Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
1. Nenda dukan umuombe akusaidie kupata report ya mauzo ya Ile siku umeenda kununua na muda pia uzingatie,Nilikuwa nae alipewa risiti ya efd
Kesi rahisi hiyo, kama anakumbuka tarehe aende dukani au aende TRA baada kutoka dukani.Nilikuwa nae alipewa risiti ya efd
Policcm wanalijua hili kweli? Hapo jamaa akizubaa atapigwa pesaHapo hakuna haja ya risti hio kesi ni rahisi sana police wana kitengo cha Cyber wana trace sim card ipi imetangulia kutumika kwenye hio simu kati ya huyo jamaa yako na ya demu case closed
Akitaka anaweza.Nitamshauri jamaa awaambie polisi hicho kitengo cha cybe kifanye kazi yake. Na vipi hapo ikitambulika demu alikuwa anajaribu kumtapeli jamaa kisa hana risiti je mshkaji anaweza kumfungulia huyo dem mashtaka ya udhalilishaji? Maana jamaa anasema alibebwa juujuu kama mwizi toka mtaani kwao hadi kituo cha polisi anasema ilikuwa ni aibu kubwa sana kwake pale mtaani anapoishi.
Mbona rahisi hilo polisi wanalimaliza mapema, waandike barua kujua namba iliyotumia hiyo simu muda fulani watajua nani mkweli
Huyo jamaa yako aende dukani aliponunua wanabaki na kumbukumbu kibao.Akumbuke tarehe na mazingira yalibyokuwa siku hiyo.Ikibainika demu anadanganya,hiyo ni jinai polisi warare naye mbele ila Nina wasiwasi huenda polis wamekula Mchongo na huyo dada.Kama vipi atafute mwanasheria ampe msaada.Kwanini hawataki jamaa aikague risit na simu?Habari wadau, natumai mko vizuri....
Iko hivi, kuna mshkaji wangu mmoja hivi yeye yuko mwanza huko.
Juzi jumaatatu alitangaza kuuza simu yake kwenye mtandao flani wa hapa bongo.
Sasa anasema ni watu wengi waliipenda Ile simu Ila kikwazo ni kwamba walikuwa wakiuliza kama ana risiti ya simu pamoja na box lake na pia emai ya risiti ifanane na ya kwenye simu ndiyo watainunua bila shida lakini kwa bahati mbaya jamaa yangu risiti na box la simu alishavipoteza kitambo kidogo Ila simu alinunua kwenye Duka kubwa tu la muuzaji mkubwa Sana wa simu pale mwanza na siku ananunua tulikuwa nae Ila Mimi kwa sasa sipo mwanza.
Jamaa anasema akatokea dada mmoja akaonesha uhitaji Sana wa hiyo simu kwa bei waliyokubaliana ilikuwa ni simu Aina ya REDMI NOTE 10pro ambapo walikubaliana wakutane jana na huyo dada kwajili ya mauziano rasmi.
Jamaa anasema mida ya asubuhi wakawasiliana na yule dada ili waonane kumbe Yule dada baada ya kuusoma mchezo kuwa mwamba Hana risiti demu akawahi kituo cha polisi Pale mwanza na kuripoti kuwa Kaibiwa simu akaitaja Ile Ile ya mshkaji na mwizi wa hiyo simu yake aka mtaja mshkaji pia na mpaka rangi ya simu aliitaja ileile maana aliona picha za simu jamaa alizopost wakati ananainadi bidhaa yake.
Sasa kumbe wakati yule demu anaenda kuonana na jamaa kwajili ya makabishiano aliongozana na polisi kama wanne hivi wamevaa kiraia mshkaji akatiwa mikononi mwa polisi na kubebwa juu juu mbele za watu maana walikubaliana waonane barabarani kisha watulie sehemu demu aikague simu ili kama ataridhika nayo basi aichukue.
Mchizi anasema alisombwa juujuu hadi kituoni akituhumiwa kumwibia huyo dada hiyo simu na kama simu ni yake alinunua basi aoneshe risiti ya hiyo simu kama anayo na wakati huo jamaa anasema demu alikuja na karisiti
kake mchizi hajui demu amekatoa wapi hako karisiti na akawapa wale Askari kale karisiti.
Lakini cha ajabu mshkaji Kila akiomba risiti ya huyo demu aiangalie kama ni ya hiyo simu kweli polisi waligoma kumuonesha wakabaki wameishikilia wenyewe na kumwambia mchizi aende Duka aliponunua hiyo simu huwa wanabaki na kopi za risiti pindi unapoinunua ikiwa mpya na wanaandika kwenye kompyuta watampa ili aipeleke hapo central police waangalie emai za risiti na simu na pia wajue Nani tapeli Kati ya mchizi na huyo demu wa mjini
Na demu kakomaa kwamba simu ni yake na mchizi ndo aliyemwibia huku akaonesha yeye anarisiti yake ambako ni karisiti uchwara sasa na mchizi hajui huyo demu kachongesha wapi hako karisiti.
Sasa wadau kama kuna aliyewahi kukutana na kesi ya kubambikiwa na kutaka kutapeliwa namna hii je hili swala linasoviwa vipi!!?
Je mchizi akienda pale tuliponunua simu kweli atapewa hiyo kopi ya risiti yake ama hizo kopi zinakuwaga hazipo. Maana sasa mchizi anatuhumiwa kuiba simu yake mwenyewe kisa hana risiti.
Kisheria hii ikoje wadau. Na je ikibainika kwamba demu ni muhuni jamaa anaweza akamfungulia mashtaka huyo demu?
Mods tafadhali naomba mnirekebishie spelling za tittle hapo juu ni msaada na sio masaada kama nilivyoandika.
Ahsante.......
Hatakiwi kuwa mnyonge kama ni haki yake apambane na hao policeKumaliza kesi kirahic hivyo hawataki coz wanataka rushwa tu
Hivi risiti za simu zinakuwaga na IMEI namba za simu husika?Huyo jamaa yako aende dukani aliponunua wanabaki na kumbukumbu kibao.Akumbuke tarehe na mazingira yalibyokuwa siku hiyo.Ikibainika demu anadanganya,hiyo ni jinai polisi warare naye mbele ila Nina wasiwasi huenda polis wamekula Mchongo na huyo dada.Kama vipi atafute mwanasheria ampe msaada.Kwanini hawataki jamaa aikague risit na simu?
Hiyo waifrush halafu kila mtu ajaribi kufungua kwa Email yake tuone nani mmilikiHivi risiti za simu zinakuwaga na IMEI namba za simu husika?
Waandike kwenda wapi?Mbona rahisi hilo polisi wanalimaliza mapema, waandike barua kujua namba iliyotumia hiyo simu muda fulani watajua nani mkweli