Kwa wataalam wa sheria masaada unahitajika

Kwa wataalam wa sheria masaada unahitajika

bafetimbi

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2018
Posts
1,085
Reaction score
1,741
Habari wadau, natumai mko vizuri....

Iko hivi, kuna mshkaji wangu mmoja hivi yeye yuko mwanza huko.

Juzi jumaatatu alitangaza kuuza simu yake kwenye mtandao flani wa hapa bongo.
Sasa anasema ni watu wengi waliipenda Ile simu Ila kikwazo ni kwamba walikuwa wakiuliza kama ana risiti ya simu pamoja na box lake na pia emai ya risiti ifanane na ya kwenye simu ndiyo watainunua bila shida lakini kwa bahati mbaya jamaa yangu risiti na box la simu alishavipoteza kitambo kidogo Ila simu alinunua kwenye Duka kubwa tu la muuzaji mkubwa Sana wa simu pale mwanza na siku ananunua tulikuwa nae Ila Mimi kwa sasa sipo mwanza.

Jamaa anasema akatokea dada mmoja akaonesha uhitaji Sana wa hiyo simu kwa bei waliyokubaliana ilikuwa ni simu Aina ya REDMI NOTE 10pro ambapo walikubaliana wakutane jana na huyo dada kwajili ya mauziano rasmi.

Jamaa anasema mida ya asubuhi wakawasiliana na yule dada ili waonane kumbe Yule dada baada ya kuusoma mchezo kuwa mwamba Hana risiti demu akawahi kituo cha polisi Pale mwanza na kuripoti kuwa Kaibiwa simu akaitaja Ile Ile ya mshkaji na mwizi wa hiyo simu yake aka mtaja mshkaji pia na mpaka rangi ya simu aliitaja ileile maana aliona picha za simu jamaa alizopost wakati ananainadi bidhaa yake.

Sasa kumbe wakati yule demu anaenda kuonana na jamaa kwajili ya makabishiano aliongozana na polisi kama wanne hivi wamevaa kiraia mshkaji akatiwa mikononi mwa polisi na kubebwa juu juu mbele za watu maana walikubaliana waonane barabarani kisha watulie sehemu demu aikague simu ili kama ataridhika nayo basi aichukue.

Mchizi anasema alisombwa juujuu hadi kituoni akituhumiwa kumwibia huyo dada hiyo simu na kama simu ni yake alinunua basi aoneshe risiti ya hiyo simu kama anayo na wakati huo jamaa anasema demu alikuja na karisiti
kake mchizi hajui demu amekatoa wapi hako karisiti na akawapa wale Askari kale karisiti.

Lakini cha ajabu mshkaji Kila akiomba risiti ya huyo demu aiangalie kama ni ya hiyo simu kweli polisi waligoma kumuonesha wakabaki wameishikilia wenyewe na kumwambia mchizi aende Duka aliponunua hiyo simu huwa wanabaki na kopi za risiti pindi unapoinunua ikiwa mpya na wanaandika kwenye kompyuta watampa ili aipeleke hapo central police waangalie emai za risiti na simu na pia wajue Nani tapeli Kati ya mchizi na huyo demu wa mjini

Na demu kakomaa kwamba simu ni yake na mchizi ndo aliyemwibia huku akaonesha yeye anarisiti yake ambako ni karisiti uchwara sasa na mchizi hajui huyo demu kachongesha wapi hako karisiti.

Sasa wadau kama kuna aliyewahi kukutana na kesi ya kubambikiwa na kutaka kutapeliwa namna hii je hili swala linasoviwa vipi!!?

Je mchizi akienda pale tuliponunua simu kweli atapewa hiyo kopi ya risiti yake ama hizo kopi zinakuwaga hazipo. Maana sasa mchizi anatuhumiwa kuiba simu yake mwenyewe kisa hana risiti.

Kisheria hii ikoje wadau. Na je ikibainika kwamba demu ni muhuni jamaa anaweza akamfungulia mashtaka huyo demu?

Mods tafadhali naomba mnirekebishie spelling za tittle hapo juu ni msaada na sio masaada kama nilivyoandika.

Ahsante.......
 
Hii kesi itahitajika nguvu ya pesa coz kesi za wizi wa simu ni chaka la Polisi kupiga pesa.
Sasa mchizi simu hajaiba tulienda Mimi na yeye kununua shida hapo ni risiti, sasa dukani wanaweza kubaki na kopi ya risiti yenye emai namba za Ile simu au ndiyo demu anakula njama na hao polisi na mchizi ataingizwa chaka!!!!?
 
Mbona kama vile ni wewe umeipiga hiyo simu jombaa? 🤔
Hahahaha jombaa siwezi kumfanyia hivyo mwana Ila Tu imeniuma maana wakati mchizi ananunua tulikuwa nae na zilimtoka Dola nyingi tu.
 
Habari wadau, natumai mko vizuri....

Iko hivi, kuna mshkaji wangu mmoja hivi yeye yuko mwanza huko.

Juzi jumaatatu alitangaza kuuza simu yake kwenye mtandao flani wa hapa bongo.
Sasa anasema ni watu wengi waliipenda Ile simu Ila kikwazo ni kwamba walikuwa wakiuliza kama ana risiti ya simu pamoja na box lake na pia emai ya risiti ifanane na ya kwenye simu ndiyo watainunua bila shida lakini kwa bahati mbaya jamaa yangu risiti na box la simu alishavipoteza kitambo kidogo Ila simu alinunua kwenye Duka kubwa tu la muuzaji mkubwa Sana wa simu pale mwanza na siku ananunua tulikuwa nae Ila Mimi kwa sasa sipo mwanza.
Huyo demu aliibiwa lini hiyo simu?
Je aliripoti kituo chochote cha polisi?
Na aliripoti lini?
 
Huyo demu aliibiwa lini hiyo simu?
Je aliripoti kituo chochote cha polisi?
Na aliripoti lini?
Mchizi anasema hawakutaka hata kumsikiliza Ila Tu walimwambia aende aliponunua simu na apewe kopi ya risiti sasa wasiwasi wake ni kwamba je hizo kopi za risiti ni kweli zinabaki madukani maana like ni duka kubwa Sana la simu na mwenye duka ni muuzaji maarufu.
 
Jamaa alikuwa anauza Mali ya wizi, binti ya bro wangu alishaipata simu yake huko mitandaoni baada ya wezi kuinadi na kuipiga picha, polisi walimuamini coz mpaka kuna scratch zilizokuwa ndani ya simu aliweka alama walizikuta! Initial za majina yake manne!

Jamaa yako awe mkweli, else atapoteza hela, muda na hiyo simu, Ka kweli ni ya kwake!
 
Mbona simple wakati ananunua alipewa risti Gani ya mkono au efd?

Km duka halina janjanjana risti anaipata ila km zile zenye vitabu vingi hapo imekula kwake
 
Mbona simple wakati ananunua alipewa risti Gani ya mkono au efd?

Km duka halina janjanjana risti anaipata ila km zile zenye vitabu vingi hapo imekula kwake
Nilikuwa nae alipewa risiti ya efd
 
Back
Top Bottom