi; kwa kutafuta kuwabana watu wa shughuli za 'Wall Street', New York, >ili >
utajiri wa kifedha na mitaji usihodhiwe na 'wajanja' wachache wasiojali tofauti na pengo kubwa kati ya 'wenye nacho' na 'wasionacho'<.
Nyerere aliona ipo shida kwenye kontrasti baina ya 'mifumo na desturi ya kaya za Kiafrika' na 'mifumo ya uchumi-misingi- fedha' kwa 'Afrika Mpya'. Kwake ilikuwa kana kwamba ni badiliko la kimifumo ya maisha lisiloepukika na hali laleta changamoto za 'kiuadilifu' na 'utendaji' katika miundo ya kiserikali na taasisi. Na hivi yeye aliandika hivi:
"This change is not just economic. By introducing the possibility of hoarding wealth through money, by encouraging the acquisitive instinct in man, and by basing social status on material wealth, the very basis of traditional social life is undermined. The economic inequalities between men become so great that man's basic equality imperceptibly transformed into a merchant and client relationship. It is then impossible for all members of the society to discuss together as equals with a common interest in the maintenance and development of society. The common interest has been at least partially replaced by two interests, those of the 'have' and those of the 'have-not. The unity of the society has been weakened because the quality of its members has been broken."
"Badiliko hili si tu ni la kiuchumi. Kwa kuleta uwezekano wa kulimbikiza utajiri kupitia fedha, kwa kuchochea moyo wa utundu wa kuotea jinsi ya kujikusanyia vitu, na kwa kuweka misingi ya 'hadhi ya kijamii' kwenye utajiri wa kimatiriali; msingi ule hasa wa 'desturi jamii--wa asili' unapotezewa. Uto-usawa wa kiuchumi kati ya watu, wajakuwa ni mkubwa kiasi kwamba ule msingi wa 'usawa wa kibinadamu' hukimbia jicho la tafsiri; ambavyo hubadilika kuwa ni uono wa kimahusiano baina ya 'bepari-mfanyabiashara' na 'mgema-uteja-biashara'. Basi yawa ni muhari kwa wanajamii kujadili kama watu waliosawa -- wenye maslahi mamoja katika udumishaji sura-jamii na maendeleo ya jamii. Maslahi ya pamoja ndiyo basi, kiaina, yameshagubikwa na maslahi ya namna mbili, ya wale 'wenye nacho' na wale 'wasio nacho. 'Umoja wa jamii' umeshadhoofishwa; kwa kuwa namna ya hadhi ya wanajamii wake imeshavunjika vipande viwili."
Sasa, hapa tunalo moja la msingi; 'fedha/sarafu' ni kitu cha kuvutia macho ya akili ya udadisi hasa. Ina mapelekeo ya moja kwa moja kwa tabia, uwezo, vitendo vya wanajamii katika hata miktudha ya siasa, uchumi na mazingira ilivyo ni sosholojia kwa mambo ya jamii. Hili halipasi kumshangaza mtu yeyote makini; maana hata katika jamii yetu tuna misemo kama 'Maskini hana tabia'--pata pesa tuijue tabia yako; Pesa ni sabuni ya roho--mwenye pesa siyo mwenzio n.k. Katika haya, tunaona kuna kigezo cha 'wakati na subira' katika 'pesa'--kila mtu huishi kwa tumaini--'One day, Yes!', iko siku yangu--Mtego wa noti.
Sasa katika jicho la 'Uono Mfumo', kisomo cha mfumo husika chaweza kufanyika ambapo 'sarafu' inaweza kutazamwa kama >
'maua' na vile vile ni namna gani 'yaua'<.... Mwalimu Nyerere, laiti kungelikuwa na mbadala kwa fedha na sarafu asingelisita kusema >
'Shilingi Yaua'<... Kwa hivyo, mbadala wake ulikuja kwa yeye kujitahidi kusisitiza njia za uzalishaji mali, biashara na uchumi kiushirika; na yeye alikuwa na namna ya kuona na kutafsri dhana ya mtu na maendeleo...
When we tried to promote rural development in the past, we sometimes spent huge sums of money on establishing a settlement, and supplying it with modern equipment, and social services, as well as often providing it with a management hierarchy. In other areas, we just encouraged young men to leave the towns for a particular rural area and then left them to their own devices. We did these things because we recognized that the land is important to our economic future, but we acted on the assumption that there was a shortcut to development in these rural areas. All too often, therefore, we persuaded people to go to new settlement by promising them that they could grow rich there, or the government would give them services and equipment which they could not hope to receive either in towns or in their traditional farming places. In very few cases was any ideology involved; we thought and talked in terms of greatly increased output, and of things being provided for the settlers.
Tulipojaribu kuinua nguvu kwa maendeleo vijijini siku za nyuma, wakati mwingine tulitumia fedha nyingi sana kwenye kuanzisha makazi, na kuyapelekea mitambo ya kisasa, na huduma za kijamii, na vilevile kuyapatia hiraki za menejimenti(utawala wa ngazi juu ya ngazi). Katika maeneo mengi tuliwatia moyo vijana kuhama mjini kwa ajili ya kwenda eneo hili na siyo lile la vijijini na kisha kuwaacha na vitu vyao vya mbinu-kazi. Tulifanya haya kwa kuwa tulitambua ardhi ni muhimu kwa mustakabali wetu wa kiuchumi, lakini tulifanya hivyo tukichukulia kwamba hakukuwa na njia ya mkato kwa maendeleo katika haya maeneo ya vijijini. Karibia mara zote, kwa hivyo, tuliwahimiza watu kwenda kwenye makazi mapya kwa kuwaahidi kwamba watakuwa matajiri huko, ama serikali ingaliwapa wao huduma na mitambo ambavyo wasingaliweza kupokea aidha mijini au katika sehemu zao mashamba ya kienyeji. Ni kwa kesi chache labda kulikuwa na kisomofikra chochote kuhusishwa; tulifikiri na kuzungumza kwa minajili ya ongezeko kubwa la vitokezi, na vitu vyakutoa kwa wakazi.
What we were doing, in fact, was thinking of development in terms of things, and not people. Further, we thought in terms of monetary investment in order to achieve the increase in output we were aiming at. In effect, we said that capital equipment or other forms of investment would lead to increased output, and this would lead to transformation in the lives of the people involved. The people were secondary; first priority was the output. As a result, there have been very many cases where heavy capital investment has resulted in no increase in output--where heavy capital investment has been wasted. And in most of the officially sponsored or supported schemes, the majority of the people who went to settle lost their enthusiasm, and either left the scheme altogether, or failed to carry out the orders of the outsiders who were put in charge--and who were not themselves involved in the success or failure of the project.
Tulichokuwa tukifanya, kwa kweli, ilikuwa ni kufikiria maendeleo kwa minajili ya vitu, na si watu. Zaidi, tulifikiri kwa minajili uwekezaji wa kifedha ili kufikia ongezeko katika vitokezi tulivyokuwa tukilenga. Kwa kukazia hili, tulisema kwamba mtaji, mitambo na namna zingine za uwekezaji vingaliongozea kwenye ongezeko la vitokezi, na hili lingaliongozea kwenye mageuzi katika maisha ya watu waliohusika. Watu walikuwa kwenye upili; kipaumbele cha kwanza ilikuwa ni vitokezi. Matokeo yake, kulikuwepo na kesi nyingi ambazo uwekezaji mtaji mzito uliishia kwenye 'pasi ongezeko' katika vitokezi--ambapo mtaji mzito uliowekezwa ulikuwa kana kwamba umetupwa jalalani. Na katika karibia skimu zote zilizofadhiliwa, wengi wa watu waliokwenda kukaa makazini walipoteza hamasa, na aidha waliondoka na kuacha skimu moja kwa moja, au walishindwa kufuatisha maagizo ya watoka-kungine waliowekwa kusimamia -- ambao wao wenyewe hawakuwa wanajihusisha katika mafanikio ama kuanguka kwa mradi.
Hili latupa picha ni namna gani, maendeleo nchini kwetu, baada ya uhuru wa kujitawala, yalianza kwa kutilia mkazo maendeleo ya vijijini -- umuhimu wa ardhi na kuzingatia kwamba idadi kubwa ya wananchi ilikuwa katika sifa, hadhi na mazingira ya vijiji; basi pia tumaini katika shughuli za kilimo na usimamizi wa mambo yake.
Sasa, kungine tumepata kuona pembetatu ya 'siasa za nchi', 'uwezo wa jamii' na 'mipango na utumishi' kama fremu-kazi ya 'uono mifumo'. Ni jinsi gani tunaweza kubayanisha kisomofikra cha Mwalimu Kambarage Julius Nyerere kina mapungufu katika miktadha ya kiuono mfumo--juu ya 'maendeleo' na 'stawi' ya nchi-taifa?
Kabla hatujaliangazia hili, ni vema tukatambua Mwalimu Nyerere alikuwa ni mtu mwenye Maono. Watu wenye maono, hutambuliwa na wenzao wenye maono ama upeo, na katika hili daima kuna kuheshiana kwa dhati na dhamira ya ushikiriano kwa mipango na utekelezaji wa hayo Maono, pia kuoneshana njia za kupita.
Utekelezaji wa Maono ni safari, ni mapito ya kutoka nyuma na kwenda mbele. Japo kwa akili ya kawaida watu hudhani 'maajabu ya safari' ni 'kuwasili' kulikolengwa--kuvuka mito na mabonde; hili si hivi kwa watu wa 'ufikirifu mifumo'. Kwa hawa, Maajabu ya Safari ni safari yenyewe...
Mwalimu Kambarage Julius Nyerere, wakati mmoja aliona ili nchi iendelee inahitaji 'watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora'... Walau fikara la ubayananishaji wa namna hii linaasili ya Uyunani ya kale--kupatwa kusemwa na >
mwanafalsafa Aristotle<. Uzoefu wa Mwalimu, kupitia yaliyosibu nchi-taifa kufika mwaka 1978, kulimfikishia busara ya jambo ambalo hata Mwanafalsafa Aristotle hakubarikiwa kupata kuwazia katika kipindi cha nyakati zake. Mwalimu aliona, utashi wa kisiasa pekee siyo jibu kwa maendeleo, ili nchi ipate maendeleo hatuna budi kuwa na taasisi zetu wenyewe za kuharakisha maendeleo vijijini na pia mijini. Hili lilipelekea kuanzishwa kwa taasisi ya mafunzo kwa wataalam wetu wenyewe kwa ajili ya mipango na maendeleo ya vijijini. >
Chuo cha Mipango cha Dodoma< ndiyo zao la fikra ile ya kimkakati ya Mwalimu. Na Chuo hichi kinamilikiwa na Wizara ya Fedha na Mipango.
Haya yanatutaka kutambua Ontolojia ya Taasisi na jitihada za kujengea jamii uwezo kupitia elimu.
Sasa, tawala ya nchi yetu ya Tanzania, ilivyo ni JMT, inaongozwa na katiba yenye kusisitiza ujenzi wa Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au chochote kati ya vyombo vyake na udugu na amani kutokana na kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ambayo inasisitiza utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira yaliyomo katika Jamhuri ya Muungano. Na kwa hiyo, Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake katika lengo la kuhakikisha, miongoni mwa mingine kadhaa,
KWAMBA:-
- 'Maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja';
- 'Kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuli yoyote ya halali inayompatia mtu riziki yake';
- 'Aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini';
- 'Matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi';
- 'Shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinaweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi';
- Nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya DEMOKRASIA na UJAMAA.
Kwa hivyo, kwa nini kungine >
tulimulika< suala katiba na sera katika kulijenga taifa.
Utumishi serikalini unaongozwa na sera; mipango yote ya kiserikali nayo hutekelezwa kwa misingi sera na Dira ya Maendeleo ya Taifa.
Dira yetu ya Taifa inamalengo ya 'kuibadili jamii kiuchumi, siasa, utamaduni' kuja kuendana na ulimwengu wa leo wa utandawazi na ushindani... Na ndani yake ndiyo huja lile shauri la 'maendeleo ya viwanda' kwa kuwa viwanda hufanya jamii kuwa na maisha tajiri, yakuridhisha, marefu ya kuishi, yaliyojaa fursa na sura anuai za mambo... Ujenzi na Upanuzi wa Miundo Mbinuni hatua za kimkakati zinazotuletea kutangamanisha fursa kwa Maendeleo ya Mjini na Vijijini...
Ujenzi wa Vituo vya Afya, Kuimarisha Huduma za upatikanaji wa Elimu, Maji na Nishati, Masoko na Mambo mengine kama huduma za kimahakama, sanaa, burudani na michezo si tu hutuletea msingi wa 'Maendeleo ya Kibinadamu' lakini yanajenga mizizi kwa ustawi wetu juu ya nchi na mazingira yake. Hili linafanya leo suala la maendeleo ya nchi lazima lijumuishe ulinzi na uhifadhi wa mazingira kwa kuwa sisi wanadamu tunaishi tukiyategemea mazingira, na hali, harakati zetu za kiuchumi na viwanda zaweza kuwa si salama kwa mazingira; na basi kutishia usalama wa vizazi vya kesho...
Hapa tunaoweza kuona kwamba, Katiba tuliyonayo, si tu inatambua umuhimu wa sera bora ili kuongoza utendaji wa kiserikali -- kwa ajili ya kuleta ustawi bora na mustakabli chanya wa taifa; lakini kuna mengine ya kuzingatia kadri tufanyavyo jitihada hizi.
Usawa unaweza kutajwa kadri ya mambo ya ulali wa 'siasa za nchi' kama kisomofikra kwa 'utashi wa kisiasa' juu ya haki, lakini katika sera ndiyo huleta dhana ya 'ikwiti', matunda ya utendaji wa serikali yalete manufaa kwa wanajamii wote bila kubagua. Haki-sawa-kimazingira kwa mfano inapelekea maana kuwa, ikiwa kuna madhara yajayo na harakati za kiuchumi na mazingira, miongoni mwa wanaoishi mijini na vijijini kwa mfano, basi isitokee jamii moja ndiyo inaathirika zaidi na huku nyingine 'ikipeta'. Haki-sawa-jamii kisera maana yake mapelekeo ya 'mizania ya kijamii' katika kufaidi mema ya nchi; isitokee mambo kwa mfano, watu wa mjini wanafaidika zaidi na huduma bora za elimu, afya, ufikiaji wa mitaji, barabara n.k kuliko wale wa vijijini. Haya yote kuwa ni sehemu ya masuala mtambuka katika sera za taifa -- katika mambo kama vile mazingira, mipango-miji, jinsia, maji, nishati, misitu, ardhi, makazi, idadi ya watu, makazi n.k
Sasa, sera za nchi, ni upande wa 'akili kubwa' wa tawala za nchi na maendeleo. Kwa namna ya visomo vyetu vya leo, tunamapungufu katika utungaji wa sera, utekelezaji na mapitio yake. Upande mmoja wa mkono shida yake inatokana uwezo wa kufanya stadi ili sera zetu zitungwe kutokana na >
shahidi za kivisomo<. Upande wa mkono wa pili, ni ukweli mchungu ambao hata wasomi wa leo wa mambo kama haya -- kutokuona kuwa namna zao za visomo zinamapungufu ya kimbinu. Elimu ya/na utafiti kwa siku za leo ina vikomo vya 'msaada'--katika kutuletea majawabu ya kweli kuhusu sura na mienendo ya jamii...
...
++++
...
Basi Mwalimu Nyerere alipotaja maadui watatu -- umaskini, ujinga na maradhi—alilizungumza hili kwa minajili ya walau adha mbaya ya kutokujua kusoma ama/na kuandika. Hili akilipambanua kama uhitaji kwa wanajamii waweze kutambua mahitaji yao—kupitia visomo na kutaarifika; na pia kuvijua ama kutambua vitu wanavyovihitaji kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao. Na basi hili pia ni kwa ajili ya kupanua mawazo yao ili waboreshe muktadha wa demokrasia na ufanyaji-maamuzi.
Ingawaje muktadha wa Mwalimu humo katika mashauri ya mawaidha ya kijichapicho cha ‘Utangulizi kwa Uhuru na Umoja’ na pia ‘Uhuru na Maendeleo’ yalijikita katika dhana za kumjenga mtu, ni wazi yeye alikuwa akidadavua mapelekeo ya ‘Uhuru na Kazi’. Yaliyo na uzito humo ni zile adha za watu, jamii, taasisi, utabia wa kishirika, uwezo na maamuzi juu ya kutekeleza siasa za Ujamaa na Kujitegemea.
Tuache kiporo mingine hayo, na tubakie na ‘elimu’ kama nyenzo ya kufanikishia ‘Uwezo wa Jamii’ ilivyo ni mabadiliko ama mageuzi katika jamii.
Katika muktadha wa elimu na kuelimika, kuna daraja la mawasiliano, ambavyo maarifa na ujuzi hutoka kwa mtu mmoja Kwenda kwa mwingine. Zamani, njia iliyokuwa mashuhuri kutumika ilikuwa ni kupitia vitabu, machapisho na maandishi. Siku hizi, kutokana na maendeleo ya sayansi na tekinolojia ndiyo tunanamna nyingi kuliko siku za mwalimu—mambo kama mifumo ya mawasiliano ya kimtandao na multimedia; watu wanaweza kuelimika kwa ufanisi na mapana zaidi kutokana na nyenzo za mawasiliano zinakwenda kwa sauti, maandishi, picha, video, uhuisho n.k.
Sisi Wabantu tunamsemo: Elimu ni Bahari…
HIli jambo makini sana kuzingatia, kwamba visomo na elimu labda havikomei na mifumo rasmi pekee; hivi huendelea hata katika mifumo isiyo rasmi… Dunia ya leo kwa sehemu kubwa imejikita katika ‘mifumo rasmi’ ya elimu—kuna namna binadamu wanapenda kurasmisha mambo kwa ajili ya ‘michezo’…
Hapa ndiyo tujue, tukiwa na uono na ufikirifu mifumo, hili ndilo lawa wazi na hasa kuakisi —michezo yetu ndiyo mauti yetu… Kwa kuwa Mtu wa ‘uono na ufikirifu mifumo’ anaweza kufikiria hata nje ya mfumo wa kawaida na kujiridhisha fasaha ya ukweli wa muktadha wa jambo hili; lakini tuliache kiporo kwa sasa na hapa…
Adha kuu ya Elimu 1.0 ni ‘vipofu kuongoza vipofu wenzao’… Je, ni kwa vipi hili ni kweli? Hili halina jibu kwa watu wenyewe wa Elimu 1.0… Mtu anaweza kusoma madarasa yote, akawa hata madigrii kama yote, lakini ikiwa yote haya ameyapata kupitia kwa Taasisi za Elimu 1.0, kuna namna hata yeye hana tofauti na mtu ambaye hajaenda darasani kabisa… Ukweli huu, haupaswi kushangaza mtu yeyote—ni mara ngapi wanajamii humuona msomi fulani jinsi ‘usomi wake’ haujamleta ‘busara’ yeyote? Akiongea—wala ‘hana maajabu’?
Kwa hiyo wapo wanajamii wanaitafuta elimu ya darasani kwa udi na uvumba ili waweze kujipambanua dhidi ya wenzao ambao ‘hawajabahatika’ ama ‘wamezembea’ ama labda wenye kuonekana kwa wao kuwa ni ‘vilaza’… Elimu 1.0 ni ‘mfariji’ kwa wanajamii wa asili hii; lakini kwa mtu wa ‘uono na ufikirifu mifumo’, hekima na busara si zao hasa la Elimu 1.0; hekima ni uwezo wa mtu kujua na kumudu >
kutangamanisha lile ‘analolijua’ na lile ‘asilolijua’<; mtu mwenye hekima anaweza kuishi na moyo wa furaha hata vile vichache anavyovijua, kadri sawa na mengi asiyoyajua kwa wakati…
Mashauri haya yaingie humu ili kuweka kumbukumbu sawa; kwa kuwa hata katika harakati zetu za kujipambanua kimaendeleo na ustawi wa jamii, kupitia mifumo na taasisi zetu, tunakuwa kama vile tunanusuru hili na kumbe hapo hapo tunachochea lingine...
Tumulike mawili matatu…
Maarifa yetu ya darasani katika nyanja zote za visomo, kuna namna ni 'mchezo wa kufuta lawama' ama 'kuvishana vilemba vya ukoka'--ya kwamba ni 'kuelimika' lakini yaweza kuwa hali tofauti ...
Watu wengi ni wenye visomo lakini elimu wanayojengea misingi ya kujivunia--labda kusema kuwa na cheti, digrii, uzamili ama uzamivu japo kiukweli haya yote ni finomena ya kijamii katika kushiriki uthamani fulani wa mambo unaoweza kuwa ni wa 'uongo na kweli'...
Kwa hapa nyumbani, tuseme, tukianza kuhoji haya 'yanayofundishwa' -- ikiwa yanatija hasa katika kutuendelea maendeleo ya kiutamaduni na ustawi, tutaweza 'kufumua na kuyasuka upya mafikara' yetu juu ya maisha, mtu, uhai na kazi. Kwa kuwa, tukiwa wakweli na nafsi zetu jambo litakuwa wazi--kuna ‘elimu ya kupewa’ na ‘elimu ya kujiongeza’...
Daima ni kupitia 'elimu ya kujiongeza' katika dhamira ya mtu mmoja mmoja, jamii hutanua wigo maendeleo na ustawi kama matunda ya mwangaza mpya wa maarifa kwa jambo/mambo. Hii ni pale mafikara ya mtu aliyepata mwangaza yanaposhawishi vitendo vipya na bora kwa shughuli, utendaji na udumumivu wa mambo.
Sayansi, kama somo--pamoja na sifa zote ambazo wasomi wa leo, wakubwa kwa wadogo, wanajengewa kuamini ina majibu ya msingi kwa kila kitu, kuna namna jambo hili ni >
'nusu ukweli' ulio ni hatari kuliko uongo taslim<.
Kuna mambo hata leo hii wengi hawajui, ama hayajawahi kuwafikia akilini, kuwa, kwenye sayansi na hata vitabu vyetu tunavyofundishia watoto sayansi--kuna porojo ya jambo/mambo kulengwa kwa wanafunzi/wakufunzi kuliko kuwaweka hao katika msingi na uwezo wa kujijengea ‘kweli’ zao wao wenyewe -- uwezo wa kuzidi vile walivyopangiwa kujifunza na hata kwa misingi ya 'vitendo vya kiuchunguzi'.
...
+++
...
Ni muhimu sana kwa jamii wa Waafrika, kadri itafutavyo ‘Sura ya Utambulisho Wake’ iwe na maarifa sahihi na ya kutosha juu ya mambo ya kijamii --juu ya ufungamano wa kiutamaduni, ama sivyo >
‘ubeberu wa kiutamaduni’< utawaandama ‘isivyo bahati njema’ ule umma wa watu wake.
Utamaduni mmoja unaweza kumezwa na mwingine kwa kuwa tu ‘ufunguo wa ufunuo’ umepotea na basi jamii moja ikatawaliwa na nyingine kwa ‘hiari ya mlango wa nyuma’… Ndilo hasa linaweza kufanya watu taifa moja ‘kujiona si bora kuliko wengine’ kwa kuwa tu hao wana ‘utamaduni’ ama ‘ustaarabu’ wenye kupendeza machoni, wenye koherensia na mambo yake juu ya nyumba, makundi ya kaya, jamii, taifa, udugu, visomo, nidhamu na maadili… Kimsingi hivi ni sehemu ya jamii yoyote, lakini kwa wakati, jamii moja inaweza kuwa imekwisha nufaika mbali kuzidi nyingine kiuchumi na tawala; basi ikikutana na nyingine ’iliyo nyuma’ basi itakuwa na ‘ushawishi’ kwa mabadiliko—hasi ama chanya.
Hata mfumo wa elimu unaweza kupotoshwa kw akule kufananisha huo na jambo la ‘Ufunguo wa Ufunuo’; na kumbe huo bado ni ‘galasha’ la ‘mchezo’. Ufunuo ni muktadha wa ‘Elimu 3.0: Ilimu ilivyo ni Metafizikia ya Elimu’, ambapo ‘Elimu 2.0: Uono na Ufikirifu Mifumo’ ni kiungo kati yake na ‘Elimu 1.0: Kujua Kusoma na Kuandika’.
Haya yatukumbushe busara ya Mtawala Haile Selassie, maendeleo yetu hapa barani Afrika hayana budi kuwa ni ya vitu na watu; tukipuuza kimoja daima tutajikuta ni mateka wa staarabu kutoka nje; ambazo zitazotibua hata jitihada zetu za kuitafuta ‘kweli na neema ya utu wetu’ kwenye mazingira yetu.
Tukipuuza maarifa ya kiroho basi tunaweza kuyumbishwa na ile tamaa ya mapenzi ya mali na ulafi wa kimagharibi… Tukipuuza maarifa ya vitu, sayansi na uhandisi, basi tunaweza kunasibika na ‘siasa za wivu’ ama ‘jicho la husda’ kwa wengine wenye kuishi Maisha ya mali na ‘pepo ya duniani’… Tunaweza hata kupotoka na >‘akili ya kimaskini’< inayoweza kujengekea ‘akilini na mioyoni’ mwetu kutokana na mapokeo ya dini na Imani za mataifa mengine – kwa kule ‘kujihesabia haki’ katika maisha mengine yenye kudhanika ama kusadikika kuwepo mbali na dunia hii. Hili linaweza hata kutumika dhidi yetu, kiuchumi na tawala, kimfananishano wa faida za mambo na mipango – sisi wabantu tuna msemo, ‘Ukisusa, wenzio twala’…
Ni vema tuwe na hekima ya kutangamanisha mambo ya dunia na mambo ya kiroho, lakini pia tuchunguze akili na mioyo yetu wakati wote, pasi kusahau ukweli wa kwamba kila mtu kazaliwa pekee yake kabisa… na atakufa pekee yake kabisa. Yote ya ubinadamu fikra, usadikifu, uono, taasisi, mifumo na utamaduni ni mambo ya ‘wepesi’ kimaisha ya mafungamano, lakini si lazima yawe ndiyo ‘ukweli’ wa jambo juu ya uzima wote.
‘Ukweli Hasa’, daima na milele, ni jambo la ‘kuiva kwa tunda la imani katika hakika’-- ile ya mtu mmoja mmoja… Ni ‘ufunuo kamili’ katika mtu isivyokutegemea la kusikia, kuambiwa, na wala kuandikwa popote; ila basi mtu mwenyewe kufanyika ‘moja’ na ‘kweli’ yenyewe…
Kila mtu ni vema atafute ‘Kweli’ imfaaye yeye kama mtu, juu ya uzima wake na hata kupitilizia mbali ya mauti yake, huku azingatia kwamba: ikiwa ‘njia yake ya kuitafuta kweli’ inalandana na mwenzake—‘basi kheri’, ikiwa ni tofauti -- nayo pia ‘kheri’; labda kuna namna mbele ya safari njia zote huishia ‘kumoja’ -- labda ni adha ya Elimu 1.0; mtu akiwa Elimu 2.0 huanza kubaini ‘alama oanifu’ kwa ‘wasafiri’ wote – almradi tu hao kuwa kwamba ‘wameongozeka vema’ katika ‘nia na mapenzi mema juu ya wanadamu, dunia na kile ‘Kilicho ni Hasa’’?… Basi ni vema kila mtu kuwa na ‘akiba ya maneno’, kutoingiliana wala kusakamana, basi tuwe na kuheshimiana, kujaliana na Imani juu yale yote yanabeba makusudi ya upamoja wetu, kwa mfano, misingi ya nchi-taifa—kama ‘Mwanzo’…
...
-_-