Kwa watu wa mkoa wa Mara

Kwa watu wa mkoa wa Mara

kweli wachaga wanajali mkoa wao na kupenda vya kwao,baada ya serengeti kujenga kiwanda cha bia Moshi bia za TBL zimekosa wateja,wote wanakunywa bia za serengeti,wanasema KIWANDA CHETU BIA ZETU!
 
Kwa kweli Mkoa wa Mara umetelekezwa sana kuna kipindi nilikuwa Mwanza wakati wa msimu wa kuwinda tulikuwa tunakwenda serengeti kuna hotel moja inaitwa Kijereshi Tended Camp, ipo mbugani tunapumzika hapo kama wiki siku ya kuondoka tunaingia porini kuwinda wanyama kibali tumekata Mwanza...kuna rafiki yangu alikuwa anatoka Musoma Mjini anakuja Lamadi nampa nyama anarudi Musoma.
 
Samahani ni makosa tu madogo,ni draft ya Muungano wa Vijana wa Mara(MUVIMA).Utanisamehe wakupita.

Accepted,sasa kama alivosema mjumbe mmoja hapo chini angusha hio katiba tuone malengo yake,muelekeo and the rest ili tukubaliane ikasajiliwe,sio unaisajili on one eye watch only!
 
Habari zenu ndugu zangu wa MARA. Mimi si wa mkoa wenu lakini nafanaya kazi kwenu. Ninyi mmejaa ukabila sana. Wala msilalamikie watu Viongozi kwamba wanaona uharibifu lakini hawaufanyii kazi. Ukiondo Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa, viongozi wengi wa kuchaguliwa ni lazima watoke Mkoa wa Mara, lakini mbona hawawasaidii lolote? Tatizo ni Ukabila.

MWITA (wa CHADEMA) aliwahi kuwa Kiongozi wa Magamba akiwa Tanga...lakini ninyi hamuwezi kumruhusu mtu wa Mkoa mwingine mwenye uwezo wa Kuongoza akawaongoza, huo ni UKABILA NA UMIMI. Musoma hawezi mtu kuwa kiongozi kama si MJITA AU MKURYA. Huo ni UKABILA NA UMIMI.

Kuna mtu Musoma anaitwa MKOREA au TONGORA...yeye ana-organization yake inatoa Scolarship, lakini lazima uwe umetoka kijijini kwake....huo ni UKABILA NA UMIMI.

Kwanza ondoeni Ukabila na Umimi kisha manaweza kupiga hatua....mnaweza kuanzisha umoja halafu watu watahoji, je kiongozi ni Mjita au Mkurya? Hiyo ni hatari.

Mi napita tu!!!!
 
Waambine wasomi wenu warudi Mara. Wote wamekimbilia DSM tu.

By the way hilo tatizo la Mara ni la Mwanza pia.
 
Kwa kweli Mkoa wa Mara umetelekezwa sana kuna kipindi nilikuwa Mwanza wakati wa msimu wa kuwinda tulikuwa tunakwenda serengeti kuna hotel moja inaitwa Kijereshi Tended Camp, ipo mbugani tunapumzika hapo kama wiki siku ya kuondoka tunaingia porini kuwinda wanyama kibali tumekata Mwanza...kuna rafiki yangu alikuwa anatoka Musoma Mjini anakuja Lamadi nampa nyama anarudi Musoma.

We jamaa ni mtu wa "system", hainwezekani uzijue sehemu zote hivi hivi tu. By the way ni juzi tu nimetoka Musoma, hakika panasikitisha, cha maana kinachofanyika ni ukarabati tu wa barabara ya Musoma-Mwanza
 
Jamani ndugu zangu mkoa wetu hauna tatizo, tatizo ni mfumo uliokuja kutuweka kando wa nchi hii na wale waliobaki wengi wao wakawa ni kama limbukeni wa kupenda maisha ya kipwani na kusahahu tulikotoka... Tunalalamika wachaga, kamwe hawako na hawatokuwa kama sisi. Kikubwa tuache ushamba wa kudhani maisha ni Dar es Salaam, Arusha na Mwanza pekee bali hata Musoma kuna maisha tena ya raha.
Vitu vya msingi ni kuwa tufanye mambo yenye manufaa kwa mkoa wetu, nashauri:
tushawishi uongozi wa nchi hii tupate angalau hata Chuo Kikuu kimoja (hii ni kwa Mara na kanda ya ziwa nzima), hospitali ya Kwangwa ijengwe, tupate vyuo vizuri vya utalii, zao la pamba lifanyiwe mapinduzi ya kilimo kiwe cha kisasa, tuweke mkakati wa kielimu kuhakikisha shule zetu zinatoa wanafunzi wenye uelewa na ufaulu mzuri (wanafunzi wa shule zetu nyingi wanapata DIV IV na 0), tuwape uhuru wanawake wa kujishughulisha na shughuli za kimaendeleo (wivu wa kimapenzi na udikteta kwa akina mama ukomeshwe) mengine ntaongeza kadri ntakavyopata wasaa.
Asante mtoa mada,, ubarikiwe sana kwa kuonesha kuguswa na hili jambo.
 
Saganka angusha hiyo draft ya katiba watu watoe comment rather than rushing na kusajili umoja.
Omongoreme,cjui wa kenyamonta,iramba,mesaga,majimoto ghasi Mwibhara.Usiwe na haraka tata,ushauri wenu nimeuchukua,wa kwamba watu waipitie kwanza draft kabla sijasajili.Nawaahidi,natafuta nafasi nitawatangazia ni lini tukaijadili draft hii kwa pamoja.Na members mtapendekeza venue.I'm serious.
 
Kwa kweli Mkoa wa Mara umetelekezwa sana kuna kipindi nilikuwa Mwanza wakati wa msimu wa kuwinda tulikuwa tunakwenda serengeti kuna hotel moja inaitwa Kijereshi Tended Camp, ipo mbugani tunapumzika hapo kama wiki siku ya kuondoka tunaingia porini kuwinda wanyama kibali tumekata Mwanza...kuna rafiki yangu alikuwa anatoka Musoma Mjini anakuja Lamadi nampa nyama anarudi Musoma.
Kwa mara ya kwanza naungana na wewe vilivyo.Katika kuujenga mkoa wetu tunakukaribisha hata kama orign yako sio mara,nitawatangazia siku ya kuwa na kikao cha mapitio ya draft ya katiba.
 
We jamaa ni mtu wa "system", hainwezekani uzijue sehemu zote hivi hivi tu. By the way ni juzi tu nimetoka Musoma, hakika panasikitisha, cha maana kinachofanyika ni ukarabati tu wa barabara ya Musoma-Mwanza

Mkuu mie muangaikaji tu...Musoma nimepafahamu kutoka na maisha tu, wasalimie sana jamaa wa Mkendo kati, Makoko na Mwigobelo.
 
Hapo kwenye red, inanishangaza sana kwani yule mzungu "PAUL" akija na timu yake wanaua wanyama ovyo mamia kwa mamia, wanaondoka na ngozi na vichwa tu. Sisi wakazi wa hapo tukigusa hata sungura unapigwa risasi. Jamaa hawa wana hela sana hata mkuu wa nchi analijua hili. Hoteli yao ndiyo imeshika namba moja kwa ubora duniani.

hapo kwenye nyeusi, ile hoteli ni kweli ni ya mkuu wa kaya inaitwa BILILA

Hapo ndo unataka kunichekesha mpaka mbavu ziniume bure, wale Wanatta, Waikoma na Waisenye wao wakishasikia Paul Jones alimaarufu PTJ kaingia ndio pona pona yao.Wanaenda getini kusubilia wale wanyama anaowatungua wao wanagawana nyama lakini wao sasa wakanyage kwenye mbuga ndo watakijua cha moto yaani kama vile Jones kanunua mbuga yote kwa hiyo akija anafanya anachokita hakuna anaekohoa yeyote.Chezeya pesa wewe hata mkuu wa Wilaya anaomba apointment kuwonana na tycoon. Ujanja hamna ataendelea kuwanyanyasa maana si mnataka awajengee uwanja pale maeneo ya Nyichoka sasa mtafanyeje lazima mtii. Na kama hujui uwanja wenyewe ungewaletea sana fursa watu wa Mara lakini watu wa Arusha wanaupiga vita eti utaua Kilimanjaro International Airport na kwa kuwa wapo makini kuliko wana Mara wenzangu wanaweza wakashinda na suala la uwanja likawa historia
 
Mwaka juzi kuna viongozi wa serikali waliosindikiza mwenge walitafutiwa kitoweo na askari game porini, mzungu akakataa akawapa hela wakanunue ng'ombe,
 
Mwaka juzi kuna viongozi wa serikali waliosindikiza mwenge walitafutiwa kitoweo na askari game porini, mzungu akakataa akawapa hela wakanunue ng'ombe,

Ni kujizalilisha tu hamna lingine maana kila mtu anafikiri eti mzungu ni kila kitu kwanza wale wazungu wenyewe ni makaburu so wana njaa kuliko hata sie maana hata tonge linalodondoka wanaliokota.Hapo kama walitoa ng'ombe mmoja walimwandikia tajiri kuwa wametoa ng'ombe 10 kwa ajili ya kusuport mbio za Mwenge na pia wanapiga picha kama vielelezo.So ukiajiliwa pale unatakiwa ujue kupiga picha hahahaha I love Mara especially Serengeti and Tarime districts maana ndo naona kuna vimbwanga sana.Watu wa huko ni maskin lakini wamekalia fursa na hawajui kama wamezikalia ndo shida.
Na mbaya zaidi nyie vijana wa mkoa huo wa Mara mkishasoma hamtaki kurudi kwenu kuijenga Mara kwa hiyo msilalame, mi chuoni nilisoma na kijana flan wa Mara nilivopata job huko kukatokea kazi nyingine nikamuunganisha akaniambia kuwa hawezi kurudi Mara kwa kuwa hatapata heshima kama Mkurya alieko Dar, nikamwambia maisha ni kujipanga aje tupige mzigo hata kwa miaka miwili then tusepe akagoma kabisa.Mwenzio nimechuma Mara nimerudi kulia Dar kiulaini na yeye bado anahangaika na Dar yake tu
 
Tusaidiane kuonyeshana hizo fursa kaka.
 
Eni wa Iramba mura,
Omongoreme,cjui wa kenyamonta,iramba,mesaga,majimoto ghasi Mwibhara.Usiwe na haraka tata,ushauri wenu nimeuchukua,wa kwamba watu waipitie kwanza draft kabla sijasajili.Nawaahidi,natafuta nafasi nitawatangazia ni lini tukaijadili draft hii kwa pamoja.Na members mtapendekeza venue.I'm serious.
 
WildCard umesema jambo muhimu nililosahau,tunawadharau wahaya,lakini hawa jamaa ni wazalendo,wanajenga kwao nyumba nzuri,mjini wanajenga za biashara.Sisi tumekuwa limbukeni mno.Tumebaki kubaguana kikabila,vikabila vyenyewe vidogo,halafu maskini sana,shida tupu.Nimeandaa katiba,nataka nipate reg. ili tuanzishe muungano wa vijana wa Mara,naomba mniunge mkono.

Nimewasoma. Yote ni heri ila hilo hapo juu la katiba ya ubaguzi wa kuwabagua wasio vijana halitatuvusha! Liangalie upya wewe mwenye katiba yako.
 
Mura "SAGANKA" mimi nakuunga mkono 100%. Mimi binafu ni mkurya wa Nyamongo ila nimejenga Bunda. Nipo Bunda huu ni mwaka wa Tatu sasa, nilipo hamia Bunda ndugu na jamaa walikuwa wanasema kukame, hakuna maji, wilaya maskini na mengi mengineyo. Kiukweli naomba niwaeleze kuwa Bunda siyo wilaya masikini hata kidogo na wala siyo kame kama inavyosemekana. Nilijaribu kufanya research ni kwa nini sifa hizi mbaya zinaelekezwa Bunda nikagundua kuwa hii ilikuwa ni propaganda ya watu waliohofia umaarufu wa Bunda kama ingesifiwa ingeliweza kuwa makao makuu ya mkoa wa Mara na kuleta ramani ya maendeleo. Kumbuka Bunda iko katika ya mkoa wa Mara ambapo wilaya zote za mkoa huo zina access nayo, mbuga ya serengeti, ziwa victoria na mengi mengineyo. Natumaini kwa great thinker mtajua nikisema kuwa kama wilaya ya Bunda ingepewa kuwa makao makuu ya mkoa wa mara, leo hii ingeitwa jiji, make uwepo wa mahoteli ya kitarii Arusha ungekuwa na utata pai na vyuo vya utalii na mambo mengine yanayo husu mbuga ya Serengeti. Naomba tutafutane na kuangalia hiyo katiba ya vijana wa mkoa wa Mara ili kuangalia mapungufu yake kabla ya reg. yake. Kwa sasa nipo nje ya mkoa wa Mara ntakuwepo Bunda kuanzia katika ya mwezi wa 11.2012.
 
Back
Top Bottom